kupitia uhalisia na ufahamu ndio najua mimi nipo, kweli yakujua nipo kweli ama uongo inathibitishwa na uhalisia.
kupitia milango ya ufahamu ndio najua mimi nipo nakujua huu ni ukweli ama uongo ni kupitia hiyohiyo.. tofauti ya ukweli na uongo ni kuwa ukweli huthibitika na uongo hauthibitiki (ktk nyanja fulani).
so hata kama utasema sipo ila nimetengenezwa na li computer tu, kuthibitisha hivyo utahitaji kuwa na upana wake ktk nyanja zote nakanuni zote zakiulimwengu ambazo tukiweza kuzijua zote ndio tutajua kinagaubaga wakuweza kuthibitisha kila kitu!,hata vile ambavyo hatujavifikia,kuvijua,kuvihisi..
na ndio maana tunapata ugumu kwenye kuthibitisha baadhi ya vitu kwasababu hatujajua kanuni zote zilizopo kwenye ulimwengu,we still don't know about God,Uungu,nini chanzo cha kila kitu,na nini sio chanzo cha kila kitu,ulazima wakuwa na chanzo ama kutokuwa na chanzo umejificha kwenye kanuni ambazo hatujazijua bado!.
Hivyo na ndio maana nashangazwa na wote wanaondika kuwa hakuna Mungu ama yupo!,haya yote mawili hayana majibu kwa asilimia 100 kwani hatujajua kwanza hiyo asilimia 100 ktk ulimwengu.. so tukijua ndipo tutapata jibu la swali linalohusu kuwepo ama kutokuwepo kwa Mungu!.
ukisoma kwa makini nafikiri nitakuwa nimejibu maswali mengi na utakuwa umeshaelewa nini hatima yangu ktk mjadala huu!.