Muongozo katika biashara

Muongozo katika biashara

mgenii

Member
Joined
May 18, 2015
Posts
10
Reaction score
4
Habari wana jamii forum ...mimi ni binti niliyemaliza chuo mwaka jana na nikahitimu masomo yangu ya stashahada ya computer science....na kupata matokeo mazuri tuu ya first class...
Mpaka sasa sijabahatika kupata kazi na kuitwa kwenye interview.....hivyo basi ningependa kujiajiri mimi mwenyewe angali bado nikiendelea kutafuta kazi sehemu tofauti tofauti....
Mimi bado ni mgeni kabisa katika biashara hivyo basi ningependa kuomba kupata ushauri katika kupata muongozo huo....
Nimefanikiwa kupata mtoto na mpaka sasa ameshakuwa mkubwa kama miezi kadha hivyo ningependa kuwa naingiza kipato kwa ajili ya mwanangu.
Ningependa kufanya biashara ya kuuza nguo za watoto kwani naona hiyo ndio ntakayoimudu na inauhitaji mkubwa kwasababu watoto kila siku wanazaliwa so mahitaji ya nguo zao huongezeka.
Bila kuwapotezea muda...ningependa kuchukua nafasi hii kuomba ushauri juu ya muongozo wa biashara ya kuuza nguo za watoto...jinsi ya kuanza, nini kinahitajika na ninahitaji kuwa na mtaji wa kiasi gani ili kufanikiwa katika biashara yangu....na incase nikipata huo mtaji...ipi itakuwa sehemu nzuri ya kuweka duka langu....asanteni....naombeni maoni yenu....
 
kwanza hongera dada yangu kwa kuangalia upande wa pili baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira.mm nadhan kikubwa hapo nikuangalia
 
Unapatikana mkoa gani? hebu sema nikupe wazo.
 
Wakati unaendelea na kutafuta kazi
Plan ya biashara ulionayo ninnzuri sana na wala haijitaji mtaji mkubwa
Nakushauri tuliza akili anza maandalia ya kuiandaa hiyo biashara huku unaendelea kutafuta kazi,kwa pamja utafanikiwa na kutokuja kua tegemez kwa mwajiri.....waajiri wanatufanya kua watumwa
 
Wazo zuri mgeni. NI kweli kujiajiri mweyewe inapendeza. Mimi na deal na nguo za maharusi mashela na magauni ya watoto ya part . I can help somehow. Visit my Facebook page East Africa wedding dresses suppliers; au Emmanuel bridal shop; pia trendy boutique.. uache message tuwasiliane. Karibu kwenye biashara.
 
napatikana mkoa wa Dar-es-salaam..... bab-D
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri mgeni. NI kweli kujiajiri mweyewe inapendeza. Mimi na deal na nguo za maharusi mashela na magauni ya watoto ya part . I can help somehow. Visit my Facebook page East Africa wedding dresses suppliers; au Emmanuel bridal shop; pia trendy boutique.. uache message tuwasiliane. Karibu kwenye biashara.

asante sana......nitafanya hivyo as soon as possible......
 
Wakati unaendelea na kutafuta kazi
Plan ya biashara ulionayo ninnzuri sana na wala haijitaji mtaji mkubwa
Nakushauri tuliza akili anza maandalia ya kuiandaa hiyo biashara huku unaendelea kutafuta kazi,kwa pamja utafanikiwa na kutokuja kua tegemez kwa mwajiri.....waajiri wanatufanya kua watumwa

asante hujui tu ni jinsi gani umenipa moyo na nguvu ya kuendelea zaidi......shukrani..sana
...mkuu
 
