Mungu awabariki Wanawake

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Katika wimbo wa Lucky Dube "God Bless The Women" yaani "Mungu awabariki Wanawake"

anasema:

Katikati ya usiku wa manane, nilisikia sauti nyororo ya mama ikiomba. Ikiomba kwa uchungu. Akiomba kwa ajili ya watoto wake, akiomba kwa ajili ya elimu yao, ikiomba kwa ajili ya kesho yao.

Nilimsikia pia akiomba kwa ajili ya mwanaume aliyemtelekeza.

Akamkimbia na kumuachia watoto, ambao sasa anahangaika mwenyewe kuwalea.

Kila siku tunasifu mashujaa wa aina mbalimbali. Lakini kuna mashujaa tunaowasahau. Wamama wa dunia hii.
Hawa ni mashujaa wa kweli, Mashujaa wasio na tuzo.

Hata hali iwe ngumu vipi hawakimbii wajibu wao. Husimama na kupambana.
Maisha yanapokuwa magumu sana husimama imara na kuyakabili.

Hawatelekezi watoto. Hupambana kwa hali yoyote kuwalinda. (Wako tayari kushinda njaa ili watoto wale, wapo tayari kufa ili watoto waishi).

Mimi tena nasema "Mwenyezi Mungu awabariki wanawake wote!"

 
Ameen Ubarikiwe, Umenikumbusha mama jinsi anavyo niombea dua nzuri kila ninapo mjulia hali.
 
Umenikumbusha mbali sana.
Mama alikuwa akiomba kila siku baba anapotoka home. Au akiwa safarini.

Siku moja nikamuuliza, mama mbona mimi nikitoka huniombei?
Akanijibu nakuombea kila unapotoka nyumbani ila wewe huwezi kujua. Hata babako hajui kama namuombea.

Mungu akuheshimu mama yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

POLENI SANA WANAWAKE:
NDIYO MAANA NAWACHUKIA SANA WATU WANAOWANYANYASA WANAWAKE
 
Moma aisee dah
 
Ameen
 
wamama hawatelekezi watoto hata kama maisha magumu!?? hapana nimekataa
 
Mungu awabariki WANAWAKE na WANAUME!

kila mmoja ana nafasi yake na sijaona alie bora kumshinda mwenzie.

- KANA -
tukipewa japo kanafasi ka kusifiwa mara moja kwa mwezi humu ndani mjitahidi japo kutuachia basii..!!
 
tukipewa japo kanafasi ka kusifiwa mara moja kwa mwezi humu ndani mjitahidi japo kutuachia basii..!!
Bora nyie mnasifiwa japo mara moja kwa mwezi. Sijapata kuona uzi ukiwasifia wababa au wanaume. Kuna ka upendeleo, ila sisi wanaume hatujali!

- KANA -
 
Ubarikiwe kwa kutukumbuka.
 
"Mungu akuheshimu Mama yangu" na si Mama yako ndiye amuheshimu Mungu?[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora nyie mnasifiwa japo mara moja kwa mwezi. Sijapata kuona uzi ukiwasifia wababa au wanaume. Kuna ka upendeleo, ila sisi wanaume hatujali!

- KANA -
Nani anampendelea mwenzie??
Maana mnaotuponda na kutusifia ni nyie nyie wababa,
Why msijisifie wenyewe kama mnavyofanya kwetu.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…