Muonekano wa Stendi ya Mabasi Kondoa (Dodoma) unatia aibu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Licha ya mamlaka za Serikali kuendelea kutoza ushuru kutoka kwenye mabasi ya abiri yanayopita kwenye Stendi Kuu ya Wilaya ya Kondoa.

Mkoani Dodoma bado hali ya mazingira si mazuri.

Mabasi yanavyopita wakati wa kiangazi vumbi linalotimka hapo si la Nchi hii, wakati wa mvua napo matope ndio usiseme.

Serikali ya Kondoa na ya Dodoma kwa jumla zinatakiwa kufanya kitu, huo ushuru wanaokusanya wanaupeleka wapi au ndio wenye matumbo yao wanakula kama kawaida yao?

Your browser is not able to display this video.



Muonekano wa Stendi ya Kondoa upande wa nyuma

Muonekano wa Stendi ya Kondoa upande wa nje

Wakati wa kiangazi mazingira ya vumbi


 
Si iko katika hatua ya Ujenzi au hamuongei na Mbunge na madiwani wenu
 
Machame Inv kateka soko la Dodoma-Kondoa-Kiteto-Kongwa. Wenyeji mmezubaa
 
Hao wapo kupiga hela Tu Ila nashangaa wenye nabas na magar kwann wasigome kupita ndo stand itengenezwe

Nchi hii watu n waoga Sana
Na uspopita hapo stand n fain
 
Machame anapiga pesa sana hizi kanda hakuna wa kumkaribia hata.

Huwezi tembea huku bila kumpa hela machame
Ni kweli mkuu. Struggle, Kamwana na MJ wamebaki kutazama tu wapo hoi- nyag'anyang'a. Mtei na mwenzake Kimotco walishajifiaga zamani hizo.
Kuna huyu jamaa anajiita Roots (Kiteto - Arusha via Babati) sijui kama atatoboa.
 
Machame anapiga pesa sana hizi kanda hakuna wa kumkaribia hata.

Huwezi tembea huku bila kumpa hela machame
My favorite transport Kwa njia ya Arusha ni machame kwanza
 
Machame ni kama mwenyeji tu japo ni mchaga ila maisha yake yote amefanyia kondoa na hata kuzaliwa kazaliwa Kondoa so ni kama mwenyeji tu
 
Jamaa anajitahidi asipoingia kwenye ligi za kipumbavu za barabarani ataendelea kuteka soko kwa miaka mingi
Machame ni kama mwenyeji tu japo ni mchaga ila maisha yake yote amefanyia kondoa na hata kuzaliwa kazaliwa Kondoa so ni kama mwenyeji tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…