Mungu baada ya kukataliwa na Wanadamu zaidi ya mara mbili akaamua kwenda Mbali na uso wa Dunia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MUNGU BAADA YA KUKATALIWA NA WANADAMU ZAIDI YA MARA MBILI AKAAMUA KWENDA MBALI NA USO WA DUNIA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Maskini! Ni simulizi ya kuhuzunisha Sana. Hakuna kitu kibaya kama KUKATALIWA, hakuna kitu kibaya kama kutokupendwa.

Mungu akaumba dunia. Kisha akaona acha amuumbe mtu kwa mfano wake ili atawale. Mfanowe Lakini hakujiumba mwingine. Aliumba kiumbe kutoka madini yapatikanayo kwenye ardhi. Kila kiungo na madini yake. Kisha kiumbe hicho akakiwekea Nishati ya uhai kutoka Katika pumzi yake ili kiwe na utashi.

Bado najiuliza nini kilipelekea kiumbe huyu aumbwe. Mimi sijui.
Lakini masharti anayopewa huyu kiumbe yananifanya nione kusudi la Mungu kumuumba huyu Mtu.

Mungu alitaka apendwe? Je nini kilitokea Mpaka akataka kupendwa na kiumbe alichokiumba yeye mwenyewe.

Kwa nini asitafute upendo kutoka kwa wanyama, milima mabonde, na viumbe wengine lakini atafute upendo kwa MTU(kiumbe alichokiumba yeye mwenyewe)?

Nikakumbuka, upendo unahusu spiritual connections na sio Physical connections. Kumbe Ile pumzi aliyopulizia kwenye Yule kiumbe aitwaye mtu ni spiritual connections Kati ya Mungu na Mtu. Au mtu na Mungu. Bado nawaza, nafikiri na isichukuliwe ndivyo ilivyo.

Mungu hawezi hitaji upendo kutoka kwa Wanyama au ndege au viumbe ambao hakuwapulizia sehemu ya roho yake.

Basi spiritual connections ikaunda love connections. Daah! Wivu ukaingia. Kwa maana upendo wa kweli lazima kuwepo Wivu.

Katika mapenzi na upendo kuna Ile kutaka kujua au kujifurahisha kwamba Fulani ananipenda. Ndipo mtu unawekewa jaribio la kupima je ananipenda KWELI?

Hapo ndipo akaweka Sheria ya kutokula Tunda la ujuzi wa Mema na Mabaya lakini msingi wa Sheria hiyo ni kupima upendo wa kweli na kama sio kupima Basi ni Ile Hali ya kuhitaji kujifurahisha.

Mungu akakataliwa, watu hawakumpenda Mungu ingawaje walikuwa wanamhitaji kwa faida Zao wenyewe.

Yaani ni Ile mtu hakupendi lakini anataka pesa na Mali zako. Ndicho ambacho Mungu akafanyiwa na binaadama. Maskini!

Sheria Ile ikavunjwa. Upendo ukakatika "love connections" na hapohapo spiritual connections ikaanza kuugua ugua. Leo kichwa, Kesho tumbo, Kesho kutwa miguu mtondogoo macho. Hatimaye Spiritual connections inakufa na Yule kiumbe ambaye ni mtu anakufa physically. Doooh!

Basi bhana! Mungu hakukata tamaa. Akawafukuza, na kwa vile love connections imekatika automatically uwezo wa kumwona Mungu ukafa kwa sababu upendo hufungua macho ya rohoni na kupofusha macho ya mwilini.

Na jicho la rohoni likifa automatically mwili hauwezi kuona mambo ya rohoni na yale yanayokuja mwilini.

Hii tunasema, WANADAMU wote ni vipofu kwa sababu macho yao hayaoni. WANADAMU wote ni viziwi kwa sababu masikio Yao hayasikii.
Wanadamu wote ni mabubu kwa sababu midomo Yao haisemi.
Taikon ushaanza kuchanganyikiwa sasa. Mambo gani haya?

