Mungu anaendelea kuwaumbua, Vanessa Mdee atajwa sakata la Unga

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Mwanadada machachari Vanessa Mdee ametajwa katika msururu wa watuhumiwa wa mihadarati pamoja na Tunda ambaye ni kidate cha mtuhumiwa mwingine Young Dee.

Mwaka jana ilikuja thread hapa JF ikimtuhumu Vanessa Mdee kwa matumizi ya Mihadarati > Vanessa Mdee katika skendo kubwa ya kutumia madawa ya kulevya (Heroin)

Lakini mwanadada huyo machachari katika Bongo Fleva aliscreen shot na kuiweka katika ukurasa wake wa Instagram na kutema mbovu dhidi ya JamiiForums na sisi watumiaji kwa ujumla.

Mtandao wa Bongo 5 nao haukuwa mbali katika kuipa mileage habari ya Vanessa Mdee kutushushua watumiaji wa JamiiForums.

Angalia Screenshot hizi;



Vanessa Mdee katika skendo kubwa ya kutumia madawa ya kulevya (Heroin)

Sasa leo yametimia! Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemuongeza mwanadada huyu katika orodha yake pamoja na Tunda na Askari Polisi wengine watatu ambao wametakiwa kuripoti kituoni siku ya Jumatatu.

Thread kwa taarifa ya leo: MADAWA YA KULEVYA: RC Makonda na Kamanda Sirro waongea na wanahabari

Ndugu zangu, wanaJamiiForums tafadhali tuendelee kuwafichua hawa maharamia wanaoteketeza kizazi cha taifa la Mwalimu Nyerere kwasababu awamu hii kila tetesi zinafanyiwa kazi.
 
V money kwazile swaga zake yawezekana ni kweli lakini Wasije wakawa wanachomeshana
 
Hatariiiiiiiiiiiiiii.
 
AISEE!!!
Pole Yao,Jamaa ya Vanessa Mdee vipi yeye

"Wajanja hawali Madude wanakula Ngaja/Msuba/akamoge"-Mr 2 Sugu.
Naona na yeye ataunganishwa soon
 
Huyu binti..hebu ngoja, yeye anatumia au?

Na yule jux "girlfriend" wake si amefungwa china kama inavyodaiwa ni kwa madawa haya haya??

Salama ya jux ni ipi??
 
hakuna sheria ya kumhukumu mtu bila kupeleka kesi mahakamani na kuwa na ushahidi wa kutosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…