SoC01 Muonekano hutengeneza uwezekano

SoC01 Muonekano hutengeneza uwezekano

Stories of Change - 2021 Competition

Mr Excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2021
Posts
526
Reaction score
1,675
Maisha ya mwanadamu kiujumla yanatengenezwa na muonekano wa kila siku anaojitahidi kuutengeneza katika mazingira yanayomzunguka. Je, muonekano ni nini? Uwezekano ni nini? Kanuni hii ni siri kubwa iliyo sheheni vipengele muhimu sana vyenye siri ya mafanikio.

Muonekano ni taswira ya nje jinsi binadamu anavyojihusisha na shughuli za kila siku ila uwezekano ni nguvu ya asili ambayo ipo ndani ya mwili wa binadamu ikiiamshwa inafanya mambo makubwa sana katika jamii.

Kila binadamu hapa duniani ana tamani kufikia malengo yake makubwa ya kimafanikio aliyojiwekea, wengine wanatamani kuwa viongozi wakubwa, wafanya biashara, wanasiasa wakubwa na wengine wanatamani dunia iwafahamu kwa uwezo mkubwa na talanta walizo nazo, hasa wewe ambaye unasoma Makala hii una shauku ya dunia kutambua uwezo wako wa kuchakata mambo kwa falsafa na hoja za kipekee.

Nikuhakikishie kuanzia sasa unaenda kuamsha uwezekano wa kutimiza ndoto zako kupitia muonekano wako.Kiasilia binadamu ana uwezo wa kufanya jambo Zaidi ya moja kwa ubora na ufasaha wa hali ya juu, kila mtu ana kipaji Zaidi ya kimoja ambacho ni karama na Baraka tangu siku anazaliwa. Ukitaka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uwe na muonekano kama wa kiongozi kuanzia mavazi,hekima,busara na maarifa pia lazima ujichanganye na watu wanaopenda mambo ya uongozi na ujifunze Zaidi kutoka kwa viongozi.

Mbinu tano zinazotumika kufikia kanuni ya muonekano hutengeneza uwezekano kama ifutavyo:

1. Mtangulize Mungu
Kubali kataa ndugu msomaji kiuhalisia muhimili wa maisha ya mwanadamu umebebwa na Mungu mwenyezi, pasipo na Mungu katika kila tendo ama hatua yoyote ya mwanadamu mafanikio huwa ni hafifu. Vilevile ukaribu kati ya Mungu na mwanadamu huleta tulizo na amani ya moyo, uimara kwenye kukata tamaa na mwanzo mpya mzuri penye kuhisi umefikia mwisho wa hatima yako. Imani yako ndiyo inamaanisha msimamo wako wa maisha, zingatia hili.

2. Jenga nguvu kubwa ya Imani yako.
Imani ya kuiambia nafsi yako kwamba una uwezo na hakuna kipingamizi kufikia malengo yako, hii huamsha nguvu ya uwezekano uliopo ndani yako kwa kupitia mfumo wa akili kwa kutengeneza njia za kuhakikisha unafikia ndoto zako. Nadhani ushawahi kusikia kuhusu “placebo effect” hii sio dawa halisi kwa mgojwa ila anachomwa mgonjwa akiamini kwamba ni dawa na itamtibu, hii hutimia na mgonjwa kupona kutokana na nguvu kubwa ya Imani aliyojijengea ndani yake. kuwa na mawazo chanya, wape udhuru chanya watu wengine na futilia mbali mawazo hasi, ndipo utakuwa mtu unayejitamani kufikia makuu katika hii dunia. Kama muda huu unavyoamini hii Makala itakusaidia kubadili maisha yako ndiyo itakavyokuwa hivyo katika uhalisia na utatimiza ndoto zako.

3. Tengeneza nguvu ya maono.
Panga malengo yako sasa kulingana na mapendekezo na matakwa yako unayohitajia kisha vuta taswira kubwa akilini mwako juu ya mafanikio utakayoyapata baada ya kukamilisha ndoto zako, hii itakutia hamasa na kuamsha akili yako kuchakata njia sahihi za kimafanikio. Maono ndiyo yanawatofautisha viongozi na wafuasi, kama ni mtu wa kutengeneza maono ili kuona mchakato akilini na kuona njia ya mafankio kabla ya utendaji hakika wewe ni mtu wa kipekee mwenye uwezo mkubwa sana ndani yako.

