Kwanza lazima uelewe kuna kitu kinaitwa fate (something which is destined to happen to you) yaani majaaliwa na kila mtu ana fate yake hapa duniani.
Sasa swali kwanini imekaa hivyo, majibu yake ni from the theological perspective kwamba Mungu alipo umba dunia akaona kila kitu kinafaa na ni chakupendeza kwa lugha laini kazi ya Mungu haina makosa.
Sasa basi, vitu vinavyozungumzwa hapa ni vile ambavyo wewe una viomba, na wengi wetu tunaomba vitu ambavyo pengine tunao wajibu wakuvitafuta kama vile mali, mke, usalama, amani, upendo na ata afya njema.
Sina nia ya kukufuru au kulaumu, matatizo mengi ya watoto wetu pengine yangeweza kuepukika kama tungezingatia kanunu za afya na kufuata maelekezo ya kitabibu. Magonjwa mengine yanayowapata watoto ni ya kurithi au yanatokana na uzembe wa wazazi katika kutunza na kufuata afya ya uzazi. Nakiri pia kwamba matatizo mengine pia yanatokea bila kuwa sababu yoyote na hakuna anayeweza kulaumiwa mfano organ failures and diseases kama cancers.
Ukiacha matatizo yanotokea kwa kujitakia wenyewe kama vile urahibu wa madawa ya kulevya, ngono na ajali kama za bodaboda na nyingine nyingi ambazo zinasababisha madhara makubwa, bado sehemu kubwa ya maisha yetu sisi wanadamu ni majaaliwa ya Mwenye -Enzi Mungu.
Bado naendelea kukusihi, tuendelee kumshukuru Mungu kwakua matendo yake ni makuu na ya ajabu