Muonekano mpya wa Azam Complex, Uwanja wa klabu ya Azam

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Azam FC wameachia picha za muonekano mpya wa mabenchi ya wachezaji wa akiba, baada ya kufanyiwa maboresho.

Azam FC wameachia picha hizo saa chache kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Uwanjani hapo.

Mara ya mwisho Azam FC ilipocheza Azam Complex dhidi ya Fountain Gate, mabenchi yalikuwa katika muonekano wa kawaida.

Ujumbe ulioandikwa katika kurasa za mitandao ya kijamii za Azam FC ambao umeambatana na picha hizo unasomeka: Azam Complex Is Ready. Uwanja wetu wa Azam Complex upo tayari kwa mechi ya mwisho ya kufunga mwaka 2024, wakati tutakapoivaa JKT Tanzania leo Ijumaa saa 1.00 usiku.
 
Bakhresa na biashara zake ni mfano mzuri kutukumbusha kuwa chochote unachotaka kufanya anza na unapoweza, utaboresha na kubanuka baadae.

Wengi tunataka tuanze biashara kwa ukubwa ule ule wa mawazo yetu jambo ambalo ni gumu na mara nyingi haliwezekani.
 
Money talk!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…