Mungu hakuumba mema sambamba na mabaya

Mungu hakuumba mema sambamba na mabaya

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
2,162
Reaction score
3,088
Habari wana jamvi!

angalizo! ninamatatizo kidogo na lugha lakini naamini nitajitahidi nipate kueleweka vizuri.

kumekuwa na michango mingi jamvini ambayo ilikuwa ikihitaji kujua nini chanzo cha mema na mabaya, wengine wakilaumu kwanini Mungu aliruhusu mema na mabaya. nimejaribu kufanya utafiti na kuchanganya na akili yangu na kuwashilikisha jambo.

Tuanze Kwa kifikilia jambo moja, Unaweza ukaamua kupima joto na kiwango cha joto kikapanda na kushuka mpaka kufikia degree sifuri, sasa matokeo ya kupima joto yanaweza yakawa ni baridi au joto, watu wengi wanaamini kuwa baridi ni kinyume cha joto, na pia wanaamini ili kukamilisha mfumo wa upatikanaji wa joto na baridi ni lazima pawe na chanzo au uumbwaji wa joto Kwa pamoja. Vivyo hivyo watu wanafikiria sawa kuhusiana na mema na mabaya na pia nuru na Giza.

Naomba tujaribu kufikili zaidi, je aliyeumba joto alikuwa anaulazimu wa kuumba na baridi? baridi ni kinyume cha joto au baridi ni matokeo ya kukosekana Kwa joto? vivyo hivyo kwenye mema na mabaya tujiulize maswali haya.

Mungu alisema na iwe nuru na ikawa nuru, kitabu hakikuonyesha kwamba Mungu aliumba giza na Giza lipo, hivyo Giza ni kama matokeo ya kukosekana Kwa mwanga.

Tujaribu kufikili kivingine, unapompeleka mtoto wako shuleni uwe na uakika kuwa utampeleka shule iliyo bora na walimu watajitahidi kuhakikisha kuwa wanamfundisha vizuri pia. Sasa, kipi kitatokea endapo akafeli? utakuwa na haki ya kuituhumu shule husika kuwa imemfundisha mwanao kufeli? la hasha! kufeli ni matokeo ya kutokufaulu. kufeli Kwa mtoto wako hakuthibitishi kuwa shule ilimuandaa kufeli.

Vivyo hivyo ninaamini kuwa Mungu hakuumba mabaya, mabaya ni matokeo ya kutokuwepo Kwa wema ambao kauumba.

Nimejaribu kutumia logic za kawaida ili tusijikite kwenye imani na tukaleta itikadi, ninaruhusu kusahihishwa sambamba na kukosolewa

Aksante.
 
Kwa hiyo mkuu mjasiliaupeo unaamini kuwa hakuna nguvu iliyo nyuma ya mabaya (ubaya unajieneza wenyewe)? Unahisi hapa duniani idadi kubwa ni ya wema au wabaya? Ipi inaongezeka? Je inaongezeka yenyewe au kuna nguvu nyuma yake?
 
Last edited by a moderator:
Mema=correct thing(good side)
Mabaya=error (evil side)

Kila system in % za errors kutokea ndo mabaya ya dunia.
 
Habari wana jamvi!

angalizo! ninamatatizo kidogo na lugha lakini naamini nitajitahidi nipate kueleweka vizuri.

kumekuwa na michango mingi jamvini ambayo ilikuwa ikihitaji kujua nini chanzo cha mema na mabaya, wengine wakilaumu kwanini Mungu aliruhusu mema na mabaya. nimejaribu kufanya utafiti na kuchanganya na akili yangu na kuwashilikisha jambo.

Tuanze Kwa kifikilia jambo moja, Unaweza ukaamua kupima joto na kiwango cha joto kikapanda na kushuka mpaka kufikia degree sifuri, sasa matokeo ya kupima joto yanaweza yakawa ni baridi au joto, watu wengi wanaamini kuwa baridi ni kinyume cha joto, na pia wanaamini ili kukamilisha mfumo wa upatikanaji wa joto na baridi ni lazima pawe na chanzo au uumbwaji wa joto Kwa pamoja. Vivyo hivyo watu wanafikiria sawa kuhusiana na mema na mabaya na pia nuru na Giza.

Naomba tujaribu kufikili zaidi, je aliyeumba joto alikuwa anaulazimu wa kuumba na baridi? baridi ni kinyume cha joto au baridi ni matokeo ya kukosekana Kwa joto? vivyo hivyo kwenye mema na mabaya tujiulize maswali haya.

Mungu alisema na iwe nuru na ikawa nuru, kitabu hakikuonyesha kwamba Mungu aliumba giza na Giza lipo, hivyo Giza ni kama matokeo ya kukosekana Kwa mwanga.

Tujaribu kufikili kivingine, unapompeleka mtoto wako shuleni uwe na uakika kuwa utampeleka shule iliyo bora na walimu watajitahidi kuhakikisha kuwa wanamfundisha vizuri pia. Sasa, kipi kitatokea endapo akafeli? utakuwa na haki ya kuituhumu shule husika kuwa imemfundisha mwanao kufeli? la hasha! kufeli ni matokeo ya kutokufaulu. kufeli Kwa mtoto wako hakuthibitishi kuwa shule ilimuandaa kufeli.

Vivyo hivyo ninaamini kuwa Mungu hakuumba mabaya, mabaya ni matokeo ya kutokuwepo Kwa wema ambao kauumba.

Nimejaribu kutumia logic za kawaida ili tusijikite kwenye imani na tukaleta itikadi, ninaruhusu kusahihishwa sambamba na kukosolewa

Aksante.

kama uliruhusu watu kukukosowa mm sikukosow bali nakukukumbuxa may itakuw umesaha!! Mkuu rudi ktk Qur'an sura ya 78:10 utakuta kuwa mungu (Allah) alishamwambia mtume wake (saw) kwamba ameumba ucku (giza) na hakusema giza (ucku) ni matokeo ya kukosekana kwa mwanga!!!
 
Mema=correct thing(good side)
Mabaya=error (evil side)

Kila system in % za errors kutokea ndo mabaya ya dunia.

Errors(good side). It helps to let you know how far you are from the correct precision. It helps to seek for perfection.
 
kama ni mkristu basi mungu amejisifu kuumba mabaya. "I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the Lord do all these things." (Isaiah 45:7)
 
Back
Top Bottom