Muongozo kamili: Kufanya biashara ya mbao za mpaina kutoka Njombe kwenda mikoa mingine kama Dar es Salaam,Dodoma nk

Muongozo kamili: Kufanya biashara ya mbao za mpaina kutoka Njombe kwenda mikoa mingine kama Dar es Salaam,Dodoma nk

Muuzaji Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2022
Posts
893
Reaction score
2,001
NYARAKA MUHIMU ZINAHITAJIKA ILI MBAO ZISAFIRISHWE BILA USUMBUFU KWENYE VITUO VYA UKAGUZI NJIANI
‎
‎ 1️⃣ Certificates (Vyeti)
‎
‎✓• Taxpayer Identification Number certificate (TIN) – Cheti cha mlipa kodi kutoka TRA.
‎✓• Business License / Registration Certificate – Leseni ya biashara.
‎
‎MUHIMU: TIN na Leseni ya biashara vitatumika kama mteja hana kibali cha kufanya biashara ya mbao na anataka kukata cha kwake mwenyewe na sio cha kukodi
‎
‎✓• Certificate of Registration of Forest Produce Dealer/Trader – Kibali cha kufanya biashara ya mbao kutoka Maliasili.
‎
‎2️⃣ Vibali
‎
‎✓• Transit Pass (T.P.) – Kibali cha kusafirisha mbao kutoka eneo la mauzo hadi mteja.
‎
‎3️⃣ Ushuru / Charges zinazohitajika
‎
‎✓• Ushuru wa Halmashauri – Kulingana na eneo uliponunua mbao.
‎✓• Forest Road Services (Ushuru wa Miundombinu) – Ada ya barabara za msitu.
‎
‎4️⃣ Risiti za Muhimu
‎
‎✓• Risiti ya manunuzi ya mbao – au risiti mbadala inayothibitisha ununuzi.
‎✓• Risiti ya gari – inayosafirisha mbao au mbadala wake.
‎
‎MUHIMU 01: “Ni lazima nyaraka zote zinazohitajika ziwepo kabla ya kuanza usafirishaji ili kuepuka usumbufu njiani.”
‎
‎MUHIMU 02: TIN na Leseni ya biashara vitatumika kama mteja hana kibali cha kufanya biashara ya mbao na anataka kukata cha kwake mwenyewe na sio cha kukodi.

‎GHARAMA ZA MUHIMU AMBAZO MNUNUZI ANATAKIWA KUANDAA BAADA YA KUWEKA ODA YA MBAO
‎
‎ GHARAMA KUU
‎✓•Manunuzi-Gharama ya manunuzi hutegemea size,idadi na bei ya mbao unazonunua.
‎✓•Usafirishaji-Gharama ya usafirishaji hutegemea umbali na aina ya gari; inatakiwa kulipwa kulingana na makubaliano.
‎✓•Upakiaji-150,000/=
‎✓•Ushuru/Halmashauri Ya:
‎ -Mji wa Njombe~100/=
‎ -Wilaya ya Makete~100/=
‎ -Wilaya ya Njombe~100/=
‎ -Wilaya ya Ludewa~100/=
‎ -Mji wa Makambako~100/=
‎ -Wilaya ya Wanging'ombe~100/
‎✓•Transit Pass (TP)-15,000/=
‎✓•Forest Road Services-20,000/=
‎✓•Kuhakiki Uzito Mizani-25,000/=
‎✓•Barua Ya Serikali Ya Mtaa-10,000/=
‎✓•Risiti Ya Manunuzi Ya TRA-300,000/=
‎
‎ GHARAMA ZA ZIADA
‎✓•Kukodi Kibali cha Kufanya biashara ya mbao- 100,000/= (Kama Mnunuzi hana hiki kibali basi ataandaa tsh 100,000/= kwaajili Ya Kukodi Kibali hiki).
‎
‎ AU
‎✓•Kukata kibali chako mwenyewe Maliasili- 200,000/= (Ukikata kibali hiki utakitumia kwa mda wa mwaka mmoja ndo unakata kingine)

