Mungu siku zote yupo kimya na haongei, nyie mnampigia kelele

Mungu siku zote yupo kimya na haongei, nyie mnampigia kelele

Bsyotyo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2022
Posts
617
Reaction score
996
Habarini Ndugu. Najua hii Itakuwa Mpya Kwenu na Siku zote itawafungua Macho wengi nyie Mliowekwa kwenye Giza Kubwa na Kuishia Kuabudu Viumbe vyenye Tamaa ya Kujiita Mungu

Hizi ni Sifa za Mungu mwenye Vyote. Aliyeumba Kila Kitu Na Kila Kiumbe Vinavyoonekana Kwa Macho na Visivyoonekana. Tuanze

1. Mungu haongei

Mungu mwenye Vyote unavyoviona haongei maana Hana Mfumo wa Kuongea kama Wewe na Mimi tunavyoongea. Ili Mungu aongee anatakiwa Awepo Mungu mwingine aliye kama Yeye Wa Kufanya Naye Maongezi

Siku zote amefanya Mambo yake kwa Ukimya na Ameumba Viumbe Wanaoongea ..wanaosema sema..wasiosikia..wasioona..wasiotembea..wasio na Miguu.. Amefanya Viumbe wa Kila Aina ukiwemo wewe Mwanadamu unayejipa Priority sana

2. Mungu hapendi na Wala hana Mapenzi na Viumbe wake


Mungu Ana Enzi tu na Viumbe wake ila Hana Mapenzi na Viumbe wake. Mapenzi yanatokana na Mapendo wanayoonyeshana Viumbe kwa Viumbe. Wewe binadamu utampenda Binadamu mwenzako na Huyo ndie utakayemuonyesha Mapenzi. Mungu hana Hicho kitu kwamba Kampenda Binadamu sana Kuliko Kuku. Kampenda sana malaika kuliko Shetani.. Kampenda sana Konokono kuliko Bacteria. Yeye ana Enzi na Viumbe wake wooote hana Mapenzi na Viumbe wake hata Mmoja

3. Mungu si Mmoja Na Wala Si Wengi

Wingi na Umoja Umetokana na Viumbe Kujua Namba baada ya Namba Kuanza Kutumika ndipo Hesabu za Wingi na Umoja Zilipoanza. Mungu hayupo katika Mahesabu Yenu. Anapoitwa Mwenye Enzi Mungu(Mwenyezi Mungu) hahesabiki kwa Hatua zenu kwamba Ni Moja au Mbili. Maana Yeye Hayupo katika Uhesabikaji huo mlionao Nyie. Maana hata Hesabu hazina Mwisho ukianza Kuhesabu 0 1 2 3 4 5. Hutokuja kupata Namba ya Mwisho

4. Mungu si Mkubwa wala si Mdogo

Utasikia watu wanasema Mungu wetu ni mkubwa. Ni makosa maana Mungu hana Size utakayoweza Kumpima na Kusema ana Ukubwa Huu au Udogo Huu. Mungu hayupo Hivyo. Yaani huwezi kusema Mungu kaanzia Hapa na Kaishia Hapa

5. Mungu haonekani

Mungu haonekani kwa sababu hayupo katika Mithili ya Rangi. Ili ww binadamu uone

6. Mungu si Mzima wala si Mfu

Mungu hana Uzima maana Hana Mwili na Wala si Mfu. Uzima ni wa Mwili

7. Mungu si Hai

Mungu si Hai kwa sababu haishi na Hatumii Roho. Uzima wa Mwili ndani yake ndio kuna Roho (memory card) ambayo ndio unapata Neno Kuishi.

8. Mungu si Mme wala Mke

Mungu si Mme kwa sababu siyo Bwana. Mme au Bwana ni Jinsia iliyoanza Katika uzazi, kwa sababu neno Bwana Linaanzisha Uzazi.. Si mke pia kwa Sababu si Bibi mzaliwa. Hawa ndio huleta Watoto kwahiyo Mungu hajakaa Kama Bwana Wala Bibi

9. Mungu si Mshiriki

Mungu si Mshriki kwa Maana Kwamba Hashirikiani na Kiumbe Chochote kile kwa Mambo yake. Mungu hatumi wala kutuma Kiumbe Kikafanye Kazi zake . Hii Ikiwa na Maana Ya Kwamba Kushirikiana ni Viumbe kwa Viumbe sisi ndio tunashirikiana katika Mambo Yetu ya Hapa na Pale kwa Ajili ya Kutimiza Mahitaji Yetu

10. Mungu si Kiumbe

Mungu si kiumbe kwa Maana Hakuumbwa. Viumbe ndio wameumbika.

