Yenye herufi gani mwisho au sio lazima sana hili.I5 3rd gen kupanda. Na gpu amd radeon 550
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yenye herufi gani mwisho au sio lazima sana hili.I5 3rd gen kupanda. Na gpu amd radeon 550
Za desktop mainstream hazina herufi kwa mbele mfano i7 3770.Yenye herufi gani mwisho au sio lazima sana hili.
Cpu i7 ipo juu, kuanzia gen ya 8 ndio inabidi uwe makini ila gen za nyuma i7 itakuwa juu.Hivi ina maana core i3 ya generation ya 6 ni kali kuliko i7 ya 4rth gen?!!!
Cpu i7 ipo juu, kuanzia gen ya 8 ndio inabidi uwe makini ila gen za nyuma i7 itakuwa juu.
Ila kwenye Gpu za ndani gen za mbele zina gpu nzuri zaidi, mfano i3 6th gen yenye intel HD 530 itacheza games vizuri zaidi kuliko i7 yenye hd 4600.
Hivyo hapo inategemea. Kama una mpango wa kuwa na dedicated gpu i7 4th gen ni nzuri zaidi ila kama huna mpango wa kuwa na dedicated gpu tafuta hata i3 gen za mbele. Ikiwa i3 8th gen ni bora zaidi maana ina core 4.
Non dedicated ama igpu (internal gpu) inakuja na processor built in inakuwa kwenye package moja. Yenyewe imetengenezwa kufanya matumizi yako madogo yote kama kuangalia movies, kuconect monitor, kubrowse, etcMkuu hapa dedicated na non dedicated gpu zinatofautiana vp kwa matumizi!?
Non dedicated ama igpu (internal gpu) inakuja na processor built in inakuwa kwenye package moja. Yenyewe imetengenezwa kufanya matumizi yako madogo yote kama kuangalia movies, kuconect monitor, kubrowse, etc
Dedicated gpu ipo separate na mara nyingi inatengenezwa na kampuni tofauti inakuwa na nguvu sana kushinda igpu sometime hadi mara kumi zaidi na pia inafanya mambo makubwa zaidi kushinda igpu. Mfano kudrive monitor nyingi sana,kucheza games kubwa kubwa, kufanya editing na animations,kurun software mbalimbali za proffesionals etc.
Hio ni HD4600 sio dedicated ni gpu ya ndani.
K hata generation ya 4 ni nzuri zaidi kushinda HQ ya gen ya 7.ivo HQ kwenye generation ya saba na K kwenye generation ya 8 ipi iko juu
Je hQ na MQ ipi iko vzuri zikiwa ktk same cpu + gen???K hata generation ya 4 ni nzuri zaidi kushinda HQ ya gen ya 7.
K ni ya desktop imetengenezwa kwa ajili ya overclock inatumia umeme mwingi zaidi mara nyingi watts 95 ama zaidi na ndio top of overall perfomance.
HQ ni ya laptop yenyewe inatumia watts kama 45 hivi kwa laptop za gen za zamani hii tunaweza kusema ndio top of line.
So inategemea na wewe mwenyewe unataka laptop ama desktop ni cpu ambazo zinakidhi mahitaji tofauti.
Ila kwa laptop kama unanunua sasa hivi tafuta zinazoishiwa na H mfano i5 8400H ama i5 8300H itakuwa na nguvu kushinda i7 zinazoishiwa na HQ za zamani sababu kwenye Gen ya 8 intel ameongeza core hizo i5 zina core 6 compare na HQ zilizokuwa na core 4.
MQ imekuwa discontinued siku hizi ila kwa zama zake hizo zenye M inamaanisha ni cpu ambazo zinachomoka, mfano una i5 4200m unaweza ukaitoa na ukaeka i7 4600m ama i7 4702MQ etcJe hQ na MQ ipi iko vzuri zikiwa ktk same cpu + gen???
Sent from my SM-G935F using Tapatalk
Nimekulewa Chief kama jina lakoMQ imekuwa discontinued siku hizi ila kwa zama zake hizo zenye M inamaanisha ni cpu ambazo zinachomoka, mfano una i5 4200m unaweza ukaitoa na ukaeka i7 4600m ama i7 4702MQ etc
Zenye Hq zilikuwa zinechomelewa kwenye motherboard kama ni i7 4700HQ utakaa nayo hiyo hiyo hadi laptop ife.