4. Jenga nidhamu binafsi.
Jiheshimu pamoja na kuheshimu mikakati uliyojiwekea kufikia ndoto zako kupitia vitu hivi vitatu;

Muda – jifunze kusema “HAPANA” kwenye matukio yote yanayopoteza muda wako na kuzuia ndoto zako, badala yake wekeza muda mwingi kusoma Makala, ongeza ujuzi, fikiri Zaidi na kujipanga kupokea mafanikio.
Pesa – nidhamu bora ya pesa huchochea kutenegeneza uwezekano wa ndoto zako kupitia kuwekeza katika kuvaa, taaluma, ujuzi na watu wa muhimu kwako. Nakushauri ndugu msomaji wekeza pesa zako katika maeneo yanayoendana na ndoto zako kwa kuinua uwezo wako.
Marafiki – kanuni hii ya muonekano hutengeneza uwezekano hubebwa na kundi la marafiki ambao ni rafiki salama kwa ndoto zako. Kama unataka kuwa kiongozi mkubwa ni lazima uifuate kanuni, tafuta marafiki wanaopenda uongozi au ni viongozi tayari maana kuna msemo unasema “ukikaa karibu na waridi, pia utanukia waridi”

5.Jikubali, Anza sasa.
Jikubali kwamba una uwezo mkubwa na acha kutamani mafanikio ila anza sasa kuanzia muda huu chukua hatua kufikia malengo yako, hii itatimia kwa kuzingatia yafuatayo;

Fursa – tafuta nafasi iliyosahihi inayoendana na ndoto zako na onyesha uwezo wako
Jina – ukishapata nafasi anza kuonyesha uwezo wako binafsi kwa kujituma, kujitahidi kufanya kazi kwa ubora ili utambulike jina lako na umuhimu wako katika hiyo fursa unayoitumikia, jenga uaminifu kwa kutimiza majukumu yako kwa muda muwafaka. kwa maana fupi ni tafuta utofauti katika utendaji kazi ili ujenge jina lako.
Pesa – watu wakikuamini na kuona umuhimu wako juu ya utendaji kazi mzuri ndipo jina lako litakuwa kubwa na pesa zitakuja zenyewe.

“Ongeza maarifa, Chochea muonekano kutengeneza uwezekano wa ndoto zako sasa”
 
Upvote 766
Hahahaha sawa ngoja nikupe tofauti zao.
Genius- huyu huwa ana ile elimu tu ila maarifa yake ni madogo, anaweza akawa anakariri na kuongoza katika hiyo elimu. Uwezo wa kuleta tafakuri na kujiongeza kimazingira, pia kujiuliza maswali binafsi na kitaftia ufumbuzi huwa hana.

Intelligent- huyu huwa ana elimu na ana maarifa mengi zaidi ya ile elimu yake. Huwa anaelewa, anajiuliza maswali na anayatafutia ufumbuzi binafsi yake. Ukimleta katika mazingira yoyote anauwezo wa kuyamudu iasavyo na kujiongeza kiakili.
 
Madini sana kiongozi
 
Samahani kiongozi Kulingana na makala Yako umeongelea kutokukata tamaa Je, mtu afanye vipi kurudisha matumaini pindi anapokata tamaa?
 
Samahani kiongozi Kulingana na makala Yako umeongelea kutokukata tamaa Je, mtu afanye vipi kurudisha matumaini pindi anapokata tamaa?
Katika kanuni hii imebeba mambo muhimu5 ambayo huwa yanabebwa na ndoto/malengo ya mtu binafsi.
Ili mtu usikate tamaa hakikisha unatumia kanuni hii katika mchakato wako wa kimafanikio.
Kama ulisoma vizuri makala hii.
Katika kipengele cha kumtanguliza Mungu nimeelezea jinsi inavyoleta utulivu wa moyo na inavyorudisha matumaini na mwanzo mpya kwa walioata tamaa.
Hivyo tekeleza points zote 5 ndipo hautakata tamaa katika malengo yako kila kitu utaona chepesi kwako.

Ahsante
 
Asante sana nimekuelewa mkuu
 
Nashukhuru sana Kwa majibu yako
 
Na kupitia hii kanuni unawashauri vipi Vijana ambao ndo kundi kubwa ulilolilenga kupata elimu hii?
 
Back
Top Bottom