Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Hivi kaka mtu akisema graphic card wakati wa kuzungumzia PC au akisema graphics maana yake anamaanisha GPU au kuna maana zaidi ya GPU?
Gpu ni graphics processing unit, ndo hio hio graphic card, japo Neno graphics linaweza kuwa na maana Pana zaidi ila watu pia hulitumia kwa maana hio.
 
Gpu ni graphics processing unit, ndo hio hio graphic card, japo Neno graphics linaweza kuwa na maana Pana zaidi ila watu pia hulitumia kwa maana hio.
Shukrani sana mkuu,mimi shida yangu kubwa sasa hivi ni vitu vya kuzingatia wakati wa kufanya upgrading ya desktop.Nimezama google nikapata maarifa kadhaa lakini kuna maswali mengi bado yamebakia kichwani pangu.

Ninajua ya kwamba nikitaka kuupgrade kitu kama CPU mambo makubwa mawili ya kuangalia ni motherboard compatibility pamoja na powersupply.Sasa:

1.Je, kama CPU niliyonunua inahitaji pawersupply kiasi fulani ni lazima motherboard yangu iwe na uwezo wa kutoa power supply hiyo au kuna jinsi ninaweza kufanya kupata powersupply hiyo bila ya kubadili motherboard?Je,kuna mambo mengine ya kuzingatia wakati wa kuupgrade CPU tofauti na motherboard compatibility pamoja na power supply?

2.Je,nikitaka kuupgrade GPU ni lazima pia niangalie compatibility ya motherboard pamoja na powersupply kama ilivyo kwa CPU?Ni lazima pia motherboard yangu iwe na uwezo wa kutoa powersupply inayotakiwa na GPU yangu au pia kuna jinsi ninaweza kufanya nikapata powersupply husika bila ya kununua motherboard mpya?Je,ni mambo gani mengine ya kuzingatia wakati wa kuupgrade GPU?

3.Je,nikitaka kuupgrade HDD kwenda SSD pia ni lazima kuwe na compatibility ya motherboard au kila motherboard ina sehemu ya kuchomeka SSD card?Je motherboard iliyokuja na HDD peke yake ninaweza kuweka SDD?Ni mambo gani ya kuzingatia nikitaka kuongeza SDD katika desktop yangu?

4.Je nikitaka kuugrade RAM kuna mashariti yoyote yale kama motherboard compatibility,power supply,e.t.c au ni ishu tu ya kuchomeka RAM basi?Je katika motherboard sehemu za kuchomeka RAM zipo nyingi au ni limited kwa sehemu mbili tu?Je,ukubwa wa RAM unapaswa kuwa na uhusiano na ukubwa wa CPU au ninaweza kuweka ukubwa wa RAM kadri nipendavyo bila ya kujali ukubwa wa CPU,yaani ninaweza kuweka RAM ya 100GB wakati processor ni ndogo sana?

5.Je,ninaweza kuupgrade peripherals kama vile ports mbalimbali za desktop bila ya kubadili motherboard?Je,ninaweza kuupgrade USB port kwenda C bila ya kubadili motherboard?
 
Mkuu cpu ndio zinahitaji powersupply na motherboard compability ila cpu tunazotumia sisi nyingi zinakula umeme kawaida around watts 50 mpaka 120 hivi, hivyo isikusumbue sana hapa, ila gpu ndio ina mziki kwenye ulaji umeme tutaiongelea chini.

Na kama kitu kinakula umeme tu wa kawaida motherboard board inatoa tu umeme toka kwenye powersupply ila kama umeme ni mwinyi zaidi inabidi utoke direct toka powersupply, hili pia tutaliongelea tena kwenye Gpu.

Na motherboard ndio kama jina lilivyo ndio base ya computer yako, bodi mama hivyo compability zake ndio zitakazoamua vifaa vyengine.
Ndio unaponunua Gpu inabidi uangalie motherboard sema gpu zetu za kimasikini nyingi ni compatible na motherboard zote.

Moja ya Sababu kwanini gpu hazichomekwi kama flash ni kwamba zinapitisha data nyingi Sana hakuna port inayoweza kuhandle isipokua pciE


PciE x 16 ndio tunachomeka Gpu yenye we kama picha ya juu inayoonesha inapitisha GB 80 kwa sekunde, hivyo motherboard zote za karibuni zina hio pciex16,

Ila hizo pcie 16 nazo zina version ya kisasa kabisa ni v. 6.0 ambayo inapita hio 80GB inakwenda hadi 120GB kwa sekunde, sema isikuhangaishe kichwa unless Unataka kutengeneza pc ya zaidi ya milioni 10, ni high-end hardware pekee kama rtx 3080 gpu inaweza kutake advantage ya hio bandwidth.

