Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Mkuu hivi hizi core za Atom kifupi utazigundua kwenye processor zinazoanziwa na herufi gani na gani?
hizi aTom za kisasa zinaanziwa na N mwanzoni, za zamani kidogo zilikuwa zinaanziwa na Z na za zamani kabisa N pia.

mfano angalia i5/i3/i7 zilivyo

i3 6100u
i5 6200u
i7 6500u

then angalia Atom zilivyo

pentium N4200
Atom X7 Z8700
atom X5 Z8500 etc

zenyewe namba inaanza herufi kisha namba (N4200) wakati hizi core series zinaanza namba kisha herufi (4200M)

hio ndio tofauti ambayo naona ni rahisi kuijua.

ila jifunze ku google ukiona cpu kama hio unaeka google then unaiangalia specifocation utaona generation na nguvu zake.
 
Naomba nifahamishe kuhusu hii kitu gpu mkuu maana sielewi inakuwaje na pia utaiangalia mf. Kwenye laptop utakayotaka kuinunua?
gpu ni processor ambayo inadeal na graphics tu, vitu vyote unavyoona vina mapicha na rangi nzuri nzuri ujue ni.kazi ya gpu, ukiangalia video, ukicheza games, uki edit video, user interface etc vyote hivyo hutumia gpu, jinsi gpu inavyokuwa kubwa ndio jinsi ambavyo hayo mambo yatafanyika kwa urahisi,

kuona gpu kwenye sehemu ya kusearch ukiclick start kwenye pc andika dxdiag kisha kitatokea ki program, kiclick hicho ki program kitafunguka, nenda kwenye display utaona gpu yako.
 
Thanks a millions Chief [emoji122][emoji122]
 
Naomba kufaham namna ya ku clear caches kwenye window 10
 
Habari zenu wakuu,
Nina tatizo kidogo kwenye PC yangu.
Natumia HP ProBook 470 G2
Windows 8.1.
Naona ghfla touch pad imegoma kufanya kazi
Hai sense wala niki click hairespond, lakini wakati wa ku sighn in nikiwa nimewasha PC kabla sijaingiza password touch pad inafanya kazi vizuri tu.
Tatizo litakua nini?
Msaada tafadhali
Cc: Yoyote mwenye ujuzi.
 
mkuu pengine umeieka off hio touchpad, kabla hujawasha pc inakuwa haijui setting ndio maana inafanya kazi, ukiwasha zile setting zinatake place.

angalia hapa jinsi ya ku disable na ku enable touchpad

http://visihow.com/Disable_and_Enable_the_touch_pad_of_HP_Probook
 
Mkuu Chief hivi hii intel hd graphics 6000 ya macbook air 13inch inaweza kuhandle game zipi kati ya hizi au zote:

NFS The Run
NFS Rivals
Fifa 2017
Assassins creed
GTA V
Hitman
Rise of the Tomb raider
Tomb raider
Mortal kombat XL
The witcher 3

Manake nimetest NFS The Run naona iko fresh sana but before nilikuwa napush hizo game zote hapo juu kwenye laptop Envy i7 6700HQ, Graphics GTX 950m 4GB dedicated
But this Macbook is i5 5250U with intel hd graphics 6000
 
hii comparison ya nguvu
-HD 6000 ina passmark score 832
-nvidia 950m passmark score 1721

hivyo hio nvidia ina nguvu mara mbili ya hio intel HD

mimi natumia HD 4600 na nimecheza GTA V, FiFA 17 vizuri tu, HD 6000 ni kama 30% more powerfull zaidi ya HD 4600, hivyo utacheza hizo game ila jifunze tu kucheza low quality.

mfano Fifa wachezaji wanaweza poteza sura zao kama gpu inazidiwa.

pia hapo sio GPU tu hata hio cpu yako inayoishiwa na U sio nzuri sana kwa games, compare na hio i7

jaribu kudownload game, ikiwa slow njoo tutaangalia namna ya kupunguza resolution
 
Ebwana VP,naomba unisaidie na hii yangu Intel pentium n3530 processor speed 2.1,hii ni generation ngap,na nguvu yake ipoaje
 
Okey thanks, sasa mkuu hivi hizi SSD za Macbook Air napata wapi ili niongeze aisee, maana hii ni ndogo sana it's about 128GB.
 
Okey thanks, sasa mkuu hivi hizi SSD za Macbook Air napata wapi ili niongeze aisee, maana hii ni ndogo sana it's about 128GB.
kwa TZ nyingi ni hizo hizo 128, na ukipata zaidi ya hapo bei itakuwa ghali sana, unaweza agizia online lakini.

pia unatakiwa ufahamu ssd zina connector nyingi sana kuna sata, msata, m2, pcie etc hivyo inabidi ujue model yako inatumia ipi, sababu ukinunua ambayo.sio yako haitafanya kazi.
 
Ebwana VP,naomba unisaidie na hii yangu Intel pentium n3530 processor speed 2.1,hii ni generation ngap,na nguvu yake ipoaje
hizi hazipo kwenye hizi generation za i series, zinaingia hapo kwenye series za atom, generation yake inaitwa braswell,

hazina nguvu mkuu, hizo zinatumia tu umeme kidogo.
 
Mkuu mimi simu yang imezingua screen haifanyi kazi hapa bongo nimekosa screen yake Bestbuy Easy Phone 5.5 Msaada wako mkuu kama unajua app yeyote ambayo naweza agiza na nikapata bila shida
 
Mkuu mimi simu yang imezingua screen haifanyi kazi hapa bongo nimekosa screen yake Bestbuy Easy Phone 5.5 Msaada wako mkuu kama unajua app yeyote ambayo naweza agiza na nikapata bila shida
angalia aliexpress simu nyingi za kichina vifaa vyake vipo humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…