Tumpara Dudu
JF-Expert Member
- Nov 15, 2016
- 625
- 506
Waungwana,naomba muongozo wa kisheria. Mitaani katika jiji la Dar kuna operesheni za usafi wa mazingira nyumba kwa nyumba. Kuna msafara wa askari wengi wakishirikiana na SUMA JKT wanapita kwenye nyumba za watu wanaingia kukagua ukumbini,vyooni na imeripotiwa baadhi ya nyumba wameingia had vyumbani wakikuta hata kitanda hujatandika au wakakuta ukumbi au chooni kuchafu au wamekuta mazingira yalokuzunguka ni machafu basi unakamatwa unawekwa ndani hadi ulipe 50'000/= kama faini.
Swali langu kisheria,je askari hao wana mamlaka ya kuingia ndani ya nyumba yangu kunikaguwa bila ya kibali cha mahakama au ofisa wa polisi? Iwapo hawana mamlaka ni kitu gani natakiwa kufanya ili kutetea na kulinda haki yangu?
Sent using Jamii Forums mobile app