Tuje sasa kwenye powersupply, Hapa ndio muhimu zaidi kwenye gpu, tutagawanya gpu kwenye makundi mawili.

1. Kundi la kwanza Gpu ambazo zinakuwa umeme mdogo toka kwenye motherboard (watts 0 mpaka 75) hizi zinaitwa low profile, zinakuja kawaida bila waya WA umeme, ikija unaichomeka tu kwenye desktop. Hizi hata powersupply ikiwa ni ndogo haina Neno around watts 240 mpaka 300.

2. Kundi la pili ni gpu zenye waya WA umeme ambayo unaconnect direct kwenye powersupply bila kutumia umeme wa motherboard hizi ndio zinakula umeme balaa, Tegemea na gpu powersupply inaweza kuwa watts 400, 600, 700 etc.

Jambo jengine la kuangalia ni nafasi, kuna Gpu ni nene na ndefu Angalia nafasi ya case yako ya desktop.
Zipo ssd za Sata, hizi Zina ingia kwenye motherboard yoyote, ila kama unataka ssd za kisasa kama m2, nvme etc inabidi iwe na port husika, unaangalia specs za motherboard kuiona, pia ni port hizi hizi hutumika kwenye network ukitaka kuweka wifi za kisasa na Bluetooth.
Ram nazo pia zina aina sema hazibadiliki sana kama cpu na gpu, mfano kuanzia Enzi za core 2 duo mpaka gen ya 6 tumetumia aina moja ya ram ddr3, na kuanzia gen ya 6 mpaka Leo ni ddr4 (gen ya 6 inasupport zote ddr3 na ddr4) na ddr5 soon inakuja.

Hivyo kwa sasa unaangalia tu hizo ddr.

Kuhusu idadi ya ram unaweza weka Kadri unavyotaka kutokana na matumizi yako, ila sweet spot kwa average user ni GB 16, zaidi ya hapo kama ni pro, unaweza ukaweka gb 32 ama 64 kama future proof,
5.Je,ninaweza kuupgrade peripherals kama vile ports mbalimbali za desktop bila ya kubadili motherboard?Je,ninaweza kuupgrade USB port kwenda C bila ya kubadili motherboard?
Sababu pcie ina bandwidth kuliko port za kawaida unaweza kuitumia hio kujiongezea ports, mfano.
1. Unaweza eka Gpu ikakupa ports kama VGA, Dvi, HDMI, Display ports etc
2. Unaweza weka adapter mbalimbali zikakupa Ether net, USB type C, wifi, Bluetooth etc.

Mfano huu


Na haziwi gimmicks kama port za simu ama laptop ambayo wanaweka type C na USB 2.0 hizi unakuta za ukweli type 3.1 na bandwidth yake yote.
 
Mkuu kuna mtambo huu nimeudaka kwa mshkaji. Ni HP ....ila haina betri .....je huwa betri zake...... Zinauzwa bei gan
 
Mkuu shukrani sana.Katika haya mambo ya desktop kuna tofauti gani kati ya socket na motherboard?Kwa sababu katika hiyo picha hapo chini tuna intel LGA 1151 socket ambayo ndani yake ina motherboards mbalimbali ambazo zimetoka katika vipindi tofauti tofauti kama vile series ya 100,200 na 300.Sasa kuna tofauti gani kati ya socket na motherboard?Socket ni nini?
 
Kama tulivyooongea juu unaweza upgrade Cpu gen moja zaidi, mfano motherboard za 2nd gen unaweza weka cpu za 3rd gen hivyo socket hio inamaanisha gen zote hizo zinaingiliana.

Kwanini gen ya 6 mpaka hio ya 9 socket haijabadilika? Sababu ni kwamba Intel Ana matatizo kwenye mitambo yake ya kutengenezea Cpu, amekwama kwenye 14nm kwa muda mrefu sana, hivyo kila mwaka anaongeza clock speed na core tu lakini Architecture ni ile ile ya Gen ya 6,

Japo socket ni moja Intel wamezitenganisha makunndi mawili

Kuna lg 1151 series 200
Na lg 1151 series 300

Angalia zaidi hapa

Kuhusu hizo H, B na Z series hizo ni feature za motherboard, H mara nyingi motherboard zake ni za kawaida hazina mambo mengi unakuta hata slot za ram ni 2 tu. Z zenyewe ndo zile zina mambo kibao, slot 4 za ram, Inaweza ku overclock cpu, ram, Zina wifi za kisasa etc.
 