Elimu hii Imetoka kwa Mtu wa Kwanza na Watoto wake na Kurithiwa na Vizazi mpaka Leo hii na Haijapotea

Sasa Mtafuteni Huyo Mnayemwabudu leo hii Muone kama Anakaa Humo,Ukikuta Hawapo hivyo Jua Kwamba Mnaabudu Viumbe. Maana baada ya Upotevu kutokea Katika Muhula wa Kumi na Mbili. Ibada za Viumbe zilishamiri Ulimwenguni. Viumbe kwa Viumbe Vikitaka Kutawalana na Kijikweza Na Kujiita Mungu

Mashetani, Malaika na Binadamu n.k n.k wengi wametaka Kuabudiwa kuwa ni Mungu

1. Binadamu waliwafanya Binadamu wengine Wawaite Mungu na Wakatawala Miaka Hiyo. Wafalme wengi walichonga Sanamu na Kuwaamuru Binadamu Wenzao Wawaite Mungu na Kusujudu. na Baadhi Ya Binadamu (Hasa Manabii na Mitume) kuwaambia Binadamu Wengine kwamba Wao wametumwa na Mungu, ikiwa uhalisia Hawajatumwa na Mungu ila Wametumwa na Wakuu wao wenyewe kwa Maslahi yao Binafsi

2. Hivyo hivyo kwa Mashetani (Majini) nao waliwafanya wenzao kuwaabudu na kuna Visa Vingine viliandikwa hadi kwenye Vitabu vya Dini kwamba Walipigana Huko kwenye Kutawala kwao na Mmoja Akafukuzwa Huko Kwa Kukataa Baadhi Ya Mambo ya Mtawala wake Mkubwa

3. Hivyo hivyo Malaika Nao Wanatawala zao na Wakubwa wao.. Ndio pia Huweza Kuja na Kufanya Vyovyote kwa Viumbe Wengine na Kuwatawala.Mfano mzuri Ni Kuwatokea Binadamu Na Kuwaambia Wafanye Hivi au Vile huku wakijinadi Wametumwa Na Mungu.. Kama Ww unavyotawala Viumbe wengine

HUU NDIO UKWELI UTAKAWAWEKA HURU AKILI ZENU NA MAISHA YENU KWA UJUMLA
 
Weka na ushahidi wa haya unayosema. Umeyajuaje haya? Umepata kuwa naye?
 
Weka na ushahidi wa haya unayosema. Umeyajuaje haya? Umepata kuwa naye?

1. Ushahidi Ni Kitabu cha Wazee wetu Kilichotunzwa afrika kiitwacho SENDE ESUPRY DEWO OCHI (kibantu) kiswahili chake ni ELIMU ILIYODUMU KATIKA JADI na Mwalimu wake ni Row Omonige.

2. Elimu ya Wazazi wetu wa Kwanza Kuumbwa

3. Huwezi Kupata Kuwa na Mungu maana Yeye si Kiumbe kama Wewe Ulivyo kwamba Uweze Kuongea naye
 
1. Ushahidi Ni Kitabu cha Wazee wetu Kilichotunzwa afrika kiitwacho SENDE ESUPRY DEWO OCHI (kibantu) kiswahili chake ni ELIMU ILIYODUMU KATIKA JADI na Mwalimu wake ni Row Omonige.

2. Elimu ya Wazazi wetu wa Kwanza Kuumbwa

3. Huwezi Kupata Kuwa na Mungu maana Yeye si Kiumbe kama Wewe Ulivyo kwamba Uweze Kuongea naye
1. Hawa wazee walioandika walitumwa na Mungu au ni utashi wa wakubwa wao kwa maslahi binafsi?

2. Elimu ya wazazi wa kwanza, hawa si ndo walitufundisha na kuhesabu pia? (Zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia na vilivyomo) Lakini hizo hesabu we unazikataa kabisa.

