Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
- Thread starter
-
- #21
Hatujui Mungu alianzaje wala yukoje. Ila ushahidi unaonyesha vitu tata kama magari, kompyuta ni, havitokei vyenyewe tu. Sasa ulimwengu na viumbe hai ni tata zaidi ya kompyuta na magari.Kama kila chenye order kinatakiwa kuwa na mpangaji hiyo maana yake Mungu hawezi kuwepo.
Sasa kama vitu tata havitokei vyenyewe tu huoni kwamba hoja hiyo maana yake Mungu muumba vyote hawezi kuwapo, kwa sababu na yeye atahitaji kusababishwa kuwapo na kingine au mwingine, na mwingine atahitaji kusababishwa kuwapo na mwingine, ad nauseam, ad infinitum?Hatujui Mungu alianzaje wala yukoje. Ila ushahidi unaonyesha vitu tata kama magari, kompyuta ni, havitokei vyenyewe tu. Sasa ulimwengu na viumbe hai ni tata zaidi ya kompyuta na magari.
Naomba afanye miujiza ili tupate katiba mpya na TANGANYIKA ibaki mikono salama.Kuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.
Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.
Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?
Thibitisha Mungu hayupoMungu hayupo.
Hakuna miujiza.
Sayansi haina uhusiano wowote ule na Mungu au miujiza.
Tunaoamini uwepo wa Mungu tunarudi nyuma na kukwama hapo kwenye chanzo cha Mungu. Hatujui chanzo chake. Kama ambavyo wanasayansi wanavyokuja kukwama kwenye singularity. Lakini hilo haliwazuii kufanyia kazi shahidi zingine za kisayansi.Sasa kama vitu tata havitokei vyenyewe tu huoni kwamba hoja hiyo maana yake Mungu muumba vyote hawezi kuwapo, kwa sababu na yeye atahitaji kusababishwa kuwapo na kingine au mwingine, na mwingine atahitaji kusababishwa kuwapo na mwingine, ad nauseam, ad infinitum?
Huoni kuwa hiyo hoja ya vitu tata haviwezi kutokea vyenyewe tu, ni lazima visababishwe, ni hoja ya kuthibitisha Mungu hayupo, si hoja ya kuthibitisha Mungu yupo?
Mungu ni zaidi ya Science
Anauwezo wa ku control chochote na ni creative
Mfano mdogo hapa duniani kuna mimea ya aina nyingi sana
Hayo kisa kusema Neno
Tu Ardhi itoe mimea
Na Ardhi ikatoa
Anachosema vitu vinatii
He manipulates matter
Unathibitishaje kisichokuwepo?Thibitisha Mungu hayupo
Wanasayansi wakikwama kwenye singularity hakuna hoja ya kisayansi inayokuwa contradicted.Tunaoamini uwepo wa Mungu tunarudi nyuma na kukwama hapo kwenye chanzo cha Mungu. Hatujui chanzo chake. Kama ambavyo wanasayansi wanavyokuja kukwama kwenye singularity. Lakini hilo haliwazuii kufanyia kazi shahidi zingine za kisayansi.
Soma post #22 na #29 hii hoja imeshapanguliwa kirahisi tu.
Umekuja na askari ghetoni kwangu ukidai binti yako yupo ghetoni kwangu. Mimi nakwambia hayupo, kuthibitisha Nina fungua mlango pekua chumba kizima Ku kuthibitisha kwamba binti yako hayupo chumba ni kwangu.Unathibitishaje kisichokuwepo?
Kisichokuwepo hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.
Ngoja nikaitazameSoma post #22 na #29 hii hoja imeshapanguliwa kirahisi tu.
Hii ni hoja ya kuthibitisha Mungu hayupo na hawezi kuwapo, si hoja ya kuthibitisha Mungu yupo.
Kwenye singularity kanuni za kisayansi hazifanyi kazi. Zinakwama. Lakini hawaachi kuzitumia. Kwa waamini Mungu, inapofika chanzo cha Mungu ushahidi unaoonyesha kuwa vitu tata vyote vinaumbwa unakwama, lakini hatuachi kuutumia kutuaminisha kuwa tumeumbwa na ulimwengu umeumbwa.Wanasayansi wakikwama kwenye singularity hakuna hoja ya kisayansi inayokuwa contradicted.
Wanasayansi hawajawahi kusema wanajua kila kitu. Hawajawahi kusema kila kitu tata ni lazima kisababishwe na kingine. Na hata wangesema hivyo, sayansi imejengwa katika misingi ya kujiongeza kwa kujikosoa na kujisahihisha.
Wewe kusema kuwa kila kitu tata ni lazima kiwe kimesababishwa hakiwezi kutokea chenyewe tu, hapo hoja ya kuwepo Mungu muumba vyote imekuwa contradicted.
Unaelewa tofauti inayofanya mfano wako usiwe na maana hapo?
Mpangilio gani? Unajuaje ni mpangilio na si anthropic bias/ anthropic principle tu? Nguvu gani? Unajuaje inajitambua? Unajuaje imehusika kupanga?
Kama kila kilicho na order kinahitaji kupangwa, unaelewa kuwa, ujiondoa special pleading fallacy, hiyo ni hoja ya kwamba Mungu mpanga vyote hawezi kuwepo?
