Travis Walker
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 323
- 334
- Thread starter
- #101
hapo kwenye nyekundu: 1. kuhusu mungu kutumia reference ya manabii na mitume kuhukumu watu, inaonesha jinsi gani huyo Mungu amekosa sifa ya haki, upendo na usawa. Hivi nikuulize tu je wewe hao mitume na manabii ulishawahi kuwaona? Sasa huyo mungu atawahukumu vipi watu kwa kufuata stori alizozikuta ilihari anajua binadamu hajakamilika? Lazima binadamu atatumia utashi wake binafsi.
2. Mungu angekuwa ana muonesha mtu katika njia njema basi angemuangamiza huyo shetani. Sasa imekuaje amruhusu shetani amtawale binadamu wakati anajua kuwa kabisa kuwa binadamu hakukamilika?
3. Kwanini huyo Mungu amuumbe kiumbe dhaifu halafu mwisho wa siku akamtie kwenye moto wakati yeye ndio aliyempangia awe hivyo?
4. Kwanini huyo Mungu anawaacha watu wanaishi katika mateso, chuki, dhuluma, bila yeye kuwalinda?
4. Kwanini huyo mungu amekosa njia sahihi ya kuwafanya watu wamjue yeye wakati yeye anajisifu kuwa ana uwezo, haki, na upendo sasa kwanini dini zisambazwe kwa uonevu wa vita, biashara ya utumwa, harakati na vita za kugombea dola?
5. Mungu ana umbile gani? Kama ana umbile basi nae kaumbwa. Kama hana umbo lolote basi huyo mungu hayupo
Kwa jina la Allah.
Kwanza lazima tujue kwa nini dunia imeumbwa.
"(Huyo Mungu) ndiye yeye ambae ameumba uhai na umauti(maisha na kifo) ili kukujaribuni akufanyieni mtihani yupi miongoni mwenu atatenda mema."
Quran 29:2
"Na mungu hutenda atakavyo".
Hivyo mungu hajapanga kushuka hapa duniani kuwa akuzuie wewe usifanye hili ni baya na fuata hili jema.Lakini alipanga kuwaleta mitume ili wakumbushe na kuhofisha na wawafundishe watu yaliyo mema.
Alichofanya yeye alikuumba na akakupa zawadi ya akili ili ufahamu jema na baya.
Mbona mtu anapohisi njaa hasubiri mungu amshushie chakula ila hutumia akili yake kusurvive.
Na kuhusu habari ya mitume hatujawaona ila tunaamini kupitia vitabu vya Mungu ambavyo walikuja navyo hao mitume.Hakuna mtume aliyekuwa akisema kwa matashi yake.
Hivi nikuulize tu je wewe hao mitume na manabii ulishawahi kuwaona? Sasa huyo mungu atawahukumu vipi watu kwa kufuata stori alizozikuta ilihari anajua binadamu hajakamilika? Lazima binadamu atatumia utashi wake binafsi.
Katika dunia kuna makundi mawili wenye imani na mungu na wenye kuamini sayansi, jee kuna mtu aliyewahi kumuona mwanasayansi wa mwanzo kabla ya jesus.
.Kwani wewe ulipozaliwa tu ulijua kama kuna kula, kunywa na e.t.c lakini mbona umefuata uliyoyakuta.Jee unaweza kuchagua mfumo tofauti na uliopo useme hutokula?Kwasababu umeukuta.
Sasa alijuwa wazi udhaifu wa alichokiumba na maisha yake ndio maana akaleta mitume na vitabu
ingawa wachache duniani wenye kuvifuata.
2. Mungu angekuwa ana muonesha mtu katika njia njema basi angemuangamiza huyo shetani.
Kwani shetani ana uwezo wa kumpoteza mtu?
"Na shaytwaan atasema itakapohukumiwa amri: (ya kuingia Jannah au Motoni) “Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na leo Ameitimiza); nami nilikuahidini lakini sikukutimizieni (nikakusalitini). Na sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni mkaniitikia. Basi msinilaumu, bali laumuni nafsi zenu. Mimi siwezi kukusaidieni (shida ya adhabu) wala nyinyi hamuwezi kunisaidia. Hakika mimi nilikanusha kwa yale mliyonishirikisha zamani. Hakika madhalimu watapa adhabu iumizayo."
14:22 QURAN
3. Kwanini huyo Mungu amuumbe kiumbe dhaifu halafu mwisho wa siku akamtie kwenye moto wakati yeye ndio aliyempangia awe hivyo?
Mungu hjampangia mtu kwenda motoni wala peponi ila yeye amewaekea tu vitu hivo viumbe wake.Yanayompeleka mtu motoni ni maasi yake mwenyewe.
Hivi kwasabu umekuwa maskini, unaweza kusema baba yako na mama yako ndio wamesababisha?si kila mtu anachagua njia ya maisha yake.
4. Kwanini huyo Mungu anawaacha watu wanaishi katika mateso, chuki, dhuluma, bila yeye kuwalinda?
Mungu hawaachi pasi nakuwalinda watu wanaofuata amri zake.kwa sababu watu wamemsahau na e amefanya kuwasahau.
4. Kwanini huyo mungu amekosa njia sahihi ya kuwafanya watu wamjue yeye wakati yeye anajisifu kuwa ana uwezo, haki, na upendo sasa kwanini dini zisambazwe kwa uonevu wa vita, biashara ya utumwa, harakati na vita za kugombea dola?
dini ya mungu wa kweli haijasambazwa kwa vita.kwa upande wangu kuran inasema hivi:
"Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini.Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu.Basi anayemkataa shetani na akamwamini mwenyezi mungu bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika.Na mwenyezi mungu ni mwenye kusikia na kujua"
2:256 QURAN
5. Mungu ana umbile gani? Kama ana umbile basi nae kaumbwa. Kama hana umbo lolote basi huyo mungu hayupo
Mungu tunaemjua sisi waislamu hana umbo ila kwa kusema alokuwa hana umbo hayupo utakuwa umekosea.
Kwasababu hata joto,baridi na upepo hatuoni umbo lake ila tunaona athari zake au unakataa?
"Na huyo mungu hajafanana na chochote kile"
112:3 Quran