Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Kwa dukani processor ya i3 1st, 2nd gen si chini ya 280k ila mtaani hata i3, i5, i7 generation yoyote unapata kwa bei yoyote hata 50k kwasababu hazina demand sana, asilimia kubwa ya watu wanamiliki(desktop) pentium 4, na core2duo, na wachache core2quad, xeon na pia wachache sana i3, i5, i7,

Nashukuru sana kaka.
 
Nisaidie hapa, intel (R) Celeron (R) CPU B800 @1.50GHz 1.50GHz CHIEF MKWAWA
 
Last edited by a moderator:
Nisaidie hapa, intel (R) Celeron (R) CPU B800 @1.50GHz 1.50GHz CHIEF MKWAWA

hii ni sandy bridge processor, ambayo ni second generation. sio mbaya kwa matumizi ya kawaida kama kuperuzi internet, kuangalia video na kutumia software za office.

ila kama utataka mambo kama kucheza games kubwa au kufanya video editing utakuwa unaionea
 
Last edited by a moderator:
Kwa wale wataalamu wa computer nini tofauti kati ya izo vitu kwenye performance ya Laptop.
 
CHIEF MKWAWA sina jinsi ya kujua huo mchanganuo wako ila hapa chini kulia mwa keyboard kuna sticker ya logo ya intel na maneno haya (intel -inside -pentium) lapto yenyewe ni Dell Inspiron 3542 laptop P-PCS 3558U/2GB/500GB/DVDW//WC/UBUNTU.
Niambie uwezo wake tafadhali
 
asante sana mkuu nimekusoma
cpu z.png
 
CHIEF MKWAWA sina jinsi ya kujua huo mchanganuo wako ila hapa chini kulia mwa keyboard kuna sticker ya logo ya intel na maneno haya (intel -inside -pentium) lapto yenyewe ni Dell Inspiron 3542 laptop P-PCS 3558U/2GB/500GB/DVDW//WC/UBUNTU.
Niambie uwezo wake tafadhali

nenda my computer, right click then properties, soma jina la cpu then lilete hapa.
 
Hebu cheki hii Chief:
2.4Ghz dual-core Intel Core i5 with 3MB L3 cache, turbo boost up to 2.9Ghz.

Hii ni macbook pro 13" ssd 128 flash storage with retina display.
 
Hebu cheki hii Chief:
2.4Ghz dual-core Intel Core i5 with 3MB L3 cache, turbo boost up to 2.9Ghz.

Hii ni macbook pro 13" ssd 128 flash storage with retina display.

hapo jina la processor hujalitaja kaka, inte core i5 xxxx kuna namba inatakiwa iwe mbele ya processor
 
Kuna watu tukienda shop tukiona i7 tunachanganyikiwa...kumbe hata i5 inaeza kua na uwezo kushinda i7...nadhan kabla ya kununua pc ni vyema mtu akapitia hii elimu...ningeomba Chief-Mkwawa ukipata chance tueleweshe pia kuhusu HDD na RAM maana nazo zina mchango katika perfomance ya pc!!!
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu tukienda shop tukiona i7 tunachanganyikiwa...kumbe hata i5 inaeza kua na uwezo kushinda i7...nadhan kabla ya kununua pc ni vyema mtu akapitia hii elimu...ningeomba Chief-Mkwawa ukipata chance tueleweshe pia kuhusu HDD na RAM maana nazo zina mchango katika perfomance ya pc!!!

soon nitapost kaka
 
Last edited by a moderator:
ya kawaida tu hiyo kaka kuangalizia video, office software na kuperuzi mtandao
Ahsante Chief Mkwawa ,kwa kuongezea hii ndio ile niliyopigwa (refer uzi mmoja niliyoomba ushauri kati ya hii na toshiba)450$ a piece nilizinunua mbili kwa dola 900$.sikuweza kucancel kwa sababu nilikuwa nimesha seal deal!
the only consolation is there is a next time and i will be prepared and wiser!
 
Maelezo mazuri sana Chief Mkwawa.. I used to fight with Chief kwenye suala la Nokia na Symbian.. Tupo pamoja mkuu
 
Intel(R) Core(TM)2 Duo CPU P8600 @2.40GHz 2.40GHz

Ram ni 2GB
PC ni dell latitude E6400

Je hiiiii processor iko kundi gani Chief-Mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.

Kwa hii ni kundi gani
Intel(R) Pentium(R) CPU N3540 @ 2.16GHz 2.16GHz
 
Intel(R) Core(TM)2 Duo CPU P8600 @2.40GHz 2.40GHz

Ram ni 2GB
PC ni dell latitude E6400

Je hiiiii processor iko kundi gani Chief-Mkwawa

hio ni before hata generation za i3,i5,i7 ni processor za zamani sana sema kipindi chake zilikuwa zina nguvu. hio ni equivalent na pentium za generation ya 4
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom