Mkuu cpu ndio zinahitaji powersupply na motherboard compability ila cpu tunazotumia sisi nyingi zinakula umeme kawaida around watts 50 mpaka 120 hivi, hivyo isikusumbue sana hapa, ila gpu ndio ina mziki kwenye ulaji umeme tutaiongelea chini.
Na kama kitu kinakula umeme tu wa kawaida motherboard board inatoa tu umeme toka kwenye powersupply ila kama umeme ni mwinyi zaidi inabidi utoke direct toka powersupply, hili pia tutaliongelea tena kwenye Gpu.
Na motherboard ndio kama jina lilivyo ndio base ya computer yako, bodi mama hivyo compability zake ndio zitakazoamua vifaa vyengine.
Ndio unaponunua Gpu inabidi uangalie motherboard sema gpu zetu za kimasikini nyingi ni compatible na motherboard zote.
Moja ya Sababu kwanini gpu hazichomekwi kama flash ni kwamba zinapitisha data nyingi Sana hakuna port inayoweza kuhandle isipokua pciE
PciE x 16 ndio tunachomeka Gpu yenye we kama picha ya juu inayoonesha inapitisha GB 80 kwa sekunde, hivyo motherboard zote za karibuni zina hio pciex16,
Ila hizo pcie 16 nazo zina version ya kisasa kabisa ni v. 6.0 ambayo inapita hio 80GB inakwenda hadi 120GB kwa sekunde, sema isikuhangaishe kichwa unless Unataka kutengeneza pc ya zaidi ya milioni 10, ni high-end hardware pekee kama rtx 3080 gpu inaweza kutake advantage ya hio bandwidth.
Tuje sasa kwenye powersupply, Hapa ndio muhimu zaidi kwenye gpu, tutagawanya gpu kwenye makundi mawili.
1. Kundi la kwanza Gpu ambazo zinakuwa umeme mdogo toka kwenye motherboard (watts 0 mpaka 75) hizi zinaitwa low profile, zinakuja kawaida bila waya WA umeme, ikija unaichomeka tu kwenye desktop. Hizi hata powersupply ikiwa ni ndogo haina Neno around watts 240 mpaka 300.
2. Kundi la pili ni gpu zenye waya WA umeme ambayo unaconnect direct kwenye powersupply bila kutumia umeme wa motherboard hizi ndio zinakula umeme balaa, Tegemea na gpu powersupply inaweza kuwa watts 400, 600, 700 etc.
Jambo jengine la kuangalia ni nafasi, kuna Gpu ni nene na ndefu Angalia nafasi ya case yako ya desktop.
Zipo ssd za Sata, hizi Zina ingia kwenye motherboard yoyote, ila kama unataka ssd za kisasa kama m2, nvme etc inabidi iwe na port husika, unaangalia specs za motherboard kuiona, pia ni port hizi hizi hutumika kwenye network ukitaka kuweka wifi za kisasa na Bluetooth.
Ram nazo pia zina aina sema hazibadiliki sana kama cpu na gpu, mfano kuanzia Enzi za core 2 duo mpaka gen ya 6 tumetumia aina moja ya ram ddr3, na kuanzia gen ya 6 mpaka Leo ni ddr4 (gen ya 6 inasupport zote ddr3 na ddr4) na ddr5 soon inakuja.
Hivyo kwa sasa unaangalia tu hizo ddr.
Kuhusu idadi ya ram unaweza weka Kadri unavyotaka kutokana na matumizi yako, ila sweet spot kwa average user ni GB 16, zaidi ya hapo kama ni pro, unaweza ukaweka gb 32 ama 64 kama future proof,
Sababu pcie ina bandwidth kuliko port za kawaida unaweza kuitumia hio kujiongezea ports, mfano.
1. Unaweza eka Gpu ikakupa ports kama VGA, Dvi, HDMI, Display ports etc
2. Unaweza weka adapter mbalimbali zikakupa Ether net, USB type C, wifi, Bluetooth etc.
Mfano huu
Na haziwi gimmicks kama port za simu ama laptop ambayo wanaweka type C na USB 2.0 hizi unakuta za ukweli type 3.1 na bandwidth yake yote.