Mkuu umewaza kama nilivyowazaga mimi
Sikuzote hauwezi kutoa hukumu au lawama kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja, na ndio maana hata mahakamani naye mtuhumiwa anahaki ya kujieleza dhidi ya mshtaki wake ili kumpa mwangaza hakimu ambaye hakuwepo wakati wa tukio ili atoe hukumu ya haki
Tunaona upande mmoja wa mungu ndio uliotoa maeleze tena na chuki kibao dhidi ya shetani huku ukisisitiza kua shetani ni kiumbe ambae hafai na anapaswa kuogopwa na yeyote atakaemfata ataangamia kwenye moto wa milele pamoja naye
Hapa tukitumia mizani ya haki za mahakama katika kutoa hukumu tutaona ni jinsi gani shetani anaonewa kwasababu hajapewa nafasi ya kusikilizwa, Kwasababu maelezo ya mungu yamekua na vitisho kiasi kwamba imekua ni vigumu kufuatilia upande wa pili ili tufahamu nani anastahili kuchukiwa
Inawezekana kabisa shetani akawa na sababu za msingi ambazo akituelezea tutamuona Mungu mnafiki lakini kutokana na husda za mungu alizozipandikiza kwenye vitabu vyake imekua ni ngumu mno
Sent using
unknown device