Mungu hasamehi Dhambi; tuache kudanganyana

Taikuni taikuni taikuni
Umepewa kipaji cha kuandika lakini sio kila Jambo lazima uandike
Umeupima upeo wako juu ya kile unachojaribu kutushirikisha?
Maana Kama zilivyo mbali mbingu na nchi ndivyo yalivyo mbali mawazo yetu (wanadamu) na mawazo ya Mungu ila mawazo hayo sio mabaya bali ni mema sana juu yetu hivyo usijaribu kumuelezea Mungu kwa maneno yako maana uwezo huo ujapewa
 
Ni maoni yako binafsi
 
Kwa iyo kula tunda kimasihara ni kosa au dhambi bwana Taikoon???
 
Kabla hatujaongea zaidi naomba unifafanulie hii,
Luka 5:32
Sikuja kuwaita wenye haki, Bali wenye dhambi, wapate kutubu.

Kama Yesu mwenyewe anasema hivo "wenye dhambi wapate kutubu" ana maana gani kama kutubu huko hakuleti msamaha?
 
Mungu hasamehi dhambi bali husamehe Makosa
Kuna aina tatu za dhambi(makosa ya kukusudia)

1.mtu anamuasi Mungu tu bila kuwakosea na wengine.

Mfano mtu akamkufuru Mungu na kusema hana lolote Mungu.

Hapa amemkosea Mungu tu.

2.mtu anamkosea Mungu na kuwakosea waja wengine.
Mfano ukimuibia mtu ama kumnyang'anya kwa nguvu .

Hapo umemkosea Mungu kwa kufanya jambo ambalo ameharamisha,lakini pia umemkosea huyu mtu kwa kummchukulia kitu kwa Nguvu.

Hapa dhambi hii ya pili ukiomba msamaha Mungu anaweza kukusamehe lakini yule mtu kama hajakusamehe Mungu anaenda kukuadhibu mpaka eidha ukaombe msamaha kwa yule mtu ama umrudishie kitu chake.

Hizi dhambi zote mungu anasamehe,ulichofanya umetumia akili kukanusha mungu kusamehe dhambi,huku ukitumia maandiko kumthibitisha Mungu na kuthibitisha hizo dhambi.
 
Isaya 55: 8-9

Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.


Pia


Isaya 1:18-19

Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi

Ndio maana akaitwa Mungu mwenye huruma, mfalme wa amani ...
 
Sheria za Mungu zipo clear.... au unaelewa nini maana ya samehe 7 mara 70? pindi tunapotubu tunamuwa wapya mbeke za Mungu.....

Fuatilia alivyoangamiza kizazi cha Nuhu na Sodoma na Gomora....kote kuwili alitoa nafasi ya kumkiri licha ya wao kuwa na maovu makubwa na mengi yaliyochukizo mbele zake
 
Naona umeshiba Ugali! Yaani kama Mungu hasamei dunia ya sasa ingefanywa majivu kama Sodoma na Gomora au kufutiliwa mbali kama enzi za Nuhu!
 
Mtu atasamehewa dhambi pindi anapotubu au anapofanya toba na kutokurudia tena yale matendo yaletayo dhambi ndani ya mtu
 
Na pia mtu afanyapo dhambi nakuamua kufanya toba atasamehewa endapo atajiepusha na kujizuia kutokufanya tena hayp maysndo yaletayo dhambi (Uaribifu
 
so biblia inapoandika neno "sin" humaanisha nini?
 
God works miraculously, not by a mere human thinking
 
Kongole mkuu. Nikiri kusema kuwa ikipita siku hujaandika jambo NAKERWA sana. Sikulazimishi uandike lakini ni roho inapenda kukusoma
 
Kuna neno waraka kwa waebrania "Kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki Tena dhabihu...Bali Kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto...

Wachungaji hawalisomagi church!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…