Subirini! Natulia ili nieleze nilichokikuta kwenye akili yangu. Kazi yangu ni kueleza hapa. Kazi yenu siijui.

Mungu akasema Sawa, sitaki kupendwa lakini acha niwaongoze watu hawa. Niwe kiongozi wao kwa maana sasa nisipowaongoza Mimi Nani mwingine atawaongoza. Tayari wamenikataa, ni vipofu hawaoni yanayokuja mbele, hawajui kilichopo mbele Yao. Ima kuna shimo au kuna bonde wao hawaoni. Ima kuna Hatari au laa Hilo hawajui. Acha niwaongoze Mimi.

Lakini watu wakakataa!
Wakamwambia Hatutaki kuongozwa na wewe. Mungu alipowauliza kwa nini hamtaki kuongozwa na Mimi Mungu wenu.
Watu wakamjibu, tazama Sisi tu vipofu, Sisi tuviziwi. Tumabubu Sisi.
Wewe pekee ndiye mwenye macho, maskio na mdomo na yote. Hata ukisema nasi hatusikii kama umesema, kwa sababu Sisi tu viziwi.

Hayo Maneno yote Mungu alichagua mtu Mmoja katikati Yao aliyemchagua, ambaye mtu huyo hakuwa anaona lakini angalau alikuwa na makengeza, hakuwa akijua kuongea lakini angalau alikuwa na kigugumizi, hakuwa anasikia lakini angalau alihisi Sauti sauti.

Mtu huyo Mmoja Kati ya watu ndiye alikuwa kama daraja la Mungu na watu, akisema na kuwaambia watu yaliyotoka kwa Mungu wao.

Lakini watu wakakataa, na kila aliyetumwa na huyo Mungu walimfukuza na ikibidi kumuangamiza.

Hatumtaki huyo Mungu
Tunataka kujiongoza Sisi wenyewe. Sisi ni vipofu Acha vipofu kwa vipofu tuongozane. Hatutaki kuijua Wala kuiona Njia tunayoipitia. Akakataliwa!

Basi akaghadhibika! Maskini! Lakini hakuna aliyejali tena kwani mioyo Yao ilikuwa imekatwa na haina upendo tena. Kwa sababu love connection imekatika na spiritual connections inalegalega.

Mungu akaondoka na hapa namaanisha akaachana na mambo ya binadamu. Akaenda mbali naye. Sio mbali kieneo Bali akawa mbali na matendo ya binadamu.

Wakazaliwa na kuzaliwa. Kila wakati ukaja na watu wake na kuondoka na wengine. Ikafikia hatua sio tuu wakamsahau Mungu Bali kizazi kingine hakikuwahi kumjua. Ukizingatia ni vipofu na viziwi.
Watu hao wakasema Hakuna MUNGU.

Huku wengine wakamuunda mungu wao kulingana na akili na mambo Yale wayapendayo.
Kila jamii ikaunda mungu wake na hapo ndipo ikawepo miungu mingi Sana.

Lakini miungu hiyo ikawa vipofu kama wao walivyovipofu.
Miungu hiyo ikawa viziwi kama wao walivyo viziwi Wakiiomba haiwasikii, na wakitaka iwajibu haijibu.
Wakitaka ifanye haifanyi kwa sababu haina nguvu Wala uweza wowote.

Jamii zingine zikaona tazama miungu tuliyoiunda haitusaidii itatufaa nini kuendelea nayo. Tuiache tutumie akili zetu wenyewe.
Yule Mungu ametuacha wakasahau Baba na babu Zao ndio walichagua kujiongoza.
Hatumtaki huyo Mungu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Brother sjui kwanin umefikiria yote hayo lakini niseme tu ni Bahati mbaya ulizaliwa Afrika. Wewe ni Genius sana ulitakiwa upige Cheers na kina Albert Stein huko.
 
Back
Top Bottom