Shukrani mkuu,hiyo socket ni kitu ambacho ni physical na ninaweza kukiona na kukishika kama ilivyo motherboard?
 
Mkuu nilikuwa busy nasoma majibu yako,nimeelewa vizuri sana ila bado kuna vitu hivi vinanitatiza:

1.Mkuu unaposema kuwa GPU zetu za kimasikini ni compatible na motherboard zote unamaanisha kuwa kama motherboard yangu ni intel basi nikienda kununua GPU ya intel wala nisiumize kichwa kuwa itaingia kwenye motherboard yangu au laa?Maana yake GPU yoyote ile ya intel itaingia kwenye hiyo motherboard yangu ya intel?

2.Je,hizi GPU ambazo zinakula umeme mwingi na zinakuja na waya wake wa umeme huwa zinafungwa ndani ya motherboard au hizi zinakuwa nje ya desktop?(external).Namaanisha, je huwa zinafungwa ndani ya motherboard halafu waya wake wa umeme unatoka nje ya desktop kwa ajili ya kwenda kwenye power supply?

3.Je,RAM aina ya ddr4 inaweza kuingia kwenye desktop ya core 2 duo mpaka generation ya 5?

4.Hizi adapter ambazo zinatoa port ya USB C au 3.1 huwa zinafungwa ndani ya motherboard ya desktop au huwa ni external?
 
Shukrani mkuu,hiyo socket ni kitu ambacho ni physical na ninaweza kukiona na kukishika kama ilivyo motherboard?
hii ni picha ya Cpu kwa nyuma,
Socket sasa inakaa kwenye motherboard kila kichuma cha cpu hapo ama kibati kina sehemu yake ina gusa kwenye motherboard.

Kwa upande wa motherboard inakuwa hivi.



Hivyo hapo unachomeka cpu yako na kufunga huo mlango,
 
Ohhhhh kumbe pale tunapochomeka CPU ndiyo socket yenyewe!
Sasa wakisema LGA 1151 ama 1150 ama nyenginezo wa Namaanisha mpangilio wa hizo pini sasa, ukichukua cpu ya LGA 1150 ukichomeka kwenye socket ya 1151 pini zake zinakuwa hazishahabiani hivyo hazikai vizuri na computer haitawaka.
 
Sasa wakisema LGA 1151 ama 1150 ama nyenginezo wa Namaanisha mpangilio wa hizo pini sasa, ukichukua cpu ya LGA 1150 ukichomeka kwenye socket ya 1151 pini zake zinakuwa hazishahabiani hivyo hazikai vizuri na computer haitawaka.
Shukrani sana Kaka!🙏🙏🙏
 
Hizi laptop za zamani mkuu unaingia tu machimbo machinga complex, Aggrey etc maduka ya mtumba.
Mkuu kuna mtambo huu nimeudaka kwa mshkaji. Ni HP ..iko flesh sana..ila haina betri .....je huwa betri yake..inaweza.... Unauzwa bei gan
 
Nimeona hiii kupatana Ila cjajua kama zina quality nzuri ila bei take NAyo imechangamka sana[emoji848][emoji848]View attachment 1734967
Bei si mbaya mkuu, ni decent monitor, na achana na TV si nzuri kwa kutumia pc unless Una hela ununue TV kama za LG nanocell.

Ila endelea kutafuta mkuu, full HD monitor zipo nyingi mtaani.
 
Najifunza mengi hapa, nina tower 3 hivi nitazifufua ziwe kitu kikubwa.
 
Sasa wakisema LGA 1151 ama 1150 ama nyenginezo wa Namaanisha mpangilio wa hizo pini sasa, ukichukua cpu ya LGA 1150 ukichomeka kwenye socket ya 1151 pini zake zinakuwa hazishahabiani hivyo hazikai vizuri na computer haitawaka.
Kaka kuna kitu nilitaka kujifunza ila nimekwama,naomba kama unaweza kunipa link.Nilitaka nijifunze mpangilio wa CPU socket zote za intel za desktop tokea zile za mwanzo kabisa hadi sasa hivi katika format ifuatayo:Jina la socket,mwaka ambapo hiyo socket imetoka,hiyo socket ina series gani za motherboards na motherboard hizo zinasupport CPU gani.Nilitaka nijifunze hayo kuanzia motherboards za mwanzo kabisa za akina dure 2 core,celeron,pentium hadi huku kwa akina core i sereies.Je,kuna website inaweza kunisaidia katika hili?
 
