Mungu Kaondoa Baraka Katika Kila Kitu

Mungu Kaondoa Baraka Katika Kila Kitu

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Ni wiki ya pili sasa tangia tumemzika babu yetu mdogo, yaani baba yake mdogo mama yangu mzazi na namuomba Mwenyezi Mungu Amsamehe dhambi zake na amfanyie wepesi katika hesabu zake, na Amuweke Alipowaweka waja Wake wema....Aamin

Siku chache kabda ya kifo chake nilipata kuongea nae mambo meengi sana kwa namna ambayo nikiitafakari sasa ni kama alikua ananiaga maana si kwa busara zile alizozimwaga. Kwa ufupi tulihadithi meengi ila kuna moja lilinipa tafakari ya kina hadi leo naumiza kichwa

Babu alinambia kutokana na mambo yanavyoendelea duniani Mungu kaondoa baraka zake katika karibia kila kitu. Sababu kuu ni kwamba yale maovu makubwa makubwa kama mauaji, utesaji, roho mbaya, ulawiti ambayo yalifanya watu waliotangulia kabda yetu kuangamizwa sisi tunayafanya kuwazidi hao waliotangulia na ndio maana japo tunajiona tunaakili sana lakini ndio maangamizi ya kizazi chetu, ni rehema ya Mungu tu ndio inatuhifadhi

1. Kutakua na wanaojiita wasomi wenye uProfessor na ma Phd lakini hawana elimu, vitendo vyao
haviakisi hadhi za elimu zao bora wenye elimu za kawaida tu

2. Nyumba za ibada zitakua nyingi sana na nzuri sana na viongozi wa dini watakua wamesoma
sana dini zao lakini uchamungu kutakua hakuna, yatabaki matendo ya mwili ikiwa ni pamoja
na hadaa na hata utapeli na kujikweza kwa kujionyesha

3.Vyakula vitakua viingi sana vya kila aina lakini haviwaletei afya walaji wake na watu wanazidi
kua magoigoi kwa kila kitu hata kwa wanaume "uwanaume" wao ni wakusuasua

4. Kutakua na madawa ya kila aina lakini hayatibu magonjwa bali yanatuliza tu magonjwa na
badala yake dawa hizo zitakua na madhara ikiwa ni pamoja na kuleta maradhi mengine
mapya

Haya ni baadhi tu ya niliyoyakumbuka katika maneno ya babu yangu. Tena akaniambia wazee wao wa zamani waliiona hali hii itayokuja kwa vizazi vijavyo na wakaomba kama yeye alivyomuomba Mungu wasiishi wakaishuhudia dunia ya namna hiyo! Hata kama mambo hayo yapo kwa hivi sasa, babu alinambia bado picha kamili linakuja siku zijazo. Yajayo yanatisha zaidi!

Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Akurehemu babu yangu, wewe na wazee wako wote mliotangulia mbele za haki, mbele yako nyuma yetu
 
Kweli yaliyopo sasa yanatisha
Hayo ni maneno ya ukweli kabisa
Dawa za kila aina lakini hazitibu
Watu wametengeneza miradi mikubwa ya kutibu mpaka India lakini gharama zake ni kujitengenezea ulaji tu
 
Umeongea kweli kabisa Sesten na ukiangalia hiyo namba 3 na 4 ni kweli kabisa na ndio hali tunayoipitia sasa.
 
Kweli yaliyopo sasa yanatisha
Hayo ni maneno ya ukweli kabisa
Dawa za kila aina lakini hazitibu
Watu wametengeneza miradi mikubwa ya kutibu mpaka India lakini gharama zake ni kujitengenezea ulaji tu
Tena Kaka kama hizo dawa yaani haziponeshi cha zaidi waeza ambiwa ukitumia sana zinasababisha ugonjwa mungine.

Basi shida tupu kwa kweli.
 
Umeongea kweli kabisa Sesten na ukiangalia hiyo namba 3 na 4 ni kweli kabisa na ndio hali tunayoipitia sasa.
Namtafakari babu na usia wake Hajar, yajayo yanatisha kama haya maneno ya babu ni ya kweli
 
Namtafakari babu na usia wake Hajar, yajayo yanatisha kama haya maneno ya babu ni ya kweli
Yanatisha hasaaa.

Siku zote wazee wetu hawakuwa wakienda mbali na ukweli ndio sababu yaliyo mengi hapo ndio tunayoyapitia sasa.

Kama hiyo namba tatu si waona siku hizi Me wanavyolalamika kupungukiwa na hiyo kitu na ukiangalia sababu kubwa ni Ulaji Sesten.
 
Kweli kabisa Hajar vyakula na hata maji tunayokunywa yaweza kua na walakini , na siku hizi vijana wadogo ndio wateja wa dawa za kuongeza nguvu za kiume kitu ambacho mababu zetu hawakua nacho

Wakati huo mzee wa miaka 60 au zaidi anaoa mtoto mbichiii tena huku ana wanawake wengine na anapiga show kama kawa
 
Tena Kaka kama hizo dawa yaani haziponeshi cha zaidi waeza ambiwa ukitumia sana zinasababisha ugonjwa mungine.

Basi shida tupu kwa kweli.

Kuna mdogo wangu alkuwa anasumbuliwa na tatizo LA macho mwanzo tulijaribu kwa madokta wa kawaid tu lakin kwa baadae tukasema tujarib kwa madokta wakubwa akachekiwa akapewa dawa za kutumia tatizo lililokuja kutokea hadi kesho huwa hatuamini aisee baada ya matumizi tu ya hizo dawa DogO aliugua kupita maelezo kwenda kumcheki hospital wakasema ana tatzo LA sukari na walisema iko juu mno na tungechelewa kumfikisha ilikuwa ndo kwa heri cha kushangaza sasa baada ya DogO kuanza kuishi kama wagonjwa wengne wa sukari kwa mwezi mzima hali yake ikabadilik kabisa kuja kucheki kiwango cha sukar kilikuwa ni 7 tofauti kabisa na siku tulompeka Hosp ilkuwa 40 kina chonishangaza asaiv DogO n mzima kabisa na hana tena hilo tatizo

Hizi dawa sinaga imani nazo kabisa
 
Umeona sasa. Yaani kwa sasa dawa ni changamoto aiseee.

Poleni sana Mkuu.
 
Umeona sasa. Yaani kwa sasa dawa ni changamoto aiseee.

Poleni sana Mkuu.
Sasa ukute kuna wabibi au wamama wa kihenga, kuna dawa za magonjwa za mitishamba wanazijua hatari! Kuanzia za watoto hata za watu wazima na wakikupa tatozo linaondoka kimoja, lakini saivi utawapata wapi? Weshakwenda zao mbele za haki
 
Back
Top Bottom