3. Sasa we umejuaje yote haya kwani uliwahi kukaa nae mahali ukamjua Mungu hadi utufundishe hapa? Umetumwa na Mungu au ni utashi wako kwa maslahi yako binafsi?
 
Mnahangaika na Mungu kupoza uchungu wa Maisha na kumsingizia na yeye alivyo Mwamba anawaacha muendelee kupigika vizuri.
1. Ndugu yangu Huo Uchungu wa Maisha Umeupimaje Kwenye Thread Hii?

2. Kwani Wanaohubiri Hasa Papa ,Masheikh,Mapdri Kwamba Mungu Yupo Hivi au Vile nao Wanauchungu Wa Maisha?

Uchungu au Furaha katika Maisha Hauwezi Mzuia Mtu Kusema Ukweli au Kuhoji na kukaa Katika Mijadala
 
1. Hawa wazee walioandika walitumwa na Mungu au ni utashi wa wakubwa wao kwa maslahi binafsi?

Nishaandika Ndugu Mungu hashirikiani na Kiumbe chake. Kwahiyo Mungu hakutuma Mtu aliacha Muujiza wake Utende Mambo yote pamoja na Elimu hiyo Kutoka Kwa Mtu wa Kwanza.

2. Elimu ya wazazi wa kwanza....hawa si ndo walitufundisha na kuhesabu pia? (Zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia na vilivyomo) Lakini hizo hesabu we unazikataa kabisa.

Hiyo Sentensi uliyoandika si Sentesi ya Wazazi wa Kwanza. Kuzaa hata Wasipotamka Wao Lazima Viumbe wazaane. Mungu aliweka Mfumo wa Uzazi kwa Mwanaume na Mwanamke.. Kwa Kuku jike na Kuku Dume. Kwahiyo Hiyo ni Mifumo Ambayo si Lazima Uambiwe Kazaeni Ndio Uzae . Kuzaa ni Lazima Maana Umewekewa Mifumo toka Mwanzo.

Jiulize Kwani Kuku,Ng'ombe,Bata,Kenge,Sungura n.k wanazaa. Kuna Mtu aliwaambiaga Wazaane?

Mtu wa Kwanza Hakufundisha Kuhesabu wala Kuandika. Hesabu zimekuja Mbeleni sana baadae. Mfano mzuri Nenda Porini huko kutana na Mmasai au MMbulu Halafu Mwambie Hakuhesabie 1 mpak 10 hatoweza au Akuandikie 1 mpka 10. Kwahiyo Hesabu Zimekuja Majuzi tu. Na Afrika Zilianza Baadae Pia Na Tulikuwa na Hesabu za Kibantu. Mosi(moja) Kabhili(mbili). Kenda(tisa ya leo)
3. Sasa we umejuaje yote haya kwani uliwahi kukaa nae mahali ukamjua Mungu hadi utufundishe hapa? Umetumwa na Mungu au ni utashi wako kwa maslahi yako binafsi?
Nimekuambia Elimu hii ilipotoka. Kiumbe hawezi Kukaa na Mungu.. Kiumbe Atakaa Na Kiumbe Mwenzake Na Wao ndio watapeana Elimu. Na Kurithishana Elimu hiyo Kizazi mpaka Kizazi.

Elimu hii Ni ya Mtu wa Kwanza Na Yeye Ndie Aliye na Ukweli kuzidi Viumbe wengine wa Kufanana naye Wote na Yeye ndie aliyerithisha Elimu hii kwa Wengine. Kuanzia alipozalika Ulaya ya Kati Mpaka Afrika Huku
 
Mungu Ni Aphla na Omega
Alpha -Mwanzo
Omega-Mwisho

Hapo Tayari ushamkadiria alivyo. Na Hata Unaweza Kupima Alivyo. Maana Mwanzo wa Kitu unaujua na Mwisho wake pia utakuwa unaujua

Mungu ni Enzi- Enzi haipimiki
 
Mnahangaika na Mungu kupoza uchungu wa Maisha na kumsingizia na yeye alivyo Mwamba anawaacha muendelee kupigika vizuri.
Inatafakarisha sana hii!

Ila ina ukweli kwa kiasi kikubwa.

"Mungu atasaidia" kumbe msela anajipoza tu na Mungu anamchora tu matokeo yake maumivi au matatizo yanabaki palepale!
 
Back
Top Bottom