VIPIMO VYA MBAO NAZOUZA
‎✓• 2×2 Futi 12
‎✓• 2×3 Futi 12
‎✓•2×4 Futi 12
‎✓•2×6 Futi 12
‎✓•2×8 Futi 12
‎✓•1×4 Futi 12
‎✓•1×6 Futi 12
‎✓•1×8 Futi 12
‎✓•1×10 Futi 12
‎--------------------------------------------------------------
‎
‎ SIFA ZA MBAO NAZOUZA
‎✓•Aina ya mti: Pines (Msonobari)
‎✓•Uainishaji: Softwood (Mbao Laini)
‎✓•Matibabu: Untreated (Hazijachakatwa kwa dawa/kemikali)
‎✓•Rangi: White (Nyeupe)
‎-------------------------------------------------------------
‎
‎ UBORA WA MBAO NAZOUZA
‎✓•Mbao zimekauka vizuri sana
‎✓•Mbao zimenyooka vizuri sana
‎✓•Mbao hazina vidonda wala nyufa
‎✓•Mbao zimekatwa kwa vipimo sahihi
‎✓•Mbao hazijaoza wala kubadilika rangi
‎✓•Mbao hazipindi/kuvunjika kwa urahisi
‎✓•Nyepesi kwa usafirishaji lakini imara kwa matumizi.
‎--------------------------------------------------------------
‎
‎MATUMIZI YA MBAO NAZOUZA
‎✓ Kujengea paa na madari ya nyumba.
‎✓ Kutengeneza milango, madirisha, na samani za ndani.
‎✓ Kutengeneza pallets za kuhifadhia mizigo.
‎✓ Kutumika kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi.
‎✓ Kutumika kwa mapambo au paneling ya ndani.
‎✓ Kutengeneza bidhaa za kibiashara/kama maboksi na shelves za biashara.
‎-------------------------------------------------------------
‎
‎MAENEO NAYOTOA MBAO NAZOUZA
‎Mbao nazouza zinatoka kwa wazalishaji wa vijiji na vitongoji za halmashauri sita za Mkoa wa Njombe ambazo ni:
‎
‎•Halmashauri ya mji wa Njombe
‎•Halmashauri ya mji wa Makambako
‎•Halmashauri ya wilaya ya Njombe
‎•Halmashauri ya wilaya ya ludewa
‎•Halmashauri ya wilaya ya makete
‎•Halmashauri ya wilaya ya wanging'ombe
‎--------------------------------------------------------------
‎
‎BEI ZA SHAMBA MBAO NAZOUZA
‎✓•2×2 Futi 12~ Tsh 800 - 1,500
‎✓•2×3 Futi 12~ Tsh 1,800 - 2,500
‎✓•2×4 Futi 12~ Tsh 2,800 - 3,500
‎✓•2×6 Futi 12~ Tsh 3,800 - 5,500
‎✓•1×4 Futi 12~ Tsh 800 - 1,500
‎✓•1×6 Futi 12~ Tsh 2,500 - 3,200
‎✓•1×8 Futi 12~ Tsh 4,500 - 6,200
‎✓•1×10 Futi 12~ Tsh 8,500 - 12,000
‎
‎MUHIMU: Bei za mbao hubadilika kutokana na sababu zifuatazo:
‎
‎✓• Msimu – Upatikanaji hutofautiana kulingana na mvua au kiangazi.
‎✓• Umbali wa usafirishaji – Kadri eneo linavyokuwa jirani na Mji bei ya mbao huongezeka.
‎✓• Ubora wa mbao – Mbao zilizonyooka, zikakauka vizuri na zisizo na vidonda huwa na bei ya juu.
‎✓• Hali ya soko – Wakati mahitaji ni makubwa bei hupanda.
‎✓• Uzalishaji - Uzalishaji ukiwa mkubwa bei huwa chini ukilinganisha na uzalishaji ukiwa mdogo.
‎--------------------------------------------------------------
‎
‎ UPATIKANAJI WA MBAO NAZOUZA
‎✓•Mbao nazouza hazipo katika eneo moja hivyo eneo la kupakilia hutokana na makubaliano ya mimi na mteja kutokana na size,idadi,bei pamoja na gharama za usafirishaji.
‎
‎✓•Mbao nazouza zinapatikana muda wote Kwa oda ya kuanzia semi moja na kuendelea kulingana na uhitaji wa mteja.
‎-------------------------------------------------------------
‎
UTARATIBU WA KUWEKA ODA YA MBAO NA USAFIRISHAJI HADI ENEO LA MTEJA.
‎
‎NAMNA YA KUWEKA ODA YA MBAO KWA WATEJA WANAOTAKA KUNUNUA MOJA KWA MOJA KWA BEI ZA SHAMBA KUANZIA SEMI MOJA (GARI) NA KUENDELEA.
‎
‎1️⃣ Taarifa za Msingi za Oda
‎
‎Mteja anatakiwa kutoa taarifa zifuatazo:
‎
‎•Size za mbao unazohitaji
‎
‎•Idadi ya mbao kwa kila size
‎
‎•Eneo la kusafirishia mbao
‎
‎- Mkoa
‎
‎- Wilaya
‎
‎- Kata
‎
‎ -Mtaa/Kitongoji
‎
‎•Gari la kusafirishia mzigo
‎
‎-Unatumia gari lako mwenyewe?
‎
‎-Unatafuta gari ya kukodi mwenyewe?
‎
‎-Unataka nikutafutie gari ya kukodi?
‎
‎•Nyaraka za msingi kwa usafirishaji
‎
‎-Unashughulikia mwenyewe?
‎
‎-Unataka nizishughulikie mimi?
‎
‎
‎2️⃣ Uandaaji wa Gharama
‎
‎Baada ya kupokea taarifa kamili ya oda yako, nitaandaa hesabu za gharama zote hadi mzigo unakufikia. Hesabu hizo nitakutumia wewe kmteja.
‎
‎
‎3️⃣ Malipo
‎
‎Mteja anatakiwa kufanya malipo kupitia njia rasmi za malipo ninazotumia.
‎
‎MUHIMU: Malipo Ya Gharama zote za msingi yanafanyika kwa asilimia 100% isipokuwa gharama za usafirishaji wa mbao inayoweza kulipwa kwa asilimia kadhaa kabla ya kusafirisha mzigo na iliyobaki inamaliziwa baada ya mzigo kupokelewa.
‎
‎
‎4️⃣ Uthibitisho & Utekelezaji
‎
‎Baada ya kuthibitisha kupokea malipo:
‎
‎•Uandaaji wa oda yako utaanza mara moja.
‎
‎•Utapokea taarifa ya kila hatua hadi mzigo wako unafika eneo lako.
‎
‎
‎KUMBUKA: Kwa wateja wanaotaka kununua mbao kwa bei za shamba moja kwa moja oda zao zinatakiwa kuanzia SEMI MOJA na kuendelea na si chini ya hapo.
‎
‎
‎NAMNA YA KUWEKA ODA YA MBAO KWA WATEJA WANAOTAKA KUNUNUA MBAO KWA BEI MPAKA ZINAFIKISHWA ENEO LAO BILA GHARAMA ZA ZIADA.
‎
‎1️⃣ Taarifa za Msingi za Oda
‎
‎Mteja anatakiwa kutoa taarifa zifuatazo:
‎
‎•Size za mbao unazohitaji
‎
‎•Idadi ya mbao kwa kila size
‎
‎•Eneo la kusafirishia mbao
‎
‎- Mkoa
‎
‎- Wilaya
‎
‎- Kata
‎
‎ -Mtaa/Kitongoji
‎
‎2️⃣ Uandaaji wa Gharama
‎
‎Baada ya kupokea taarifa kamili ya oda yako, nitaandaa hesabu za gharama zote hadi mzigo unakufikia. Hesabu hizo nitakutumia wewe kmteja.
‎
‎3️⃣ Malipo
‎
‎Mteja anatakiwa kufanya malipo kupitia njia rasmi za malipo ninazotumia.
‎
‎MUHIMU: Malipo Ya Gharama zote yanafanyika kwa asilimia 100% kabla ya mzigo kusafirishwa kuja eneo ulipo.
‎
‎4️⃣ Uthibitisho & Utekelezaji
‎
‎Baada ya kuthibitisha kupokea malipo:
‎
‎•Uandaaji wa oda yako utaanza mara moja.
‎
‎•Utapokea taarifa ya kila hatua hadi mzigo wako unafika eneo lako.
‎
‎
‎KUMBUKA: Kwa wateja wanaotaka kununua mbao kwa bei mbao zikiwa zimefikishwa mahali walipo chini ya semi moja oda zao zitaunganishwa na wateja wengine ili kujaza gari hivyo basi utekelezaji wa oda yao utategemea oda za wateja wengine wa eneo hilo.
‎-------------------------------------------------------------
‎
‎NJIA NAZOTUMIA KUPOKEA MALIPO
‎
‎1.PESA TASLIMU
‎✓ Malipo yanaweza kufanyika moja kwa moja iwapo mteja atafika mwenyewe au atatuma mwakilishi wake.
‎
‎2.BENKI
‎✓ Malipo yanaweza kufanyika kupitia akaunti yangu iliyopo benki ifuatayo:
‎
‎ •CRDB
‎Akaunti Namba: Utapewa
‎Jina La Akaunti: Utapewa
‎

