Mungu katengenezwa na nani?

Mungu katengenezwa na nani?

Habari, nilikuwa nalisikia sana suali hili lakini leo nimeamuwa kulijibu kwa kunukuu maneno yake mungu
Kiukweli ni suali moja gumu ambalo haliwezi kujibiwa na yoyote katika dunia ama kwengine kokote kule isipokuwa yeye mwenyewe mungu ndio ana jawabu ya hili suala.
Masuali kama haya yanakuja kwasababu watu hawafahamu maana ya mungu.

Mungu ni nani?
Neno mungu ina maana nyingi lakini moja wapo ni yule ambaye ana sifa ya kuumba ama kutengeneza chochote kile pasi na kufundishwa wakati yeye hakutengenezwa.
Ina maana yoyote alietengenezwa au kuumbwa basi hana nafasi ya kuwa mungu.Ndio sisi waislamu ikawa tunaamini mungu mmoja tu ambae ni muumbaji wa kila kitu na tunakataa kuwa mtu au chochote kilichoundwa kuwa ni mungu.

Kuna msemo usemao kila kitu kilichotengenezwa kina mtengenezaji wake.Ni kweli

Lakini pia nina suali hili, jee fomula ya kutengeneza ama kuumba kaanzisha nani?
Nina Imani tukijua aliyeanzisha kuumba ama kutengeneza basi itakuwa ni wa mwanzo kabisa kutengeneza ama kuumba, kwa maana hiyo hakutakuwa na mwengine aliyekuwa akijua kufanya hivyo kabla.

Jawabu linakuwa kama ifuatavyo mungu ndio muanzilishi wa uumbaji ama utengenezaji kwa hiyo kama yeye ndiye mwanzilishi wa fani hiyo sasa inakujaje awe yeye kaumbwa wakati ndiye aliyeanzisha huko kuumba na ushahidi sahihi wa hili upo katika kitabu cha Mungu ambacho mimi nakiamini ni kuran. Kuran sura ya 112 katika aya 3 (112:3) inasema hivi "yeye hakuzaliwa wala hakuzaa."

Kwa hiyo ili itikadi ya mmoja ikimalike lazima aamini kuwa mungu hakuumbwa wala hana familia.wakati yeye ndiye wa mwanzo kuanzisha kuumba , pasi na hapo imani ya mmoja huyo haitakuwa sahihi.

Ili mungu awe mungu lazima awe hajaumbwa na yeye ndiye aliyetufundisha ujuzi huu sisi wanadamu kwa idhini yake.Na akatuekea limit ya huko kutengeneza

Hivyo kama utajiuliza suali nani katengeneza gari jawabu itakuwa mtu ndio mtengenezaji wa gari na wala gari haikuja wenyewe, na kama ukijiuliza jee mtu katengenezwa na nani basi huyo mungu ndio aliyemtengeneza mtu na kama ukijiuliza mungu katengenezwa na nani basi hutopata jibu kwasababu yeye ndiye mwanzilishi wa uumbaji wote.

Hivyo mungu hajatengenezwa ama kuzaliwa . Na kama ikiwa kuna mungu aliyetengenezwa ama kuumbwa basi huyo atakuwa siye mungu wa kweli.

Ushahidi nimetowa kutoka kwenye quran tu na kwasababu nimeona vitabu vingi vina mgongano wa huyo mungu kwa mfano bible utakuta wengine wanasema mungu ni jesus wengine wanasema hapana, jesus sio mungu ila ni mtoto wa mungu ila kuran peke yake haina mgongano katika suala la mungu ni nani.

Ametukuka mola wangu ambae hakujifanyia mtoto wala mke

Mkuu hapa unataka tuamini kuwa bwana Yesu sio Mungu. ..kwa kupitia imani yako tu. Ila sio kosa lako siku ukiutambua ukweli basi utakuwa huru, tena huru kweli kweli.
 
Dini ni mfumo sahihi wa maisha ya binaadamu kutoka kwa yule aliyemuumba.
Na sio kila mwenye dini anafuata mfumo huo kiusahihi, kuna mtu anaefuata dini na kuna mtu anaefuata matamanio ya nafsi yake.Sasa ukimuona mtu anafanya chuki kwa mwenziwe,mzinzi, anauwa basi huyo anafuata matakwa yake binafsi na wala hafuati dini kwa sababu dini yenye ukweli haina hata pahala pamoja itaamrisha kuchukiana.