Kuhusu perfomance zinafanana.
1. nimekutana na intel pentium N4200, 1.5ghz, acer nyembambahii ina
Intel Core i3 2310M / 2.1 GHz
-kwanza ni intel i3 ambayo siombaya
-pili namba yake imeanziwa na elfu mbili yaani 2310 inamaana ipo second generation pia sio mbaya
-herufi ya mbele ni M ina maana ni mobile hivyo utapata perfomance kubwa kushinda za U na Y
-clock speed ni 2.1ghz ambayo nayo kwa laptop ni nzuri tu.
hata single core perfomance ya hio processor ni nzuri
overall ni laptop nzuri kwa matumizi ya kawaida huwezi kuwa slow
Hii ni cpu ya kisasa ila ipo slow, itafanya mambo mengi ya kileo kama kuplay video za 4k, support ya codecs mpya, video editing ya quicksync etc sema sio powerhouse usitegemee kuweka software nzito yoyote ifanye kazi vizuri.1. nimekutana na intel pentium N4200, 1.5ghz, acer nyembamba
Hii ina nguvu na gpu dhaifu ila nayo ni ya zamani,kama miaka 7 ama 8 iliopita hivyo tunaiweka kama used.2. nimekutana na core i5 2520M, 2.5 ghz, dell
Hii ni ya kizamani na inatumia umeme mwingi kuliko pentium N4200 hivyo naona kama haina maana kama unanunua laptop sasa hivi. Na jina nafikiri ni pentium 987 badala ya 982.3. nimekutana na intel pentium cpu 982, 1.5 ghz. sony nyembamba.
Hutaweza ku upgrade graphics, na bei ya hizo laptop ni ipi?na wewe una budget gani? Ili kama kuna option nzuri zaidi nikupe.nichague ipi kati ya hizo mkuu, matumizi yangu makubwa nataka kujifunza programming.
hii dell graphics yake imekaa kizamani je inawezekana kuiupdate.
injinia asanteComputer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
kuhusu budget isizidi laki 4 na nusu, bei zake kuanzia laki tatu na nusuHii ni cpu ya kisasa ila ipo slow, itafanya mambo mengi ya kileo kama kuplay video za 4k, support ya codecs mpya, video editing ya quicksync etc sema sio powerhouse usitegemee kuweka software nzito yoyote ifanye kazi vizuri.
Advantage yake inakaa sana na charge.
Hii ina nguvu na gpu dhaifu ila nayo ni ya zamani,kama miaka 7 ama 8 iliopita hivyo tunaiweka kama used.
Hii ni ya kizamani na inatumia umeme mwingi kuliko pentium N4200 hivyo naona kama haina maana kama unanunua laptop sasa hivi. Na jina nafikiri ni pentium 987 badala ya 982.
Hutaweza ku upgrade graphics, na bei ya hizo laptop ni ipi?na wewe una budget gani? Ili kama kuna option nzuri zaidi nikupe.
ahsante sana muheshimiwa kwa ufafanuzi na nimeamua kuachana nazo kwanza, leo nimekutana na hii jamaa kanianzia laki 4.Hii ni cpu ya kisasa ila ipo slow, itafanya mambo mengi ya kileo kama kuplay video za 4k, support ya codecs mpya, video editing ya quicksync etc sema sio powerhouse usitegemee kuweka software nzito yoyote ifanye kazi vizuri.
Advantage yake inakaa sana na charge.
Hii ina nguvu na gpu dhaifu ila nayo ni ya zamani,kama miaka 7 ama 8 iliopita hivyo tunaiweka kama used.
Hii ni ya kizamani na inatumia umeme mwingi kuliko pentium N4200 hivyo naona kama haina maana kama unanunua laptop sasa hivi. Na jina nafikiri ni pentium 987 badala ya 982.
Hutaweza ku upgrade graphics, na bei ya hizo laptop ni ipi?na wewe una budget gani? Ili kama kuna option nzuri zaidi nikupe.
Hio ya sasa hivi ni 1st gen haina maana na hio laki 4 ni ghali.kuhusu budget isizidi laki 4 na nusu, bei zake kuanzia laki tatu na nusu
ahsante sana muheshimiwa kwa ufafanuzi na nimeamua kuachana nazo kwanza, leo nimekutana na hii jamaa kanianzia laki 4.
intel(R) core (TM) i5 CPU M520 @2.53 GHZ