Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Vp kuhusu hp probook 8449?
 
wakuu nafikiria kununua laptot msimu huu ....ni vitu gan vya ndani vya kuzingatia nitakapo kwenda kununua .....nahtaji mawazo yenu
 
Kwanza tuambie dhumuni la kununua laptop hasa ni kufanyia shughuri gani
Na pia tuambie bajeti yako umetenga tshs ngapi yaan kati ya tshs ngapi mpk tshs ngapi
Na je ulikuwa unataka bland new au used ama vyovyote vile ili mradi kuendana na bajeti yako ?

Then tutakushauri kupata bora kulingana pesa yako na unachoenda kufanyia


Zaidi pitia hizi thread zitakupa muongozo




 
wakuu nafikiria kununua laptot msimu huu ....ni vitu gan vya ndani vya kuzingatia nitakapo kwenda kununua .....nahtaji mawazo yenu
Sijajua bajeti gani umeandaa ila kama unampunga mzuri unaweza chukua yenye minimum specs kama hizi
1. Processor
Intel core i3 kwenda juu (i3, i5, i7 & i9) na iwe generation kuanzia ya 7 au AMD ryzen 2000+ series

2. RAM
8GB inakuwa poa maana kuanzia windows 10 huwa inataka ram isiyopungua 4GB angalau iweze kurun vizuri.

3. Storage
Komputa yenye SSD storage hata kama ni 128gb (zipo nyingi tu zinakuwa hybrid yani SSD na Hard disk, OS unaweka kwenye kwenye SSD na data zako unaweka kwenye HDD) faida ya ssd utaona kompyuta inawaka haraka sana na ukifungua programs zinaopen instantly

4. Display
Nowdays hakikisha unachukua pc yenye resolution ya 1080p (e.g. 1920 x 1080) au zaidi hii itafanya maandishi yaonekane vizuri zaidi bila kuona vile viboksibiksi (pixels)

Note: kwa PC kama hii unaweza pata kwa 900K ikiwa mpya.
 
. Aaaah shukrani sana mkuu
 
. Shukran mkuu .....but kwa upande wangu laptop itakuwa kwa masuala ya elimu....kutype
 
. Shukran mkuu .....but kwa upande wangu laptop itakuwa kwa masuala ya elimu....kutype
Basi go to brand new kama upo DSM Anzia mitaa mtaa UHURU round about kujia mnazi mmoja yapo maduka ya wasomari na wahindi
Utapata brand new ya PENTIUM au CELELONI latest ikiwa na 4gb na 500gb HDD au zaidi ambapo bei itakuwa ni kati ya 550000 mpk 750000/= mpya kabisa kwenye box na walanty utapata mwaka mzima

ama la go to used laptop kwa matumizi yako Core i3 inatosha ikiwa na 4gb na 500gb ama zaidi ambapo kwa maduka used mtaa MUHEZA Mkabala na CHINA PLAZA utapata kwa bei kati ya 350000/= mpk 500000/= kutegemea na aina ya laptop na muonekano wake nk
 
. Shukrani mkuu but nipo pande za mbeya
 
Pole sana mkuu ngoja waje wambeya watakupa muongozo
muhimu zingatia mahitaji yako hayahitaji procesa kubwa go tu brand new ya pentium au celelon latest utapata kwa bei nzuri na utaenjoy kubuka dusplay iwe 15.6 na full keyboad
. .....miaka mingi kwako mkuu....kuhusu display umenikumbusha ..coz Mimi pia ni mpenz wa muvi
 
kuna hii Optilex nimeletewa niikague TM i5 - 4570 CPU@3.20 UNAIONAJE Hiyo chief inaweza nifaa,anataka nimpe 300k bei iko fair au anataka anizabue makofi?
 
kuna hii Optilex nimeletewa niikague TM i5 - 4570 CPU@3.20 UNAIONAJE Hiyo chief inaweza nifaa,anataka nimpe 300k bei iko fair au anataka anizabue makofi?
Hio ni 4th Gen, bei ni OK, angalia vitu vyengine kama ram, hdd, psu etc
 
mkuu chief mkwawa nina tatizo moja hapa
nina computer aina ya dell kuna kipindi niliiacha kuitumia kwa muda mrefu sana. kutokana na kuiacha ndani juzi kati nimeamua kuiwasha ili niitumie kidogo cha ajabu kila ikiwaka inaandika maneno yafuatayo.

strike the f1 key to continue,f2 to run the setup utility,f5 to run onbord diagnostics
na ukumbuke kwamba haikuwai kuniambia maneno haya hapo wali na ninaona ni ghafra tu na pindi ninapo press f1 button naona inaganda yenyewe na inashindwa kuendelea kabsa.
 

Attachments

  • IMG_20201229_145927_7.jpg
    350.9 KB · Views: 4
Jaribu kufanya hio diagnosis, ama uingie bios ukAgue kama kila kitu Kinakuwa detected.
 
Dell ndio mchezo wake pale memory battery inapokua imekwisha chaji fungua ndani toa hiyo battery soma namba zake nenda kwenye maduka ya vifaa vya saa utaipita weka mpya rekibisha muda hutaona ona huo ujumbe na itawaka fasta haitakua na ile loading time ndefu
 
Asanteni sana kwa elimu nzuri.
Sasa nikienda kununua laptop used hizi specification naziona wapi? Nyuma ya laptop? Mbele? Au ndani kabisa? Naomba msaada tusiingizwe mjini. Nataka kununua lkn nikifikiria kuuziwa galasha roho inauma.
Chief-Mkwawa Mzimu wa Kolelo na wengine msaada plz.
 
Ndani, mwambie awashe laptop kisha nenda my computer ama this pc halafu right click chagua properties.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…