SoC01 Muonekano hutengeneza uwezekano

SoC01 Muonekano hutengeneza uwezekano

Stories of Change - 2021 Competition

Mr Excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2021
Posts
526
Reaction score
1,675
Maisha ya mwanadamu kiujumla yanatengenezwa na muonekano wa kila siku anaojitahidi kuutengeneza katika mazingira yanayomzunguka. Je, muonekano ni nini? Uwezekano ni nini? Kanuni hii ni siri kubwa iliyo sheheni vipengele muhimu sana vyenye siri ya mafanikio.

Muonekano ni taswira ya nje jinsi binadamu anavyojihusisha na shughuli za kila siku ila uwezekano ni nguvu ya asili ambayo ipo ndani ya mwili wa binadamu ikiiamshwa inafanya mambo makubwa sana katika jamii.

Kila binadamu hapa duniani ana tamani kufikia malengo yake makubwa ya kimafanikio aliyojiwekea, wengine wanatamani kuwa viongozi wakubwa, wafanya biashara, wanasiasa wakubwa na wengine wanatamani dunia iwafahamu kwa uwezo mkubwa na talanta walizo nazo, hasa wewe ambaye unasoma Makala hii una shauku ya dunia kutambua uwezo wako wa kuchakata mambo kwa falsafa na hoja za kipekee.

Nikuhakikishie kuanzia sasa unaenda kuamsha uwezekano wa kutimiza ndoto zako kupitia muonekano wako.Kiasilia binadamu ana uwezo wa kufanya jambo Zaidi ya moja kwa ubora na ufasaha wa hali ya juu, kila mtu ana kipaji Zaidi ya kimoja ambacho ni karama na Baraka tangu siku anazaliwa. Ukitaka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uwe na muonekano kama wa kiongozi kuanzia mavazi,hekima,busara na maarifa pia lazima ujichanganye na watu wanaopenda mambo ya uongozi na ujifunze Zaidi kutoka kwa viongozi.

Mbinu tano zinazotumika kufikia kanuni ya muonekano hutengeneza uwezekano kama ifutavyo:

1. Mtangulize Mungu
Kubali kataa ndugu msomaji kiuhalisia muhimili wa maisha ya mwanadamu umebebwa na Mungu mwenyezi, pasipo na Mungu katika kila tendo ama hatua yoyote ya mwanadamu mafanikio huwa ni hafifu. Vilevile ukaribu kati ya Mungu na mwanadamu huleta tulizo na amani ya moyo, uimara kwenye kukata tamaa na mwanzo mpya mzuri penye kuhisi umefikia mwisho wa hatima yako. Imani yako ndiyo inamaanisha msimamo wako wa maisha, zingatia hili.

2. Jenga nguvu kubwa ya Imani yako.
Imani ya kuiambia nafsi yako kwamba una uwezo na hakuna kipingamizi kufikia malengo yako, hii huamsha nguvu ya uwezekano uliopo ndani yako kwa kupitia mfumo wa akili kwa kutengeneza njia za kuhakikisha unafikia ndoto zako. Nadhani ushawahi kusikia kuhusu “placebo effect” hii sio dawa halisi kwa mgojwa ila anachomwa mgonjwa akiamini kwamba ni dawa na itamtibu, hii hutimia na mgonjwa kupona kutokana na nguvu kubwa ya Imani aliyojijengea ndani yake. kuwa na mawazo chanya, wape udhuru chanya watu wengine na futilia mbali mawazo hasi, ndipo utakuwa mtu unayejitamani kufikia makuu katika hii dunia. Kama muda huu unavyoamini hii Makala itakusaidia kubadili maisha yako ndiyo itakavyokuwa hivyo katika uhalisia na utatimiza ndoto zako.

3. Tengeneza nguvu ya maono.
Panga malengo yako sasa kulingana na mapendekezo na matakwa yako unayohitajia kisha vuta taswira kubwa akilini mwako juu ya mafanikio utakayoyapata baada ya kukamilisha ndoto zako, hii itakutia hamasa na kuamsha akili yako kuchakata njia sahihi za kimafanikio. Maono ndiyo yanawatofautisha viongozi na wafuasi, kama ni mtu wa kutengeneza maono ili kuona mchakato akilini na kuona njia ya mafankio kabla ya utendaji hakika wewe ni mtu wa kipekee mwenye uwezo mkubwa sana ndani yako.

