Afrocentric view
JF-Expert Member
- Jun 19, 2022
- 1,374
- 2,280
Kupumzika simaanishi lazima iwe baada ya kuchoka, namaanisha ile kuacha kufanya kitu ambacho unafanya kila siku hata kama hakikuchoshi.
Nlisahau salamu.
Mambo vipi wakulungwa?
Hili swali waga najiuliza sana.
Kama Mungu ndio anacontrol kila kitu yani anagovern ulimwengu. Anajua saivi sehemu kuna mtu wangu anapaswa nimlinde asipate ajali, kuna mtu wangu huku anasali nimsikilize, kule kuna mtu wangu nimpe riziki, huku kuna jua linatakiwa lichomoze, pale kuna mtoto anatungwa mimba, huku kuna watu wanakufuru niwaadabishe.
Naona kama ratiba yake ipo tight sana 24/7
Ingawa bible inasema kuna siku alipumzika
Sasa si akipumzika Hivyo vitu vyote vitafeli?
Na kama hawezi kupumzika, je mungu ana free will?
Anaweza kuamua kuacha kuufatilia ulimwengu hata kwa sekunde 1?
Mungu si anaweza kila kitu?
Na kama anaweza kuacha, ila akauset ulimwengu ukaendelea kama kawaida yani akaweka autopilot...je tuna uhakika gani hata saivi hajafanya hivyo?
Je, Mungu anaweza kuumba Mungu mwingine?
Nliwaza hayo baada ya kusoma kitabu cha Ayubu mungu mwenyewe anasema kazi zake:
Ayubu 38
1Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu ayubu kutoka dhoruba:
4“Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia?
Niambie, kama una maarifa.
8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari
wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?
9Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawingu
na kuiviringishia giza nene.
12“ayubu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke?
na kulifanya pambazuko lijue mahali pake,
25“Nani aliyechora angani njia kwa ajili ya mvua?
Nani aliyeionesha radi njia yake mawinguni,
26ikasababisha mvua kunyesha nchini kusikoishi mtu
na jangwani ambako hakuna mtu
28“Je, mvua ina baba?
Au nani ameyazaa matone ya umande?
29Je, barafu ilitoka tumboni kwa nani?
Nani aliyeizaa theluji?
34“Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawingu
yakufunike kwa mtiririko wa mvua?
Nani anayemwambia jogoo kwamba mvua inakuja?
39“Je, waweza kumwindia simba mawindo yake
au kuishibisha hamu ya wana simba;
40wanapojificha mapangoni mwao,
au kulala mafichoni wakiotea?
41Ni nani awapaye kunguru chakula chao,
makinda yao yanaponililia mimi Mungu,
na kurukaruka huku na huko kwa njaa?
Je, wajua mbuzi wa milimani huzaa lini,
au umewahi kuona kulungu akizaa?
2Je, wajua huchukua mimba kwa muda gani,
au siku yenyewe ya kuzaa waijua?
3“Wajua wakati watakapochuchumaa kuzaa,
wakati wa kuzaa watoto wao?
4Watoto wao hupata nguvu,
hukua hukohuko porini,
kisha huwaacha mama zao na kwenda zao.
“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha,
lakini hawezi kuruka kama korongo.
14Mbuni huyaacha mayai yake juu ya ardhi
ili yapate joto mchangani;
15lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa,
au kuvunjwa na mnyama wa porini.
27Je, tai hupaa juu kwa amri yako,
na kuweka kiota chake juu milimani?