Na kwasababu hiyo haimaanishi ukiwa mkiristo au muislamu ndio hutakuwa mwenye kutenda makosa. kwani wangapi wanajua ukweli lakini wana ukataa.

Atakaeokoka ni yule atakefuata kila amri ya mola wake na mpumbavu ni yule anaetaraji pepo huku anafanya makosa, awe mkiristo ama muislamu

Na pia itambulike kwamba mmoja afanyapo wema au ubaya haitomsababishia chochote huyo mungu.
Mungu anawatia watu motoni milele? sio kweli baadhi ya watu watatoka motoni kutokana na imani yangu mimi na kile kitabu ninachokisoma.Mungu anapomtia mtu motoni ni kweli hapati faida yoyte na wala hajali ila majuto kwa huyo mwenye kuchomwa kwasababu hakuna kufa.

Wakati mungu amewaumba wanadamu na majini amewapaka akili ili wachaguwe wenyewe pakufuata.Kwa maana hiyo lazima tutambue ya kwamba huyo shetani ni miongoni mwa majini hivyo ana machaguzi yake mwenyewe. kwasababu hiyo shetani alichagua kupinga na kuwapoteza wengine basi atakwenda motoni yeye na hao watakaomfuata.

Mungu hana mapenzi na wanaokufuru, mungu hana mapenzi na shetani na wenye kumfuata shetani.
Ukisikia mungu anawapenda waja wake basi upendo huo ni kwa wale wanaofuata amri zake kiusahihi.

Halafu mungu akatoa nafasi ya kusamehe pindi tunapokosea ina maana hata kama shetani ataomba msaha basi anasamehewa

Mimi sijaona watu wa jinga duniani kama atheist, halafu nahisabu wakiristo wote ni makafiri

Kama majini aliyaumba Mungu, inawezekana wakawa malaika? Sio kwamba Mungu alishachagua wawe mashetani/majini? Sasa watahukumiwa vp ikiwa yeye mwenyewe Mungu alishachagua hivyo? Yaani katuumba wadhaifu halafu tukimkosea anatutupa kwenye moto?! ...duh, Mung huyu.
 
Kwani kama utaambiwa uchague kati ya kaa la moto na tende utachukua nini?
pamoja na udhaifu uliyonao
 
Ck zt uclolijua saw na uck wa giz jarbun kusoma ili muwez ifaham ip ni din sahihi acha kufuat mkumb utapotezwa
Dini ni moyo wako na matendo yako huko siku ya judjement hutaulizwa wewe ni muslam au mkristo
 
Kutokana na andiko hili la bibilia ukiristo ni upagani
"Wakiristo maana yake ni mfuasi wa kiristo, hilo ni jina la kupanga tu. Lililotumiwa na wapagani wa antioquia"
Matendo ya mitume 11:25
Nilikuuliza WK Jana kwa nn mtume aliingia na viatu msikitini hukujibu nikakupa wk uniletee jibu umeleta? Unapiga kelele tu
 
Maneno yako yanasibitishwa na 2:255 Qur'an.
"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu."
2:255 Qur'ani Albakara
C kweli
 
Mwanzo wa UZI huu nilidhani hautahusisha matumizi ya vitabu vya dini.
Nilidhani Great thinkers watasugua vichwa na kuja na majibu ya kidunia ukiingiza dini UMEJIFUNGA majibu ni ya KUKARIRI zaidi ikiongozwa na wapi? Ulipoikuta dini yaani umezaliwa baba/mama (waislam/wakristo) ukafuata mkumbo.Dini hizo zinakusomea waumini ni kulishwa tu .
Kujifanya kujua sababu ya KUKARIRI mwisho wa yote hakuna masikilizano kila MTU anajifanya anajua sababu tu kakalilishwa WAUMINI tuwasikilize wakuu wetu wa dini husika wanatufundisha nn wao wamesomea ndo maana tafsiri zao tunazikubali.
 
Bora hata wewe umeliona hilo, Mara oooh sjui Quruan ngapi ngapi ..Mara biblia ngapi ngapi,
Wamesahau kabisa sababu ya kuja hizo dini Africa na historia juu ya uislam na ukristo.

Wengiwetu tunatetea dini kwasababu tumekuta wazazi wetu ndio wanazitumia .
 
Wewe unaongea kwa matamshi yako .Na kama huongei kwa matamshi yako tupe ushahidi wowote kutoka katika kitabu usemao
hayo maneno si kweli
Nilikuuliza swali kabla ya mtume waislam walitumie mwongozo upi?
Hukujibu

Nikakuuliza kwa nn mtume aliingia na viatu msilitini hukujibu yote hayo mawili

Ndio sasa nikaona huna uhakika wala huna uelewa na hayo unayoyaongea ndio nikasema c kweli niambie umefundishwa majibu au!!
 