4. Jenga nidhamu binafsi.
Jiheshimu pamoja na kuheshimu mikakati uliyojiwekea kufikia ndoto zako kupitia vitu hivi vitatu;

Muda – jifunze kusema “HAPANA” kwenye matukio yote yanayopoteza muda wako na kuzuia ndoto zako, badala yake wekeza muda mwingi kusoma Makala, ongeza ujuzi, fikiri Zaidi na kujipanga kupokea mafanikio.
Pesa – nidhamu bora ya pesa huchochea kutenegeneza uwezekano wa ndoto zako kupitia kuwekeza katika kuvaa, taaluma, ujuzi na watu wa muhimu kwako. Nakushauri ndugu msomaji wekeza pesa zako katika maeneo yanayoendana na ndoto zako kwa kuinua uwezo wako.
Marafiki – kanuni hii ya muonekano hutengeneza uwezekano hubebwa na kundi la marafiki ambao ni rafiki salama kwa ndoto zako. Kama unataka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uifuate kanuni, tafuta marafiki wanaopenda uongozi au ni viongozi tayari maana kuna msemo unasema “ukikaa karibu na waridi, pia utanukia waridi”

5.Jikubali, Anza sasa.
Jikubali kwamba una uwezo mkubwa na acha kutamani mafanikio ila anza sasa kuanzia muda huu chukua hatua kufikia malengo yako, hii itatimia kwa kuzingatia yafuatayo;

Fursa – tafuta nafasi iliyosahihi inayoendana na ndoto zako na onyesha uwezo wako
Jina – ukishapata nafasi anza kuonyesha uwezo wako binafsi kwa kujituma, kujitahidi kufanya kazi kwa ubora ili utambulike jina lako na umuhimu wako katika hiyo fursa unayoitumikia, jenga uaminifu kwa kutimiza majukumu yako kwa muda muwafaka. kwa maana fupi ni tafuta utofauti katika utendaji kazi ili ujenge jina lako.
Pesa – watu wakikuamini na kuona umuhimu wako juu ya utendaji kazi mzuri ndipo jina lako litakuwa kubwa na pesa zitakuja zenyewe.

“Ongeza maarifa, Chochea muonekano kutengeneza uwezekano wa ndoto zako sasa”
 
Upvote 766
Mfano mzuri ni humu JF kama mdau akiwa anapost Uzi zisizo na maadili au kutumia lugha za kihuni, basi ni lazima MTU huyu jamii ya JF itamfikiria ni muhuni.
Hapa tunaona umuhimu wa kutengeneza muonekano wako ambao ni kitambulisho kwa jamii isiyokufaham na hata inayokufaham pia
 
Jinsi ya kuipigia kura hii makala ni kama ifuatavyo.
Fungua JF kwa browser ya google kisha login. Fungua hii makala shuka mpaka mwisho wa makala utaona neno VOTES likiwa na idadi ya kura. Hapo Hapo kwa upande wa kushoto bonyeza Mara moja kwenye alama hii ^ utaona kura zinaongezeka.
Ahsante Hapo tayri umeshapiga kura
 
Ahsante sana Mkuu nimatumaini yangu umejifunza mengi na kupata Mwangaza mpya wa kuzifuata na kukamilisha ndoto zako bila kujali ugumu au kukatishwa tamaa.
Hakika unaweza, PAMBANA Hapo ulipo bado, endelea kuunganisha ujuzi,uzoefu na talanta zako utafanikiwa sana zaidi ya sana.
Utanikumbuka
Mkuu nashukuru sana kwa maneno yako maana nimekuwa kwenye changamoto nyingi hasa baada ya kuanguka kibiashara mkuu ..kwa kweli Niko kwenye hali ya kukata tamaa kabisa kwa umri wangu huu wa 27 nimefanya biashara sita na zote zimeanguka kiasi kwamba moyo umekosa nguvu ya kusonga mbele lakini kwa iman nitainuka tena kuanza umpya.
Wanasema "Inuka ule nyama tele"
Nashukuru sana Mr Excel..
 
Umekuwa shujaa nikupongeze kwa umri wako kufanya biashara 6 ni jambo kubwa sana.
Nakusihi usikate tamaa hapo ulipo umepitia mafunzo ya ukomavu kibiashara unajua chamgamoto zote za biashara hivyo anza kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya kila siku ukiamka inenee nafsi yako mazuri kwamba utafanikiwa hakika mdomo unaumba 100%.
Itafute nafsi yako ya kweli na talanta zako kwa vile vitu ambavyo uliwahi kufanya au unavifanya watu wakakunenea kwamba "ukifanya jambo hili unafanya vizuri sana" hakika hapo shikilia kuna kheri, pia usiogope kufanya jambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja kuwa Multi-tasker.
Tafuta watu, wekeza kwenye kujifunza biashara kwa waliofanikiwa, vutia watu unaowataka waje upande wako kwa kuwa na hekima, jishushe kwao ili upate unachotaka "mtaka cha uvunguni sharti ainame".
Pia panga mipango yako ya mafanikio kwa siri, tekeleza kimya kimya usiwe mtu wa matangazo kwa watu na sio mtendaji.
Takwimu zinaonyesha kwamba wanaozungumza sana kuhusu ndoto zao zijazo na mipango yao mizuri ya baadae huwa inafeli.
Sema na nafsi yako, waeleze mipango yako familia yako au watu unaowaamini watakusaidia..
Amini unaweza
 