Bei si mbaya mkuu, ni decent monitor, na achana na TV si nzuri kwa kutumia pc unless Una hela ununue TV kama za LG nanocell.

Ila endelea kutafuta mkuu, full HD monitor zipo nyingi mtaani.
Mkuu hizi hapa chini ni screenshots kutoka CPU.upgrades.com,kuna vitu kadhaa naomba msaada wako latika ufafanuzi:

1.Tonafahamu kuwa kwa mfano socket ya LGA 1151 maana yake ni kwamba hiyo socket ina vile vipini vidogo dogo kiasi cha 1,1151.Je,kazi ya hivi vipini ni nini?Je,socket yenye vipini vichache mfano 765,hii inamaanisha hii socket haina nguvu sana?

2.Kwenye hii website wanaonyesha socket,motherboards mbalimbali ndani ya hiyo socket pamoja na CPU ambazo ziko supported na hiyo motherboard mfano wanaandika core i3,core i7 na kadhalika lakini hawaonyeshi generations.Je,nikitaka kujua motherboard fulani inasupport generation gani ya CPU naangalia wapi?

4.Kuna socket hapo inaitwa 1366 ina motherboard inayosupport CPU za xeoni.Je,motherboard kama hii inasupport CPU za xeoni peke yake au pia itakuwa inasupport na CPU zote za generations za nyuma kama vile pentium,Celeron,core i series na kadhalika?

5.Kuna faida gani kwa motherboard ambayo ina CPU socket kubwa mfano 1151,1366 na kadhalika?

6.Motherboard nzuri ni ipi?Ni ile yenye socket yenye namba kubwa pekee mfano 1366?
 
Jinsi socket inavyokuwa latest ndio Jinsi ilivyo nzuri hata kama socket ya 765 ni nzuri itakusaidia nini kama cpu zake ni slow sana? Hivyo vipini ni design tu, usiviweke sana kichwani na kukuinfluence kwenye mawazo yako wakati unachagua pc.
Jaribu pcpartpicker ukichagua motherboard itakupa aina cpu and vice versa, pia Wikipedia wanakuwa na hizi list
Mfano hii
Ukiclick motherboard husika ina kupeleka moja kwa moja site ya Intel unaona na support.
4.Kuna socket hapo inaitwa 1366 ina motherboard inayosupport CPU za xeoni.Je,motherboard kama hii inasupport CPU za xeoni peke yake au pia itakuwa inasupport na CPU zote za generations za nyuma kama vile pentium,Celeron,core i series na kadhalika?
Xeon ni professional cpu japo zinatumika same architecture na Cpu za kawaida, motherboard zake ni tofauti, huwa kimakusudi Intel wanazitofautisha na motherboard za majumbani kawaida, kuna baadhi ya mods watu wanafanya lakini kurun xeon kwenye mobo za kawaida, na motherboard za xeon zinakuwa na Bei ndefu sana.
5.Kuna faida gani kwa motherboard ambayo ina CPU socket kubwa mfano 1151,1366 na kadhalika?
Uzuri wa motherboard si hizo socket Bali ni features nyengine, fatilia H series, B na Z series zaidi kuliko socket, socket ipo hivyo Sababu ya maamuzi tu na design ambazo zipo nje ya uelewa wetu watumiaji wa kawaida.
6.Motherboard nzuri ni ipi?Ni ile yenye socket yenye namba kubwa pekee mfano 1366?View attachment 1736386View attachment 1736387View attachment 1736388
Kama nilivyosema juu motherboard nzuri si socket Bali ni series yake, motherboard ya elfu 60 na motherboard ya milioni 1 zote zinaweza kuwa na socket moja, ukipata motherboard Z series high-end ndio inakuwa nzuri zaidi utapata features za kisasa kama
-uwezo wa ku overclock,
-support ya frequency kubwa
-slot nyingi za ram
-slot nyingi za storage
-optical audio
-wifi 6
-gigabit ether net etc

Mfano Angalia hii
Amazon product ASIN B087LHPYT6
Hivyo socket ni lazima iwepo ile ile Haijalishi ni motherboard ipi ila features zinabadilika baina ya H, B na Z motherboard.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…