Habari wana jamii forum ...mimi ni binti niliyemaliza chuo mwaka jana na nikahitimu masomo yangu ya stashahada ya computer science....na kupata matokeo mazuri tuu ya first class...
Mpaka sasa sijabahatika kupata kazi na kuitwa kwenye interview.....hivyo basi ningependa kujiajiri mimi mwenyewe angali bado nikiendelea kutafuta kazi sehemu tofauti tofauti....
Mimi bado ni mgeni kabisa katika biashara hivyo basi ningependa kuomba kupata ushauri katika kupata muongozo huo....
Nimefanikiwa kupata mtoto na mpaka sasa ameshakuwa mkubwa kama miezi kadha hivyo ningependa kuwa naingiza kipato kwa ajili ya mwanangu.
Ningependa kufanya biashara ya kuuza nguo za watoto kwani naona hiyo ndio ntakayoimudu na inauhitaji mkubwa kwasababu watoto kila siku wanazaliwa so mahitaji ya nguo zao huongezeka.
Bila kuwapotezea muda...ningependa kuchukua nafasi hii kuomba ushauri juu ya muongozo wa biashara ya kuuza nguo za watoto...jinsi ya kuanza, nini kinahitajika na ninahitaji kuwa na mtaji wa kiasi gani ili kufanikiwa katika biashara yangu....na incase nikipata huo mtaji...ipi itakuwa sehemu nzuri ya kuweka duka langu....asanteni....naombeni maoni yenu....
Amka alfajiri kabla ya jogoo kuwika
Nenda soko la mitumba
Utapata vinguo vizuri kwa watoto bei nafuu.
Kifuatacho unapiga hela mitaani.
Huhitaji kulipia fremu kwanza
Tembeza nyumba kwa nyumba.
Mtaa kwa mtaa
Ofisi kwa ofisi
hoteli kw ahoteli
kiwanda kwa kiwanda
stendi kwa stedni
n.k.
 
Nilizani uko mwanza kwan huku kuna baadhi ya masoko na minada inalipa sana kwa biashara uliyoibuni

nafikiria kupanua biashara yangu....nikipata soko zuri .....asante kwa ushauri
 
Amka alfajiri kabla ya jogoo kuwika
Nenda soko la mitumba
Utapata vinguo vizuri kwa watoto bei nafuu.
Kifuatacho unapiga hela mitaani.
Huhitaji kulipia fremu kwanza
Tembeza nyumba kwa nyumba.
Mtaa kwa mtaa
Ofisi kwa ofisi
hoteli kw ahoteli
kiwanda kwa kiwanda
stendi kwa stedni
n.k.

nashukuru sana mkuu wapi soko la mitumba linapopatikana???
 
Barabara ya Uhuru kama unatokea kwenye yale maji yaliyolaaniwa
Chukua uelekeo kama waelekea Buguruni Ulizia soko la viatu(mwanzo) au soko la nguo(kwa mbele kabla ya kufika malapa).
Bei ya nzuri ya jumla jumla ni Ulfaajirr
 
asante sana .......ubarikiwe.....
 
Dada Mgeni sijui ni kwa nini umechagua biashara ya nguo?naona unaacha fani yako, unasema umemaliza Computer science,kwa ni nini usitafute kujiajiri ktk computer science and information technology,kuna fursa nyingi ktk kaa tafakari uone,sijui una mtaji kiasi gani but unaweza kuanzisha course fupi za computer(application and software).,utatoka utasahau hata kutafuta kuajiliwa,hata hivyo mimi sisapoti sana kuajiliwa if your smart and hard working, knowing what your doing.
"HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA".
 
uko sahihi sana...lakini mtaji wa kufungua course ni mkubwa na mimi kwa kuwa bado sina kipato so nimeshindwa kufanya hivyo.....nimeamua kuanza na biashara yenye mtaji kidogo kutokana na mfuko wangu....pale ntakapokuwa na capital ya kutosha nitafanya hilo.....nina malengo makubwa sana na ningependa kuyatimiza...hivyo basi ....mtaji ndo unanilimit......nikikuwa katika biashara nitatekeleza yote yaliyo kichwani kwangu.....
 
Back
Top Bottom