Kwa sababu katika sayansi kuna kanuni kwamba hatujui kila kitu. Tunaweza kuwa tumekosea lakini tukajua zaidi tukajiongeza.Kwenye singularity kanuni za kisayansi hazifanyi kazi. Zinakwama. Lakini hawaachi kuzitumia. Kwa waamini Mungu, inapofika chanzo cha Mungu ushahidi unaoonyesha kuwa vitu tata vyote vinaumbwa unakwama, lakini hatuachi kuutumia kutuaminisha kuwa tumeumbwa na ulimwengu umeumbwa.
Wewe mbona unarudia hoja niliyokwisha ipangua bila ku address point yangu niliyoitumia kuipangua hiyo hoja?Unajua kwa kutazama matokeo yake. Kwa mfano mfumo wa mwili wa binadamu jinsi unavyo function, hauwezi kuwa umetokea wenyewe tu bila ya uwepo wa a smart and very intelligent brain behind it
Sidhani kama Special pleading fallacy inaingia kwenye hoja ya Lycaon pictus
Unataka nikuthibitishiaje Mungu hayupo?Umekuja na askari ghetoni kwangu ukidai binti yako yupo ghetoni kwangu. Mimi nakwambia hayupo, kuthibitisha Nina fungua mlango pekua chumba kizima Ku kuthibitisha kwamba binti yako hayupo chumba ni kwangu.
Sisi tunao sema Mungu yupo tuna a mini Mungu yupo. Wewe unae sema Mungu hayupo, una uhakika na unajua kwamba Mungu hayupo. So tunataka ututhibitishie kwamba Mungu hayupo kwa sababu wewe ndio unajua hayupo
Nimesema ushahidi unaonyesha(sikumbuki kusema lazima) vitu tata huwa vimeumbwa. Lakini ushahidi huu haufai kuelezea chanzo cha Mungu ambaye tunasema hajaumbwa na mwanzo wa vitu vyote. Inafanana na ulivyosema. Kanuni za Newton haziwezi kuelezea Relativistic Speed.Kwa sababu katika sayansi kuna kanuni kwamba hatujui kila kitu. Tunaweza kuwa tumekosea lakini tukajua zaidi tukajiongeza.
Ndiyo maana kanuni za Newtonian classical mechanics zinafanya kazi katika context ya Newtonian classical mechanics, hazifanyi kazi katika Einstenian Relativistic physics, lakini hilo halitufanyi tutumie Einsteinian Relativistic physics popote pale.
Kwa sababu hatuhitaji Einsteinian Relativistic physics kwenye non Relativistic setting.
Kwenye sayansi kama nyundo inatosha kung'oa msumari huhitaji kutumia winch hata kama winch lina nguvu zaidi.
Kanuni kutofanya kazi si kanuni kuwa contradicted. Hayo ni mambo mawili tofauti.
Kanuni za Newton hazifanyi kazi katika speeds zinazokaribia speed ya mwanga, hapo tunahitaji kanuni za Einstein.
Lakini, ukweli huo hau contradict kanuni za Newton, unatuonesha tu kuwa kanuni za Newton domain yake si Relativistic speeds zikizo karibu na speeds za mwanga, domain yake ni speeds ndogo za kila siku hapa duniani.
Unachanganya suala la domain ya kanuni na kanuni kuwa contradicted.
Tofauti ya mfano wako na habari za kila kitu tata kuhitaji kusababishwa na muumba ni kwamba kanuni hii ina contradict uwepo wa Mungu.
Ukisema kila kilicho tata ni lazima kiumbwe na kingine hapo umeshasema kuwa Mungu muumba vyote hawezekani kuwapo.
Na kusema hujui Mungu katokeaje hujaepuka logic kwamba kanuni hii ina contradict uwepo wa Mungu. Inawezekana hujui Mungu katokeaje kwa sababu hayupo. Ni muhisika katika hadithi ya kuungaunga tu. Ushawahi kufikiria hilo?
Huelewi wapi hapo?
Sayansi inachoweza ni kuchunguza kazi za MunguKuna stori kuwa Columbus alipokuwa anaondoka kisiwa fulani huko Amerika aliwaambia wenyeji wampe chakula cha safari. Wakagoma. Akasema mkigoma kesho nitafanya miujiza. Nitautia mwezi giza. Kweli kesho yake mwezi uliingiwa giza. Wenyeji wakamsujudu Columbus na kumpa chakula. Waliona miujiza mtu kuutia mwezi giza. Lakini Columbus alitumia sayansi. Alijua habari za kupatwa kwa mwezi na mzunguko wake.
Binadamu anaweza kurusha mzinga na ukaenda kutua sehemu anayotaka. Anaangalia umbali alipo adui, spidi ya mzinga, joto, mgandamizo wa hewa, spidi ya upepo nk. Anaingiza yote haya(Variables)kwenye formula na kupata angle anayopaswa kuweka mzinga wake. Na kweli mzinga unaenda kutua alipopanga.
Si Mungu naye anapotabiri mambo hutumia formula kama hiyo. Anapotabiri mfano kifo anaingiza mabilioni ya variables kumhusu mtu huyo kwenye formula. Alichokula, mawazo yake(Brain waves) maneno anayoongea, afya yake, watu wanaomzunguka, hali ya hewa. . . Yaani anaingiza kila kitu kinachomhusu mtu huyo kwenye formula kisha anapata jibu kuwa kesho Absalomu mwana wa Daudi atakufa kwa kunaswa kwenye mti. Hafanyi miujiza, anafanya hesabu. "Miujiza" inawezekana bila sayansi?