Kama majini aliyaumba Mungu, inawezekana wakawa malaika? Sio kwamba Mungu alishachagua wawe mashetani/majini? Sasa watahukumiwa vp ikiwa yeye mwenyewe Mungu alishachagua hivyo? Yaani katuumba wadhaifu halafu tukimkosea anatutupa kwenye moto?! ...duh, Mung huyu.
Hili swali najiulizaga sana, kama Mungu anajua A to Z about you kabla hata haujazaliwa (kwamba utazaliwa hosp flani, na utakufa sehem flani either ukiwa bado una dhambi sasa ,kwann aliruhusu ukazaliwa na alijua dhahiri kuwa mwisho wako utakufa ukiwa na dhambi.
 
Kumbe Yesu sii Mungu eeh!!nilitaka kushangaa,mungu gani anapigwa bakora na aliowaumba "bana"?ahsante kwa taarifa na kunifumbua macho.

Mnaemwita Nabii Issa sisi huyohuyo tunamtambua kama Yesu Kristo mwana wa Mungu ambaye ni Mungu pia..,, Katika Quran yenu mnaandika aya kwamba moja ya miujiza aloifanya ni kuumba ndege wa udongo na kumpulizia pumzi kisha kuruka.,, kwa kifupi alishiriki uumbaji

Swali ni Je kuna mwanadamu aliwahi kutengeneza au kufanya kitu chenye pumzi..?? Na kama hakuna basi hata Quran yenu inakiri Yesu Kristo ni Mungu....!!!
 
Nilikuuliza swali kabla ya mtume waislam walitumie mwongozo upi?
Hukujibu

Nikakuuliza kwa nn mtume aliingia na viatu msikitini hukujibu yote hayo mawili

Ndio sasa nikaona huna uhakika wala huna uelewa na hayo unayoyaongea ndio nikasema c kweli niambie umefundishwa majibu au!!
 
Dini ni mfumo sahihi wa maisha ya binaadamu kutoka kwa yule aliyemuumba.
Na sio kila mwenye dini anafuata mfumo huo kiusahihi, kuna mtu anaefuata dini na kuna mtu anaefuata matamanio ya nafsi yake.Sasa ukimuona mtu anafanya chuki kwa mwenziwe,mzinzi, anauwa basi huyo anafuata matakwa yake binafsi na wala hafuati dini kwa sababu dini yenye ukweli haina hata pahala pamoja itaamrisha kuchukiana.

Na kwasababu hiyo haimaanishi ukiwa mkiristo au muislamu ndio hutakuwa mwenye kutenda makosa. kwani wangapi wanajua ukweli lakini wana ukataa.

Atakaeokoka ni yule atakefuata kila amri ya mola wake na mpumbavu ni yule anaetaraji pepo huku anafanya makosa, awe mkiristo ama muislamu

Na pia itambulike kwamba mmoja afanyapo wema au ubaya haitomsababishia chochote huyo mungu.
Mungu anawatia watu motoni milele? sio kweli baadhi ya watu watatoka motoni kutokana na imani yangu mimi na kile kitabu ninachokisoma.Mungu anapomtia mtu motoni ni kweli hapati faida yoyte na wala hajali ila majuto kwa huyo mwenye kuchomwa kwasababu hakuna kufa.

Wakati mungu amewaumba wanadamu na majini amewapaka akili ili wachaguwe wenyewe pakufuata.Kwa maana hiyo lazima tutambue ya kwamba huyo shetani ni miongoni mwa majini hivyo ana machaguzi yake mwenyewe. kwasababu hiyo shetani alichagua kupinga na kuwapoteza wengine basi atakwenda motoni yeye na hao watakaomfuata.

Mungu hana mapenzi na wanaokufuru, mungu hana mapenzi na shetani na wenye kumfuata shetani.
Ukisikia mungu anawapenda waja wake basi upendo huo ni kwa wale wanaofuata amri zake kiusahihi.

Halafu mungu akatoa nafasi ya kusamehe pindi tunapokosea ina maana hata kama shetani ataomba msaha basi anasamehewa

Mimi sijaona watu wa jinga duniani kama atheist, halafu nahisabu wakiristo wote ni makafiri
Mkuu hayo uliyoandika umeyatoa wapi?naona umekuwa msemaji wa Mungu!
 
Back
Top Bottom