Mungu wa Mbinguni mrehemu Hayati Magufuli, Saba Saba magari yanateleza tu. Kilwa road haina foleni Flyover mkombozi!

Kuna maeneo alikuwa na madhaifu yake kama Mwanadamu lakini kwenye Ujenzi wa miradi amejitahidi sana

Saivi ukiambiwa uoneshe hata mradi mmoja pamoja na kukopa na kupigwa tozo za Dr Mwigulu lakini huoni sana sana utaoneshwa miradi ya madarasa na Vyoo πŸ™Œ
 
Alikuwa akipambana tu na hali yake, sasa hayupo tena nasi. Utawala wake imebakia kuwa ni historia lakini tutamkubuka kwa upendeleo wake wa kikanda, na kwa "home town" yake ya Chato, na deni kubwa la taifa ambalo serikali aliyoiongoza ilituachia.
Mboe alikimbilia kwao Dubai aliporudi tu akatiwa mbaroni na Kingai kwa ugaidi🀣🀣
 
Bwashee, hizo ni matokeo ya kodi na madeni ya Watanzania. Jamaa alikuwa ni mwajiriwa tu, na aliyoyafanya yalikuwa ni kipaumbele cha taifa letu kwa wakati huo.
Eehh sawa, Na anayofanya wa Sasa nacho ni kipaumbele Cha Taifa
 
Usipimbazwe wewe magufuli alikua mwizi mkali kama hujui
 
kwani hayo madarasa si wanasoma watanzania? hivi nyie wajinga mtaelimika lini? kwenu madaraja ni bora kuliko elimu ya watoto wenu? saivi kila mkoa inajengwa shule maalum ya sayansi kwa wasichana. lakini tarula tunaona saiv wanavyopambana na barabara za vijijini na mambo mengi tu yanafanywa sema mmekariri madaraja madaraja.
 
Kasi ya Ujenzi wa hiyo miradi iendane na fedha tunazokopa kila siku pamoja na hizi Tozo tunazopandishiwa kila leo.

Uje huku Vijijini utuoneshe hizo barabara unazosema zinajengwa na Tarura, barabara za Vijijini boss wangu ni disaster.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…