Maisha ya mwanadamu kiujumla yanatengenezwa na muonekano wa kila siku anaojitahidi kuutengeneza katika mazingira yanayomzunguka. Je, muonekano ni nini? Uwezekano ni nini? Kanuni hii ni siri kubwa iliyo sheheni vipengele muhimu sana vyenye siri ya mafanikio.

Muonekano ni taswira ya nje jinsi binadamu anavyojihusisha na shughuli za kila siku ila uwezekano ni nguvu ya asili ambayo ipo ndani ya mwili wa binadamu ikiiamshwa inafanya mambo makubwa sana katika jamii.

Kila binadamu hapa duniani ana tamani kufikia malengo yake makubwa ya kimafanikio aliyojiwekea, wengine wanatamani kuwa viongozi wakubwa, wafanya biashara, wanasiasa wakubwa na wengine wanatamani dunia iwafahamu kwa uwezo mkubwa na talanta walizo nazo, hasa wewe ambaye unasoma Makala hii una shauku ya dunia kutambua uwezo wako wa kuchakata mambo kwa falsafa na hoja za kipekee.

Nikuhakikishie kuanzia sasa unaenda kuamsha uwezekano wa kutimiza ndoto zako kupitia muonekano wako.Kiasilia binadamu ana uwezo wa kufanya jambo Zaidi ya moja kwa ubora na ufasaha wa hali ya juu, kila mtu ana kipaji Zaidi ya kimoja ambacho ni karama na Baraka tangu siku anazaliwa. Ukitaka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uwe na muonekano kama wa kiongozi kuanzia mavazi,hekima,busara na maarifa pia lazima ujichanganye na watu wanaopenda mambo ya uongozi na ujifunze Zaidi kutoka kwa viongozi.

Mbinu tano zinazotumika kufikia kanuni ya muonekano hutengeneza uwezekano kama ifutavyo:

1. Mtangulize Mungu
Kubali kataa ndugu msomaji kiuhalisia muhimili wa maisha ya mwanadamu umebebwa na Mungu mwenyezi, pasipo na Mungu katika kila tendo ama hatua yoyote ya mwanadamu mafanikio huwa ni hafifu. Vilevile ukaribu kati ya Mungu na mwanadamu huleta tulizo na amani ya moyo, uimara kwenye kukata tamaa na mwanzo mpya mzuri penye kuhisi umefikia mwisho wa hatima yako. Imani yako ndiyo inamaanisha msimamo wako wa maisha, zingatia hili.

2. Jenga nguvu kubwa ya Imani yako.
Imani ya kuiambia nafsi yako kwamba una uwezo na hakuna kipingamizi kufikia malengo yako, hii huamsha nguvu ya uwezekano uliopo ndani yako kwa kupitia mfumo wa akili kwa kutengeneza njia za kuhakikisha unafikia ndoto zako. Nadhani ushawahi kusikia kuhusu “placebo effect” hii sio dawa halisi kwa mgojwa ila anachomwa mgonjwa akiamini kwamba ni dawa na itamtibu, hii hutimia na mgonjwa kupona kutokana na nguvu kubwa ya Imani aliyojijengea ndani yake. kuwa na mawazo chanya, wape udhuru chanya watu wengine na futilia mbali mawazo hasi, ndipo utakuwa mtu unayejitamani kufikia makuu katika hii dunia. Kama muda huu unavyoamini hii Makala itakusaidia kubadili maisha yako ndiyo itakavyokuwa hivyo katika uhalisia na utatimiza ndoto zako.

3. Tengeneza nguvu ya maono.
Panga malengo yako sasa kulingana na mapendekezo na matakwa yako unayohitajia kisha vuta taswira kubwa akilini mwako juu ya mafanikio utakayoyapata baada ya kukamilisha ndoto zako, hii itakutia hamasa na kuamsha akili yako kuchakata njia sahihi za kimafanikio. Maono ndiyo yanawatofautisha viongozi na wafuasi, kama ni mtu wa kutengeneza maono ili kuona mchakato akilini na kuona njia ya mafankio kabla ya utendaji hakika wewe ni mtu wa kipekee mwenye uwezo mkubwa sana ndani yako.

