Mungu ameumba!!!!

Mungu ameumba!!!!

Tatizo ni kuita uasherati/umalaya 'NGONO' ,kwa maana kwa Mungu iwe ngono,iwe ngomo,iwe ng'ono yote ni umalaya ama uasherati,lakini pia tumeelekezwa ni akina nani wafanye tendo la ndoa na si 'kufanya mapenzi' kama mnavyoita nyinyi siku hiziMungu anataja 'tendo la ndoa' kwa maana liwe ni tendo kwa wanandoa TU,sasa leo wakwale nao wanafanya hili tendo,ni sawa?mbali ya hivyo tumeambiwa hili tendo ni la siri,sasa leo ni wapi kuna siri?make watu mna...kama mbwa nje njesasa kama mnaamua kuliita tendo LA NDOA ni kufanya MAPENZI tayari hilo ni kosa kubwa sana,kwa maana tumelitia najisiNionavyo mimi!
Nimeipenda hii!you well analyesed(sijui nimekosea kiingereza)
 
Mi nna mwaka wa 13 tangu nimeoa, na sijaona machungu ya mapenzi. kwani wenzangu hayo machungu yanatoka wapi?
Tatizo lenu ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu, watu hawataki kuacha baba na mama na kuambatana na mke/mme, kubebana na ndugu ndo chanzo cha machungu ya ndoa.
 
Nini kilichopelekea vijana wa siku hizi wasiweze??

Kwa sasa hivi tumeamua kubadilisha mambo na kuwa kinyume chake.. Sasa hivi mtu anasifiwa kwa idadi ya wanaume au wanawake aliolala nao.

watu wanatoa sababu za tamaa, tabia, n.k

lakini ni nani ambaye hana tamaa; ni nani anayependa kuona au kuolewa na mwenye tabia mbaya?

Ninachokiona mimi ni kuwa

1.kwa sasa, kadiri siku zinavyokwenda ndoa inazidi kuwa ni gharama, nikimaanisha kwamba mchakato mzima wa kuoa umekuwa ni mgumu kutokana na masharti kama vile mahari, na gharama nyingine za harusi.
Hiyo inapelekea wengi watafute njia mbadala - (yaani kupunguza hamu tu )

2.elimu na uelewa umekuwa mwingi, sana sana kwa upande wa wanawake ambao sasa wamekuwa makini kutokuingia ndoa kichwa kichwa.
3.utandawazi pia umechangia kwa namna fulani; kwani kila mtu anataka "kujaribu" kile anachokiona au kusikia aone kuna nini

4. Kwa sasa mafundisho kutoka kwa mabibi na mababu hayapo tena. Pia mafundisho ya dini mbali mbali hayajatiliwa msisitizo na wafundishaji -

Pia kwa maisha ya sasa wengi tumeacha mahudhurio kwenye nyumba za ibada, kwa hiyo hakuna tena hofu ya Mungu - ya kusubiri ndoa.
Yaan kaka mi sina la kuongeza hapo
 
Mi nna mwaka wa 13 tangu nimeoa, na sijaona machungu ya mapenzi. kwani wenzangu hayo machungu yanatoka wapi?
Tatizo lenu ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu, watu hawataki kuacha baba na mama na kuambatana na mke/mme, kubebana na ndugu ndo chanzo cha machungu ya ndoa.
Eh jaman hongera kwa hilo
 
Uwe umeoa, au haujaoa, uwe na mpenzi au rafiki......Tatizo kubwa ni ubinafsi.. Selfishness.. ubinafsi.. either kwa mwanume au kwa mwanamke unakufanya usahau ahadi zetu, Pepo la ubinafsi likikuingia linakufanya upate tamaa, udanganye, utafute nyumba ndogo, n.k. Hivyo vingine vyote ni matokeo au outcomes ubinafsi wetu....Ukiweza kushinda ubinafsi..utamfikiria mwenzako, utahisi machungu yake, utathamini mchango wake, utajiweka nyuma badala ya kimbelembele..
MI pia nadhan tukielewa jambo ilo kwa pamoja machungu ya kimapenz yatapotea
 
Back
Top Bottom