hiv kwa maisha ya vijana hili linawezekana kweli
Nini kilichopelekea vijana wa siku hizi wasiweze??
Kwa sasa hivi tumeamua kubadilisha mambo na kuwa kinyume chake.. Sasa hivi mtu anasifiwa kwa idadi ya wanaume au wanawake aliolala nao.
watu wanatoa sababu za tamaa, tabia, n.k
lakini ni nani ambaye hana tamaa; ni nani anayependa kuona au kuolewa na mwenye tabia mbaya?
Ninachokiona mimi ni kuwa
1.kwa sasa, kadiri siku zinavyokwenda ndoa inazidi kuwa ni gharama, nikimaanisha kwamba mchakato mzima wa kuoa umekuwa ni mgumu kutokana na masharti kama vile mahari, na gharama nyingine za harusi.
Hiyo inapelekea wengi watafute njia mbadala - (yaani kupunguza hamu tu )
2.elimu na uelewa umekuwa mwingi, sana sana kwa upande wa wanawake ambao sasa wamekuwa makini kutokuingia ndoa kichwa kichwa.
3.utandawazi pia umechangia kwa namna fulani; kwani kila mtu anataka
"kujaribu" kile anachokiona au kusikia aone kuna nini
4. Kwa sasa mafundisho kutoka kwa mabibi na mababu hayapo tena. Pia mafundisho ya dini mbali mbali hayajatiliwa msisitizo na wafundishaji -
Pia kwa maisha ya sasa wengi tumeacha mahudhurio kwenye nyumba za ibada, kwa hiyo hakuna tena hofu ya Mungu - ya kusubiri ndoa.