Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Ni wiki ya pili sasa tangia tumemzika babu yetu mdogo, yaani baba yake mdogo mama yangu mzazi na namuomba Mwenyezi Mungu Amsamehe dhambi zake na amfanyie wepesi katika hesabu zake, na Amuweke Alipowaweka waja Wake wema....Aamin
Siku chache kabda ya kifo chake nilipata kuongea nae mambo meengi sana kwa namna ambayo nikiitafakari sasa ni kama alikua ananiaga maana si kwa busara zile alizozimwaga. Kwa ufupi tulihadithi meengi ila kuna moja lilinipa tafakari ya kina hadi leo naumiza kichwa
Babu alinambia kutokana na mambo yanavyoendelea duniani Mungu kaondoa baraka zake katika karibia kila kitu. Sababu kuu ni kwamba yale maovu makubwa makubwa kama mauaji, utesaji, roho mbaya, ulawiti ambayo yalifanya watu waliotangulia kabda yetu kuangamizwa sisi tunayafanya kuwazidi hao waliotangulia na ndio maana japo tunajiona tunaakili sana lakini ndio maangamizi ya kizazi chetu, ni rehema ya Mungu tu ndio inatuhifadhi
1. Kutakua na wanaojiita wasomi wenye uProfessor na ma Phd lakini hawana elimu, vitendo vyao
haviakisi hadhi za elimu zao bora wenye elimu za kawaida tu
2. Nyumba za ibada zitakua nyingi sana na nzuri sana na viongozi wa dini watakua wamesoma
sana dini zao lakini uchamungu kutakua hakuna, yatabaki matendo ya mwili ikiwa ni pamoja
na hadaa na hata utapeli na kujikweza kwa kujionyesha
3.Vyakula vitakua viingi sana vya kila aina lakini haviwaletei afya walaji wake na watu wanazidi
kua magoigoi kwa kila kitu hata kwa wanaume "uwanaume" wao ni wakusuasua
4. Kutakua na madawa ya kila aina lakini hayatibu magonjwa bali yanatuliza tu magonjwa na
badala yake dawa hizo zitakua na madhara ikiwa ni pamoja na kuleta maradhi mengine
mapya
Haya ni baadhi tu ya niliyoyakumbuka katika maneno ya babu yangu. Tena akaniambia wazee wao wa zamani waliiona hali hii itayokuja kwa vizazi vijavyo na wakaomba kama yeye alivyomuomba Mungu wasiishi wakaishuhudia dunia ya namna hiyo! Hata kama mambo hayo yapo kwa hivi sasa, babu alinambia bado picha kamili linakuja siku zijazo. Yajayo yanatisha zaidi!
Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Akurehemu babu yangu, wewe na wazee wako wote mliotangulia mbele za haki, mbele yako nyuma yetu