Mungu saidia Lesotho ishinde!

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
3,732
Reaction score
6,561
SABABU ZA UZALENDO KUNITOKA NI HIZI HAPA.
1- Walioteuliwa kuunda kamati ya uhamasishaji siyo wanasoka. Hakuna hata mmoja aliwahi kuichezea timu ya taifa, wengine ni watu wenye scandal mbaya kama Wema Sepetu.

2- mechi iliyopita dhidi ya Lesotho kocha alijaza mabeki tupu mchezoni kana kwamba tumeenda kuzuia tu. HAKUNA MECHI MBAYA NILIYOWAHI KUSHUHUDIA KAMA ILE.

3- Kikosi kilichotajwa kushindana na Uganda hakikutajwa kama ilivyopaswa..... Nyoni na Yondani wamekuja kuitwa baadaye ila bado kuna mapungufu mengi sana hasa eneo la viungo washambuliaji.

4- Kocha anajiona sana. Hafuatilii ligi kujua wachezaji bora ni wapi..... SIJUI KWA NINI BANDA, DILUNGA, HAJIB, NA YULE BEKI KITASA WA AZAM HAWAKUJUMUISHWA........ nashangaa sana uwepo wa kichuya na ulimwengu.

NATAKA LESOTHO WASHINDE DHIDI YA CAPE VERDE HALAFU NIONE ILE KAMATI ITAFANYA NINI.
 
Sababu zako ni za chuki na mhemko ukitulia hasira zikakuishia utabadili msimamo.

Huna tofauti na wanaoombea tushindwe ili kocha afukuzwe.

Hopeless kabisa
 
Vizuri wote ni watoto wa Mungu na wote wanamuomba Mungu washinde na kwa kuwa wote ni watoto wake hatatoa upendeleo kwa mtoto yeyote atasimama katikati ili mwenye juhudi ashinde.
 
Vitalis Msungwite hata mimi sipendi ujinga wa viongozi na wasimamizi wa soka bongo kwa kuhamasisha pale tumeshakwama baada ya kuzembea mechi za awali.

Ila tuombe tupite na sisi tuonekane Afrika au tukatie aibu kwa kupigwa vipigo heavy
 
Hayo ni mawazo yako binafsi. Mtanzania mwingine atakuwa na mawazo tofauti na mwingine atakuja na yake. Kuhusu nani acheze, ni kocha pekee ndiye mwenye neno la mwisho kwani, kama nilivyosema hapo juu, kila mtu atakuwa na mawazo yake tofauti. Kama wewe ungekuwa kocha basi ungewaweka hao wakina Banda, Dilunga, n.k. na Mtanzania mwingine angekusuta kwa kuwaweka hao na kumwacha fulani na fulani. Tumwachie kocha afanye kazi yake. Zaidi ya hayo tusikose uzalendo eti kwa kuwa kamati ya uhamasishaji si ya watu waliocheza soka. Wewe mwenyewe unayewataja wanaopaswa kuwa kwenye timu sijui ulichezea timu gani: ya taifa, au ya klabu gani? Kama hujafanya hivyo kitu gani kinakufanya uweze kuwakosoa wengine eti kwa sababu tu siyo wanasoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…