Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Mwombolezaji Leah Ngowi, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 mkazi wa Kiboriloni wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, amefariki dunia akiwa kwenye msiba wa aliyekuwa mwanafunzi wa Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), James Temba (24).
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Mei 7, 2026, wakati baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mkesha wa msiba huo kijijini Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia tukio hilo, shangazi wa marehemu, Ruth Fabian amesema walikuwa wamepumzika usiku huo msibani, ndipo mtu mmoja alipowaamsha ili wanywe chai.
Amesema alipoinuka, alimwamsha mama huyo lakini hakuitika.
Soma Pia: Mwili wa James Temba, aliyepotea umeokotwa mto Msimbazi ukiwa hauna kichwa
“Licha ya kumtikisa mara kadhaa, hakuonesha dalili yoyote ya uhai, jambo lililotulazimu kuwaita ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa msibani hapo,” amesema Ruth.