Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Katika wimbo wa Lucky Dube "God Bless The Women" yaani "Mungu awabariki Wanawake"
anasema:
Katikati ya usiku wa manane, nilisikia sauti nyororo ya mama ikiomba. Ikiomba kwa uchungu. Akiomba kwa ajili ya watoto wake, akiomba kwa ajili ya elimu yao, ikiomba kwa ajili ya kesho yao.
Nilimsikia pia akiomba kwa ajili ya mwanaume aliyemtelekeza.
Akamkimbia na kumuachia watoto, ambao sasa anahangaika mwenyewe kuwalea.
Kila siku tunasifu mashujaa wa aina mbalimbali. Lakini kuna mashujaa tunaowasahau. Wamama wa dunia hii.
Hawa ni mashujaa wa kweli, Mashujaa wasio na tuzo.
Hata hali iwe ngumu vipi hawakimbii wajibu wao. Husimama na kupambana.
Maisha yanapokuwa magumu sana husimama imara na kuyakabili.
Hawatelekezi watoto. Hupambana kwa hali yoyote kuwalinda. (Wako tayari kushinda njaa ili watoto wale, wapo tayari kufa ili watoto waishi).
Mimi tena nasema "Mwenyezi Mungu awabariki wanawake wote!"