Mungu asipokuona watu hawezi kukuona. Aliyeonwa na Mungu huwezi kumficha

Mungu asipokuona watu hawezi kukuona. Aliyeonwa na Mungu huwezi kumficha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Sabato Njema Wakuu!

Mungu akikuona Watu watakuona, aliyeonwa na Mungu kamwe huwezi kumficha asionekane na watu.

Mungu akikukubali hakuna atakayekuzuia. Lakini haimaanishi vipanya na ndorobo havitatokea kukupigia kelele. Lakini siku zote kelel za panya hazimzuii Paka kulala usingizi.

Kijana kabla ya kutaka kuonwa na Wanadamu basi hakikisha Mungu anakuona.
Vinginevyo, utakuwa chawa na kujikombakomba miaka nenda Rudi na hautofanikiwa Kwa lolote. Hakuna atakayekuona.
Utakuwa Kama mtumwa.

Tafuta kuonwa na Mungu.
Jipendekeze Kwa Mungu.
Usimuonee aibu Mungu.
Tafuta Sana kumjua Mungu ili uishi Kwa furaha.

Usiogope kukabiliana na Shetani na vibaraka wake.
Kama Shetani haogopi na anajuhudi kusambaza Uasi na maovu.
Nawe usiogope na fanya juhudi kusambaza wema na haki ya Mungu.

Namna Bora ya kuwa na elimu, na maarifa, na Ujuzi, na ufahamu ni kuupendq ukweli, haki na kuusimamia.
Usiogope watu wenye tabia za kishetani, kuwa na msimamo thabiti, Kama wao wasivyokata tamaa kuhamisha maasi basi wewe uwe mara mbili Yao kutokata tamaa kuhamasisha na kupinga Uovu Kwa akili zako zote, Kwa moyo wako wote na nguvu zako zote. Huko ndiko kumpenda Yule aliyekuumba, na Hilo ndilo kusudi la uwepo wako hapa Duniani.

Usitafute kujulikana na watu, wala usijionee fahari kujua na watu uliowapa hadhi ya ukubwa au waliopewa hadhi ya ukubwa na dunia hii. Bali tafuta kujulikana na Mungu, tena jionee fahari kujuana na MUNGU.

Taikon Leo sina la ziada, sinaga upole Kwa watu wapumbavu, Mstaarabu nisiye na matata Kwa watu waungwana.

Sabato njema tena.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, Nairobi, Kenya.
 
Back
Top Bottom