Habari wakuu,
Kuna wadogo zetu wamepata matokeo yao ya kidato cha nne. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio inayotoa upepo awe nani baadae kitaaluma kwa uchaguzi anaofanya sasa japo kwa baadhi wanaweza kuwa na wigo mpana wa kuchagua tena baadae.
Hapa jukwaani kuna wengi ambao walipita huko na wana uzoefu wa matokeo tofauti, iwe ya kufaulu, wastani au kufeli na jinsi gani walijikwamua kutoka kwenye hali yaliyokuwa nao wakati husika.
Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu ama kukata tamaa kwa kupata matokeo hafifu. Kwa heshima ningependa kuwaita wanajamvi wote katika kufikisha lengo la mada hii.
Karibuni!