Mungu au Shetani? Tutazame upande wa pili wa shilingi

Ashelimo

Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
45
Reaction score
29
Tulianza maisha kwa kuzaliwa. Tukajazwa hadith juu Wema wa mungu na uovu wa shetani. Habari wanazotuambia zimechukuliwa katika vitabu vya watu wa kale. Kila mmoja na wakati wake na wengine wakawa na ushawishi mkubwa kushinda wengine.

Vitabu hivyo pia viliandikwa na wanadamu ambao walizaliwa, wakawa watu wazima na wakaendesha harakati zao. Ukitafuta chanzo cha habari hizo utaambiwa zimetoka kwa Mungu ambaye amewafunulia manabii wake.

Ugomvi kati ya Mungu na Shetani wote watukuwepo na kwanini waligombana tunapata visa ambavyo chanzo chake ni Mungu. Japo hadithi ziko nyingi lakini hukubalina kwamba Shetani aliasi.

Yaani kama uko na wife akamegwa na washikaji na mwisho akaamua na nyumba kuhama. Ukitaka kusulihisha kesi kama hiyo lazima upate nafasi ya kusikiliza pande zote mbili.

Ukisikia upande wa mume pekee au ukisiliza upande wa mke pekee utapata picha isiyosahihi juu ya tukio husika.
Ugomvi wa Mungu na Shetani hautuhusu maana hatukuwepo. Walichofanya mafahari hawa wawili ni kutuweka katika mabano.

Shetani kushoto Mungu kulia. Najua wengi mtachagua upande wa kulia kwa sababu Tunajipendekeza kwa Mungu lakini bila kushoto kulia sio chochote.

Messi ni Mchezaji, Lakini angekosa mguu mmoja uwe wa kulia au kushoto basi maisha yake yangekuwa ni ngoto flani tu ambayo isinge timia

Wametuweka kati, Ugomvi wao usiotuhusu unaadhiri kila hatua ya maisha yetu. Labda Tungepata na manabii wa Shetani watupa kisa cha ugomvi wao katika mtizamo wa Shetani Ingekuwa vizuri sana. Labda Shetani anazosababu za msingi za kutotafuta muafaka na kuyamaliza kwa Amani.

Ikiwezekana manabii wa Mungu na manabii wa shetani wafanye maombi ya pamoja ili Tuwaite wababe hawa wawili katika meza ya Majadiliano. Yaishe kwa Amani. Unaujua moto au unausikia?

Huyu Satani anatumaini gani mpaka asiogope minyoro na Kuishi motoni milele maana imeandikwa mauti yatawazunguuka watu wa motoni kutoka kila upande lakini hawafi wala hawawi hai (Quran) Kwenye moto wa milele ambao funza wake wawafi wala hawasiinzi (Biblia)

Tumaini La shetani liko wapi? Kwanini hajatetereka katika msimamo wake mbali na ahadi kede kede za kuangamizwa.

Ukweli unaweza kuwa kinyume kabisa. Mfano hai, Wengi hatutoi nyuma kwasababu Mungu amekatakaza. Lakini waliotoa wamegoma kuacha hako kamchezo.

Mbele kwa mbele hayo ni mambo ya mungu na kuliwa kiboga, vimichezo vya Sodoma Gomora ni mambo ya Shetani, Au sio wadau? Mbona hawaachi haka kamchezo? Utamu hadi kisogoni? Ka utamu gani hako?

Labda hata Jehannam ni changa la macho. Au sema mazigaziga. Kwanini Tunamhukumu Shetani wakati hatujui tumaini lake?

NB: Atayetuchoma ni Mungu na malaika wake wala sii shetani. Mungu hana Democrasia. Hashauriki. Mpango wake wa kuchoma wanadamu na Mashetani uko pale pale. Just kama kuna manabii wa Shetani Tunataka hadithi yao ili Tuwe na ufahamu maana Mungu na Shetani wametuweka katika mabano.
 
kipi kinashindikana kumkamata shetani au kumua hili mambo yakae sawa au shetani atoke adharani aseme anataka nini tuangalie kama tutaweza kumtimizia atulie..Sisi binadamu hatuja muumba shetani so kwanini atusumbue tulimfanyia nini? Kibaya ninacho kiona tuna teseka duniani na tukienda mbinguni tunateseka tena..Wafia dini nao hawana majibu wana unga unga tu..Dini yangu ya kiafrika haina vitisho mambo raha mustarehe..
 
Kuna mambo yaache kama yalivyo...

Ni sawa na kutafakari bila giza, mwanga ungekuwepo wa nini?


