muongozo katika biashara

muongozo katika biashara

mgenii

Member
Joined
May 18, 2015
Posts
10
Reaction score
4
habari wana jamii forum.....mimi ni binti niliyemaliza chuo mwaka jana....na nikahitimu masomi yangu ya stashahada ya computer science na kupata matokeo mazuri tuu ya first class.....
Mpaka sasa sijabahatika kupata kazi na kuitwa katika interview...hivyo basi ningependa kujiajiri mimi mwenyewe angali bado nikiendelea kutafuta kazi...sehemu tofauti tofauti...
Mimi bado ni mgeni kabisa katika biashara hivyo basi ningependa kuomba ushauri katika kupata muongozo huo.
Nimefanikiwa kupata mtoto na mpka sasa ameshakuwa mkubwa kama miezi kadhaa hivyo ningependa kuwa naongiza kipato kwa ajili ya mwanangu....
Ningependa kufanya biashara ya kuuza nguo za watoto....kwani naona hiyo ndo ntakayoimudu na inauhitaji mkubwa kwa sababu watoto kila siku wanazaliwa so mahitaji ya nguo zao huongezeka.
Bila kuwapotezea muda ..ningependa kuchukua nafasi hii kuomba ushauri juu wa muongozo wa biashara ya kuuza nguo za watoto....jinsi ya kuanza, nini kinahitajika na nahitaji kuwa na mtaji wa kiasi gani ili kufanikiwa katika biashara yangu.....na incase nilipata huo mtaji...ipi itakuwa sehemu nzuri ya kuweka duka langu......asanteni.....naombeni maoni yenu...
 
Back
Top Bottom