Muombee Adui Yako Njaa; Maandamano Yanayoendelea Kenya Yawafurusha Watalii 800 na Kukimbilia Tanzania.

Muombee Adui Yako Njaa; Maandamano Yanayoendelea Kenya Yawafurusha Watalii 800 na Kukimbilia Tanzania.

Mimi nimeshangaa wapigaji wa 40bil wanaamishwa ofisi floor ya juu na kupelekwa ofisi floor ya chini kabisa!.
Mimi nimesikitika mwenye mamlaka yote anashindwa kuchukua hatua kwa majizi na mafisadi alafu anaishia kulalamika na kuishia kuwaambia eti nawao watakufa na pesa zote wataziacha hapa duniani...😂🤣
 
Pole yao sana majirani... Vita ya panzi furaha kwa kunguru...
 
Tuachane na hayo,
Jamani I wish na Mimi nije kuwa mtalii kama hao wazungu ni mwendo waku Cruz across the world 🥰
Life is so beautiful
Seems unapenda adventure kama nipendavyo
 
Mzee RAO anamuangamiza kiuchumi Rais Ruto na makamu wake Gachagua kupitia maandamano.

Meli ya kitalii iitwayo MV Seabourn Sojourn, iliyopo njiani kwenda nchi mbalimbali duniani, ambapo kwa afrika mashariki ilikuwa isimame kwa siku 6 kwenye bandari ya Mombasa, sasa imebadiri uelekeo hadi Tanzania kutokana na maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Kenya.
View attachment 2573107
Meli hiyo inayotoka Mahe, nchini Shelisheli, ina watalii 800 sasa itatia nanga kwenye visiwa vya Zanzibar na Dar es Salaam kwa siku sita kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

Meli hiyo ilianza safari yake huko Miami Florida, mnamo Januari mwaka huu, ambapo safari yao inategemewa itakamilika Mei 27 huko katiak jiji la Barcelona, Uhispania.

Awali Kenya ilikuwa kwenye ratiba ya safari ya Mv. Seabourn Sojourn ambapo ilitegemewa kutia nanga katika bandari ya Mombasa.

Kufuatia hali hiyo nchi hiyo imepata athari kwenye sekta ya utalii huku wadadisi wakisema taifa hilo la Afrika Mashariki linapoteza mamilioni ya dola za kimarekani.

“Tumepoteza pesa nyingi sana, kutokana na matumizi ya awali, kila abiria hutumia angalau usd 200 kwa siku, kwa siku tatu hizo ni usd 600, tumepoteza usd 800,000, tukichukulia kila mmoja angetumia kiasi hicho,” kauli ya Bw Masemo, kutoka nchini Kenya.


Credit: The Citizens
Ila ujiandae na wewe kuombewa njaa siku moja na jirani yako ila usiokote mawe na kuyarusha kwake.😂
 
ni bure tu, TZ inakosa miundombinu bora kwa ajili ya Utalii
Hebu angalia hapa hii meli ilipotia nanga, ni hapo hapo meli za mizigo nk hutia nanga na hadi hapo haziwezi kuja hadi hiyo iondoke.
IMG_20230415_071718.jpg
 
Mombasa imetengenezwa katika hali maalumu ya watalii kufurahi, muunganiko wa bandari na sehemu za starehe zipo programed well, Dar yetu cruise ikitia nanga mazingira yanakwaza, atleast zanzibar pako ok!
N. B, IPO HAJA KWA MAMLAKA HUSIKA KULIANGALIA JAMBO HILI KWA AJILI YA CRUISE SHIP TOUR, GATTY LA CRUISE LIJENGWE WAPI, NA WATAKAPOSHUKA WATAELEKEA WAPI PA KUWAPA RAHA, NA SI KUBASE TU SERENGETI NA MBUGANI NI LAZIMA VYANZO VYOTE MUHIMU VIWE ACTIVATED.
Watanzania wenyewe tunakerwa ma sehemu za starehe full upuuzi.

Mawaziri wanakenua tu
 
Tuachane na hayo,
Jamani I wish na Mimi nije kuwa mtalii kama hao wazungu ni mwendo waku Cruz across the world [emoji3059]
Life is so beautiful
Mbona waweza na bei sio kubwa kihivyo.

Angalia cruisers ambazo zinapita Afrika ie South Afrika au Uanzie safari Dubai
 
Bandari ya Malindi ilitakiwa iwe kwa ajili ya Utalii tu, Mizigo na masuala ya Abiria yalitakiwa viwepo maeneo mengine.
Nilibahatika kufika eneo jipya panapojengwa bandari mpya kule mangapwani, nadhani itapendeza ikiwa malindi pataboreshwa na kuwa special zone of tourism, sababu ni eneo tayari lina miundombinu na ni karibu na stone town ambayo ndilo eneo maradufu kwa utalii.
 
Back
Top Bottom