Mungu au Shetani? Tutazame upande wa pili wa shilingi

Mungu au Shetani? Tutazame upande wa pili wa shilingi

Mkuu umewaza kama nilivyowazaga mimi

Sikuzote hauwezi kutoa hukumu au lawama kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja, na ndio maana hata mahakamani naye mtuhumiwa anahaki ya kujieleza dhidi ya mshtaki wake ili kumpa mwangaza hakimu ambaye hakuwepo wakati wa tukio ili atoe hukumu ya haki

Tunaona upande mmoja wa mungu ndio uliotoa maeleze tena na chuki kibao dhidi ya shetani huku ukisisitiza kua shetani ni kiumbe ambae hafai na anapaswa kuogopwa na yeyote atakaemfata ataangamia kwenye moto wa milele pamoja naye

Hapa tukitumia mizani ya haki za mahakama katika kutoa hukumu tutaona ni jinsi gani shetani anaonewa kwasababu hajapewa nafasi ya kusikilizwa, Kwasababu maelezo ya mungu yamekua na vitisho kiasi kwamba imekua ni vigumu kufuatilia upande wa pili ili tufahamu nani anastahili kuchukiwa

Inawezekana kabisa shetani akawa na sababu za msingi ambazo akituelezea tutamuona Mungu mnafiki lakini kutokana na husda za mungu alizozipandikiza kwenye vitabu vyake imekua ni ngumu mno

Sent using unknown device
Wengi siku hizi mnakuwa devil worshippers kwa hizi fikra. Mtapitapita sana ila mwishoni mtarudi kwenye mstari.
 
Mambo ni mengi ila tatizo ni muda.
Ukijatibu kuchunguza kwa undani kabisa bila chembe/mahaba ya dini utaona jinsi gani kisa cha Mungu na Shetani kilivyojaa uwongo ulio dhahiri.
Eti hapo mwanzo Mungu aliumba viumbe malaika, alafu shetani akamuasi Mungu.Lakini muhanga mkubwa wa uhasi huu ni binadamu ambaye hakuwa na hatia yoyote ile katika uhasi wa shetani.
Lakini Mungu kama alichukizwa na shetani kwanini hakumuangamiza tangu hapo kabla lakini akamuacha huyu shetani kuangamiza uumbaji wa Mungu binadamu.
Kitendo cha mungu kumuacha shetani tangu hapo kabla hadi sasa kimeleta machafuko kila kona ya dunia lakini huyo mungu anauwezo wa kumuangamiza.Hii nadharia inakosa mashiko kwa mwenye kufikiri kwa logic.
Mungu na shetani ni majina tu yanayotumika kuziongoza/kutawala baadhi ya jamii ambazo bado zipo katika illusion.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ukifikiria kwa makini utakundua Mungu na shetani ni majina yaliyotungwa tu na watu ili kuogofya watu washindwe kuutafuta ukweli

Sent using unknown device
 
Habari za uwepo wa Mungu ni moja kati ya njia zilizotumika kuwafanya watu waishi katika mfumo mmoja.

Sijui kama utanielewa.

Ipo, hivi. Ili watu uwatawale kiurahisi, unawatengenezea kitu ambacho watakifuata wengi na kitakua utamaduni wao.
Hivyo, habari za uwepo wa Mungu ni hadithi za kutungwa walizolishwa wazee wetu ili sisi tutawalike kirahisi.

Ndio maana leo hii wewe huna sauti wala nguvu
 
Kuna vitu ukivifikiria sana unaweza kufuru lakini mkuu,tukisema tuishi kadri ya mtu anavyotaka... Unadhani dunia itakuwa na utulivu kama tulionao kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa kua hizi dini zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uovu hapa duniani

Lakini tukiangalia upande wapili tunaona hizi dini ni kamba tu, izrael ambae ni taifa teule kila siku ni mtu wa kurusha makombora dhidi ya mpalestina na kuua watu, hivi kweli Mungu huyu yupo au kamba tu?



Sent using unknown device
 
Tulianza maisha kwa kuzaliwa. Tukajazwa hadith juu Wema wa mungu na uovu wa shetani. Habari wanazotuambia zimechukuliwa katika vitabu vya watu wa kale. Kila mmoja na wakati wake na wengine wakawa na ushawishi mkubwa kushinda wengine.

Vitabu hivyo pia viliandikwa na wanadamu ambao walizaliwa, wakawa watu wazima na wakaendesha harakati zao. Ukitafuta chanzo cha habari hizo utaambiwa zimetoka kwa Mungu ambaye amewafunulia manabii wake.

