Ndiyo maana nikasema wewe bado ni "dogo sana" kifikra. Njia rahisi ya wewe, nadhani, ni kutumia mifano tu ili uelewe hekima za Mungu.
Wewe mbele ya Mungu ni chini zaidi kuliko wewe jinsi unavyommiliki mbuzi wako, leo ukiamua kumchinja mbuzi wako na kupika supu nani atakuuliza??, halikadhalika kama Mungu angeamua kukufanya wewe uwe kitoweo chake ungeropoka " that's unfair ??!!" wakati huna lolote la kumfanya kwani yeye atabaki kuwa Muumba wako na wewe utabaki kuwa kiumbe chake, full stop.sasa kiburi cha kumjudge Mungu eti, kawa muuaji unakitoa wapi??, naam, Mungu atawaua wale ambao ni majeuri na waharibifu na mafedhuli katika ardhi kama Firauni alivyokuwa.
Eti, unaendelea kumkosoa Mungu kwanini kamfanya Firauni awe na moyo mgumu na kisha kumuadhibu.
Nimesema upeo wako wa kuelewa falsafa ya maneno ya Mungu ni mdogo na inaonekana umetawaliwa na jazba (emotions).
Firauni alikuwa ni jeuri mno na hakukubali kabisa jambo lolote aliloambiwa na Musa (as) na kilichompa jeuri na kiburi ni mali, ufalme na kuogopwa na raia na hasa Waisraeli, Musa akamuomba Mungu aangamize mali zake na hatua hii ilikuja baada ya hatua mbalimbali kushindwa na inaonyesha kamwe Firauni asingekubali kunyenyekea mbele ya Musa, ndipo Mungu akakubali maombi ya Musa kwa kumdhoofisha katika mali jambo lililomfanya Firauni awe na kiburi na jeuri zaidi kuliko hapo kabla kwasababu musa alimueleza kuwa kuanguka kwa mali zake ilitokana na hasira za mungu juu yake. Hivyo maneno "kutia ugumu moyoni" maana yake ni jeuri na kiburi na hasira na adhabu za Firauni zilizidi dhidi ya waisraeli kutokana na yale matokeo ya adhabu ya Mungu na hatimaye Mungu akamgharikisha baharini. Sasa huo ndiyo ufafanuzi wa habari hiyo.
Nikupe mfano mmoja; unapowinda chui "(a feral leopard)" anaponasa kwenye mtego ili kumuua kirahisi wawindaji humsogelea karibu na kumsakizia mti "(a poking pole)" ili kumpandisha hasira na mara moja ataung'ata huo mti na hapo inakuwa rahisi kumtwanga risasi, hapo kwa fikra zako utauliza kwanini apandishwe hasira halafu auawe??!!, mfano huo ndiyo jinsi Firauni alivyotiwa ugumu wa moyo na Mungu ili aangamizwe kwa sababu hatua aliyofikia ni "point of no return" na hakuwa tena mtu wa kheri.