Cc: mahondaw
 
Ukwel ni kwamba Shetan ameachwa ili tuone utwala wake, maana yeye alidai kwamba Mungu anawabania wanadam so ikabd aachiwe madaraka ili sisi tupime kwamba je utawala wa shetan upo sahih so amn now tupo kwenye utawala wa shetan Unaposoma 1Yohana 2:19 inasma tunatokana na Mungu ila ulmwengun unakaliwa na Shetan, So ukitaka kuukataa utawala huu usifanye yanayompendeza Shetan


Nb kama kna swal la nyongeza niulze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi tumekua tukijiuliza Kwa nin Mungu aliruhusu shetani amdanganye hawa, jibu ni kwamba Mungu alimpa mwanadamu option mbili ya kumkata au kumkubali, bahati mbaya Adam akamkataa Mungu, na Mungu bila hiana akakubaliana na adamu kwa-sababu angeingilia angevunja sheria aliyojiweka yeye. Na shetan anamjua Mungu Kwa sababu ameshakaa naye ndo maana alijiamini alivyomfuata hawa.
Ndo maana hata wanadamu wanamtukana Mungu na haingilii, jibu ni kwamba hawez kukulazimisha umtumikie/umfuate, yaan wanafamu tuna Uhuru wa kumkataa Mungu, ndo maana ni Hatar sana kulazimisha watu kumfuata Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma yote, mada za namna hii siku hizi nazipenda, zinanipa kufikiri.

Shetani na Mungu ni mpango wa mzungu, kama alivyopanga mambo mengi na tukayafuata. Huwa nikipita kanisani nikisikiliza mahubiri, nikitafakari, naona jinsi gani mzungu/muisraeli/muebrania au yoyote anayehusika alivyotumia akili kuiteka dunia ya kikristo...
 
Ulikuwepo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I concur with you Bro Eli79
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hakuna ugomvi kati ya Mungu na shetani, kwani mmoja ni Muumba na mwingine ni kiumbe tu. Shetani alishahukumiwa na Mungu hatabadilisha msimamo wake kwani shetani hataki kubadilika.

Anachofanya shetani kuharibu uumbaji wa Mungu kwa kadiri anayoweza kwani kwa kufanya hivyo anafikiri kwamba anapambana na Muumba kwani shetani hana matumaini tena.

Matatizo ya wanadamu ni ya kujitakia na yanatokea kutokana na matendo ya wanadamu, pamoja na kwamba siyo lazima utende wewe ili uteseke hata baba yako akitenda vibaya yawezekana ukateseka pia kutokana na matendo yake lakini haki ya Mungu ipo siku ya mwisho katika umilele.
 
Mkuu umewaza kama nilivyowazaga mimi

Sikuzote hauwezi kutoa hukumu au lawama kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja, na ndio maana hata mahakamani naye mtuhumiwa anahaki ya kujieleza dhidi ya mshtaki wake ili kumpa mwangaza hakimu ambaye hakuwepo wakati wa tukio ili atoe hukumu ya haki

Tunaona upande mmoja wa mungu ndio uliotoa maeleze tena na chuki kibao dhidi ya shetani huku ukisisitiza kua shetani ni kiumbe ambae hafai na anapaswa kuogopwa na yeyote atakaemfata ataangamia kwenye moto wa milele pamoja naye

Hapa tukitumia mizani ya haki za mahakama katika kutoa hukumu tutaona ni jinsi gani shetani anaonewa kwasababu hajapewa nafasi ya kusikilizwa, Kwasababu maelezo ya mungu yamekua na vitisho kiasi kwamba imekua ni vigumu kufuatilia upande wa pili ili tufahamu nani anastahili kuchukiwa

Inawezekana kabisa shetani akawa na sababu za msingi ambazo akituelezea tutamuona Mungu mnafiki lakini kutokana na husda za mungu alizozipandikiza kwenye vitabu vyake imekua ni ngumu mno

Sent using unknown device
 

Hapo kwenye bold mkuu naona unamtetea mungu

Mungu asingekua na hiana asingetoa laana kumwambia adamu kua atakula kwa jasho na kuyafupisha maisha yake wakati alimpa option mbili ambazo yeye adamu kwa mapenzi yake akaona upande huu wa shetani unafaa

Mungu anahiana kwasababu mhasimu wake wa kwanza ambae ni shetani amemuacha ale bata miaka yote hajagusa hata maisha yake kusema labda ataishi miaka michache alafu atakufa

Kama mungu hakupenda adamu amchague shetani ilikuaje akampa option ya kuchagua iliyomjumuisha na shetani?



Sent using unknown device
 
Mambo ni mengi ila tatizo ni muda.
Ukijatibu kuchunguza kwa undani kabisa bila chembe/mahaba ya dini utaona jinsi gani kisa cha Mungu na Shetani kilivyojaa uwongo ulio dhahiri.
Eti hapo mwanzo Mungu aliumba viumbe malaika, alafu shetani akamuasi Mungu.Lakini muhanga mkubwa wa uhasi huu ni binadamu ambaye hakuwa na hatia yoyote ile katika uhasi wa shetani.
Lakini Mungu kama alichukizwa na shetani kwanini hakumuangamiza tangu hapo kabla lakini akamuacha huyu shetani kuangamiza uumbaji wa Mungu binadamu.
Kitendo cha mungu kumuacha shetani tangu hapo kabla hadi sasa kimeleta machafuko kila kona ya dunia lakini huyo mungu anauwezo wa kumuangamiza.Hii nadharia inakosa mashiko kwa mwenye kufikiri kwa logic.
Mungu na shetani ni majina tu yanayotumika kuziongoza/kutawala baadhi ya jamii ambazo bado zipo katika illusion.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…