WAJIBU WA MNUNUZI WA MBAO
‎✓• Kutoa taarifa sahihi za oda (size, idadi, na eneo la kupeleka).
‎✓• Kuhakikisha anatoa nyaraka muhimu zinazohitajika kusafirisha mbao endapo haitaji kushughulikiwa na mimi.
‎✓• Kufanya malipo kwa wakati ili maandalizi ya oda yaanze mara moja.
‎✓• Kushirikiana katika kupata usafiri (kama ameomba nitafute au akitafuta mwenyewe).
‎✓• Kupokea mzigo kwa wakati pindi unapoletwa katika eneo lake.
‎✓• Kuhakikisha anazingatia utaratibu na masharti ya biashara (hakuna mzigo utasafirishwa bila kupokea malipo).
‎
‎WAJIBU WANGU KAMA MUUZAJI WA MBAO
‎
‎✓• Kuhakikisha mbao zinazoagizwa zinakidhi ubora uliotangazwa (zimekauka vizuri, hazina nyufa, zinakaa zenye mnyooka mzuri).
‎✓• Kutoa hesabu kamili ya gharama zote hadi mzigo kufika kwenye eneo la mteja endapo mteja ametaka nishughulikie mimi usafirishaji wa mbao zake.
‎✓• Kusimamia utayarishaji wa oda mara tu baada ya kuthibitisha nimepokea malipo.
‎✓• Kutoa maelezo ya kila hatua ya utayarishaji na usafirishaji wa mzigo.
‎✓• Kuhakikisha mbao zinapatikana kwa muda wote kulingana na uhitaji wa mteja.
‎✓• Kutoa msaada wa ushauri pale panapohitajika kuhusu upakiaji, usafirishaji na utunzaji wa mbao.