4. Jenga nidhamu binafsi.
Jiheshimu pamoja na kuheshimu mikakati uliyojiwekea kufikia ndoto zako kupitia vitu hivi vitatu;

Muda – jifunze kusema “HAPANA” kwenye matukio yote yanayopoteza muda wako na kuzuia ndoto zako, badala yake wekeza muda mwingi kusoma Makala, ongeza ujuzi, fikiri Zaidi na kujipanga kupokea mafanikio.
Pesa – nidhamu bora ya pesa huchochea kutenegeneza uwezekano wa ndoto zako kupitia kuwekeza katika kuvaa, taaluma, ujuzi na watu wa muhimu kwako. Nakushauri ndugu msomaji wekeza pesa zako katika maeneo yanayoendana na ndoto zako kwa kuinua uwezo wako.
Marafiki – kanuni hii ya muonekano hutengeneza uwezekano hubebwa na kundi la marafiki ambao ni rafiki salama kwa ndoto zako. Kama unataka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uifuate kanuni, tafuta marafiki wanaopenda uongozi au ni viongozi tayari maana kuna msemo unasema “ukikaa karibu na waridi, pia utanukia waridi”

5.Jikubali, Anza sasa.
Jikubali kwamba una uwezo mkubwa na acha kutamani mafanikio ila anza sasa kuanzia muda huu chukua hatua kufikia malengo yako, hii itatimia kwa kuzingatia yafuatayo;

Fursa – tafuta nafasi iliyosahihi inayoendana na ndoto zako na onyesha uwezo wako
Jina – ukishapata nafasi anza kuonyesha uwezo wako binafsi kwa kujituma, kujitahidi kufanya kazi kwa ubora ili utambulike jina lako na umuhimu wako katika hiyo fursa unayoitumikia, jenga uaminifu kwa kutimiza majukumu yako kwa muda muwafaka. kwa maana fupi ni tafuta utofauti katika utendaji kazi ili ujenge jina lako.
Pesa – watu wakikuamini na kuona umuhimu wako juu ya utendaji kazi mzuri ndipo jina lako litakuwa kubwa na pesa zitakuja zenyewe.

“Ongeza maarifa, Chochea muonekano kutengeneza uwezekano wa ndoto zako sasa”
Safi sana mkuu yote uliyo yaeleza ameyaeleza bwana Napoleon Hill kwenye kitabu chake cha Think and Grow Rich ,hayo ndoo matunda ya kusoma vitabu ukipata nafasi unatema madini.Ubarikiwe sana.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Nitakifatilia hiki Kitabu Mkuu maana sikifaham kabisa.
Hili chapisho nimeliandika binafsi kwa mkono wangu, lengo kuu liwe chachu ya kuwa badilisha watanzania na dunia kwa ujumla tuweze kutimiza ndoto zetu.

Ahsante Mkuu tupo pamoja
 
Ujitoe kisawasawa kutimiza mikakati
Yakuzingatia ili uwe na furaha maishano mwako.
1.Fanya kitu unachokipenda
2.Usiwachukie waliokuzidi kimafanikio ila jifunze kutoka kwao.
3.Saidia wengine uliowazidi
4.Onyesha vitendo zaidi usiwe na maneno mengi.
5.Kuwa mvumilivu kwa kila hali

izingatia haya utafurahia kanuni ya muonekano hutengeneza uwezekano kwa kuwa na furaha.mida wote.
 
Kulingana na makala Yako kiongozi umeongelea kuhusu marafiki hivyo basi kwetu sisi unatushauri vip katika kuchagua marafiki wa kua nao?
Nakumbuka mwaka wa kwanza chuoni niliweza kuishi bila rafiki wa kudumu mwaka mzima mpaka darasa langu wakaanza kuniita mbinafsi, lakini sikujali. Kichwani nilijenga malengo yangu kuifuata kanuni hii kupitia kipengele cha nidhamu binafsi katika marafiki nilihakikisha nachagua marafiki wanaoendana na ndoto zangu.
Hivyo nawashauri uchague rafiki kulingana na ndoto zako watakuwa msaada kwako. Pia kuchagua mchumba chagua anayekupenda na anathamini malengo yako kimkakati au mchakato kuelekewa kufanikiwa kimaisha
 
Back
Top Bottom