Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Namba 3 uko sahihi kabisa..
Mengine sijui


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mungu anatengeneza njia " ebu tuambie zipi izo njia Mungu anazotengeneza hili mashetani waangamizane, pili vip mungu aepuke lawama za uuaji wakati yeye ndio bwana mipango ?
 
Jf inawezekana Kuna majini mashetani maagent wa ibilisi wengi sana. Tujihadhari kwa post zao, kwa nn kila siku wanakuja na hoja za kumpinga Mungu.
 
"Mungu anatengeneza njia " ebu tuambie zipi izo njia Mungu anazotengeneza hili mashetani waangamizane, pili vip mungu aepuke lawama za uuaji wakati yeye ndio bwana mipango ?



Ngoja nikupe mfano hai ndipo utaelewa, kulitokea wezi wawili na kila mmoja alikuwa na nia ya kuiba sehemu fulani bila wao kujuana kuhusu jambo hilo lakini wao walikuwa wanafahamiana kwa tabia ya wizi, ikatokea siku moja wakakutana mahali fulani kwa bahati kabla ya kufanya tukio la wizi , walipokutana tu kila mmoja akatambua dhamira ya mwenzake hivyo wakasalimiana lakini kila mmoja akiwa na chuki moyoni juu uwepo wa mwenziwe mahali pale na hii yote ilitokana na kila mmoja kuwa na tamaa ya kutaka kuiba zile mali pekee yake, kilichotokea wakaondoka mahali pale kwa pamoja kirafiki na kwenda falagha kujadiliana huko falagha mmoja akamuwahi mwenzake na kumuua na kabla hajatoroka akashikwa na watu akala kibano kabla ya kuchukuliwa na polisi kwa upelelezi zaidi.

Hapo sasa unaona wahalifu wakidhuriana na kushindwa kutimiza dhamira zao za uhalifu, na ndivyo kama hivyo mipango ya Mungu inavyofanya kazi.
 
1.Fungu la kumi linahitajika kama shukrani kwa MUNGU mkuu nakushauri usome biblia vizuri.
3, Nabishana na wewe.
Mungu kamuumba binadamu ili amtumikie na kumpa uhuru wa kuchagua yeye mwenyewe.
Hata Yesu alifunga kwa hiyo utaona maombi ni muhimu.
Ufalme wa mbingu unapatikana vigumu ndugu so pambana kuutafuta ufalme wa mbinguni.
Kwa namna uliyoweka hapo sidhani kama kungekua na haja ya uwepo wa MUNGU.
 
Siri zipo hapa Vatican Inamiliki Dunia - JamiiForums
 
Itakuaje kama Mungu ndio kafanya wale wawe waharifu kwa uwezo wake aliokuwa nao ?
 
Nikweli mungu hana njaa ya hivyo vitu, ila wapo viumbe wanaohitaji misaada. Mi sadaka huwa nawapa wanaohitaji. maskini na mafukara. kama nitapeleka kwenye nyumba za ibada nitapeleka kwa lemgo la kuchangia labda ujenzi NK.
 
Yesu Kristo alipokuja Kwenye agano jipya mbona hajazungumzia kuhusu swala la zaka?
Kama kuna mahali alizingumzia Naomba Mwenye andiko anipe
 
Halafu agano la kale limeanisha matumizi ya zaka !
Mfano kutegemeza wajane na yatima n.k
Swali ni Je yanafanyika hayo?
Kwa asilimia ngapi ?
 
Mimi nazani kuna haja ya kuwepo na sheria ya kufanya auditing ya hesabu za taasisi zote Za kidini !
Ili kuona mambo Yao yanavyo endeshwa
 
Halafu bora hata wangekuwa wanafungua hospitals na Shule na huduma nyingine Za jamii ambazo wananchi wangeweza kupata huduma kwa unafuu lakini wala!
 
Oneni Kakobe alivyo kutwa na zile billioni Za pesa [emoji87][emoji87][emoji87]
Lakini waumini wengine hata nauli hawana, wamechoka ile mbaya!
Angefungua hospital ambayo baadae ingeleta faida pia
 
Halafu Siku hizi mahubiri ya utoaji sadaka ndo yameshika kasi kweli kweli na changizo!
 
Mahubiri ya utaua na utakatifu yamekuwa adimu!
Wewe vaa hata robo tatu uchi hakuna atakae kuonya wala kukemea
 
Unakuta yuko kanisani amevaa utazani yuko night club [emoji87][emoji87][emoji87]
Cha ajabu hakuna wa kumuonya wala nini!
Hapana naona si Sawa hata kidogo!
 
Halafu kumejengeka misingi ya nidhamu ya woga kwa kiwango cha hali ya Juu kiasi Kwamba Mtu akijaribu kuhoji anaonekana muasi!
Kitakachofuata ni kutengwa!
Mioyo wa wanadamu hii Mmnh !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…