‎“Lengo langu ni kujenga uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara unaozingatia uaminifu, uwazi, na ubora wa mbao. Nathamini kila mteja na nitashirikiana nawe kwa mafanikio endelevu.”

SIMU: 0748874928

KARIBU SANA NJOMBE

Screenshot_20250824-202654.jpg
Screenshot_20250824-202706.jpg
Screenshot_20250824-202715.jpg
 
Duh umemaliza kila kitu mkuu,hongera kwa uandishi mzuri.
Nikuulize swali, kwa makadirio semi moja inabeba mbao za 2, 4 na 6 mchanganyiko. Makadirio ya semi moja ununuzi yaweza kuwa sh ngapi, na kukodi gari kutoka huko Hadi Morogoro mjini ni sh ngapi
 
Duh umemaliza kila kitu mkuu,hongera kwa uandishi mzuri.
Nikuulize swali, kwa makadirio semi moja inabeba mbao za 2, 4 na 6 mchanganyiko. Makadirio ya semi moja ununuzi yaweza kuwa sh ngapi, na kukodi gari kutoka huko Hadi Morogoro mjini ni sh ngapi
Ili kupata hesabu kamili
•Size ya mbao unazohitaji
•Idadi ya mbao kwa kila size
•Morogoro kubwa sema zinatakiwa kushushwa wapi ili tufanye makadirio ya gharama za usafiri

Asante
 
huku lupembe mtu akichepuka kuomba maji ya kunywa tu, anapewa debe la parachichi na mbao kama fimbo ya kutembelea. kumbe kuna sehemu mnauza aisee

anyway, uandishi na ufafanuzi bora sana umemaliza kila kitu. japo sijaona mahali unapopatikana rasmi
 
huku lupembe mtu akichepuka kuomba maji ya kunywa tu, anapewa debe la parachichi na mbao kama fimbo ya kutembelea. kumbe kuna sehemu mnauza aisee

anyway, uandishi na ufafanuzi bora sana umemaliza kila kitu. japo sijaona mahali unapopatikana rasmi
Njombe Mjini
 
Back
Top Bottom