Ugomvi kati ya Mungu na Shetani wote watukuwepo na kwanini waligombana tunapata visa ambavyo chanzo chake ni Mungu. Japo hadithi ziko nyingi lakini hukubalina kwamba Shetani aliasi.

Yaani kama uko na wife akamegwa na washikaji na mwisho akaamua na nyumba kuhama. Ukitaka kusulihisha kesi kama hiyo lazima upate nafasi ya kusikiliza pande zote mbili.

Ukisikia upande wa mume pekee au ukisiliza upande wa mke pekee utapata picha isiyosahihi juu ya tukio husika.
Ugomvi wa Mungu na Shetani hautuhusu maana hatukuwepo. Walichofanya mafahari hawa wawili ni kutuweka katika mabano.

Shetani kushoto Mungu kulia. Najua wengi mtachagua upande wa kulia kwa sababu Tunajipendekeza kwa Mungu lakini bila kushoto kulia sio chochote.

Messi ni Mchezaji, Lakini angekosa mguu mmoja uwe wa kulia au kushoto basi maisha yake yangekuwa ni ngoto flani tu ambayo isinge timia

Wametuweka kati, Ugomvi wao usiotuhusu unaadhiri kila hatua ya maisha yetu. Labda Tungepata na manabii wa Shetani watupa kisa cha ugomvi wao katika mtizamo wa Shetani Ingekuwa vizuri sana. Labda Shetani anazosababu za msingi za kutotafuta muafaka na kuyamaliza kwa Amani.

Ikiwezekana manabii wa Mungu na manabii wa shetani wafanye maombi ya pamoja ili Tuwaite wababe hawa wawili katika meza ya Majadiliano. Yaishe kwa Amani. Unaujua moto au unausikia?

Huyu Satani anatumaini gani mpaka asiogope minyoro na Kuishi motoni milele maana imeandikwa mauti yatawazunguuka watu wa motoni kutoka kila upande lakini hawafi wala hawawi hai (Quran) Kwenye moto wa milele ambao funza wake wawafi wala hawasiinzi (Biblia)

Tumaini La shetani liko wapi? Kwanini hajatetereka katika msimamo wake mbali na ahadi kede kede za kuangamizwa.

Ukweli unaweza kuwa kinyume kabisa. Mfano hai, Wengi hatutoi nyuma kwasababu Mungu amekatakaza. Lakini waliotoa wamegoma kuacha hako kamchezo.

Mbele kwa mbele hayo ni mambo ya mungu na kuliwa kiboga, vimichezo vya Sodoma Gomora ni mambo ya Shetani, Au sio wadau? Mbona hawaachi haka kamchezo? Utamu hadi kisogoni? Ka utamu gani hako?

Labda hata Jehannam ni changa la macho. Au sema mazigaziga. Kwanini Tunamhukumu Shetani wakati hatujui tumaini lake?

NB: Atayetuchoma ni Mungu na malaika wake wala sii shetani. Mungu hana Democrasia. Hashauriki. Mpango wake wa kuchoma wanadamu na Mashetani uko pale pale. Just kama kuna manabii wa Shetani Tunataka hadithi yao ili Tuwe na ufahamu maana Mungu na Shetani wametuweka katika mabano.


Shida ni kwamba mnadhani shetani ni kiumbe mmoja aliyeumbwa na Mungu (a single creature),

Ukitaka kujua shetani anafanana vipi chukua mfano wa nuru na Giza, nuru imeumbwa lakini giza halijaumbwa na penye nuru giza huondoka na kinyume chake ndivyo hivyo Mungu na malaika ni kama nuru na shetani ni kama giza.
 
Mada imeingiliwa na wapagani, acha nirudi jukwaa la michezo 👋👋👋👋👋👋👋👋
 
Hakuna ugomvi kati ya Mungu na shetani, kwani mmoja ni Muumba na mwingine ni kiumbe tu. Shetani alishahukumiwa na Mungu hatabadilisha msimamo wake kwani shetani hataki kubadilika.

Anachofanya shetani kuharibu uumbaji wa Mungu kwa kadiri anayoweza kwani kwa kufanya hivyo anafikiri kwamba anapambana na Muumba kwani shetani hana matumaini tena.

Matatizo ya wanadamu ni ya kujitakia na yanatokea kutokana na matendo ya wanadamu, pamoja na kwamba siyo lazima utende wewe ili uteseke hata baba yako akitenda vibaya yawezekana ukateseka pia kutokana na matendo yake lakini haki ya Mungu ipo siku ya mwisho katika umilele.
Tumaini lake ni lipi? Au haujui moto?. Au labda ni mwendawazi anayestahili Mirembe na sio Jehannan
 
Back
Top Bottom