kipara feki
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 231
- 210
Kwa bajeti ya laki Sita nitapata laptop yenye specification zipi ambayo ni used kutoka kampuni ya dell CHIEF MKWAWA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Gen ya 6 unapata, i3 ama i5Kwa bajeti ya laki Sita nitapata laptop yenye specification zipi ambayo ni used kutoka kampuni ya dell CHIEF MKWAWA
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Hii ni gen ya 7 official haikubali win 11 ila unaweka.Chief naomba msaada wa kujua kwa nini hii mashine kila nikiweka windows 11 inakataa kwamba hameet requirementsView attachment 2313039
toa neno mkuuHii ni gen ya 7 official haikubali win 11 ila unaweka.
Kuna ki program kinaitwa rufus kidownload kwenye machine, download win 11 iso kama unayo tayari tumia rufus kuiweka kwenye flash, Rufus itakupa option ya kuondoa hio requirement.
Hio desktop ya Xeon si mbaya ila ni ya kizamani, toka 2012, cpu yake ina core nyingi ila nguvu ya core 1 ni ndogo.
Chief, intel xeon e5-2666 v3, inafaa kwa software za modeling?Hio desktop ya Xeon si mbaya ila ni ya kizamani, toka 2012, cpu yake ina core nyingi ila nguvu ya core 1 ni ndogo.
Mfano laptop ya i3 ya gen ya 12 inaikalisha hio desktop. Desktop+hio monitor ni ghali kuliko laptop ya i3.
Monitor nayo nzuri kwa media ila kama unafanya vitu serious kama competitive games 60hz si nzuri kwa games, ila overall ina Value. Na pia wanadanganya si mpya
Cpu nzuri sana mkuu. sema tu inakula umeme. Perfomance yake ni equivalent ya i7 gen ya 9, ama original Ryzen 7 1700.Chief, intel xeon e5-2666 v3, inafaa kwa software za modeling?
Asante, GPU gani itafaa ?Cpu nzuri sana mkuu. sema tu inakula umeme. Perfomance yake ni equivalent ya i7 gen ya 9, ama original Ryzen 7 1700.
Inategemea unai pair na gpu gani, ila cpu kama cpu haina shida itafanya hiyo kazi kwa ufanisi.
Angalia power supply mkuu, kama ni ndogo na haina extra pin za Gpu the best kwa Amd ni 6400xt, kwa Nvidia Gtx 1650.Asante, GPU gani itafaa ?
Sawa. [emoji1545]Angalia power supply mkuu, kama ni ndogo na haina extra pin za Gpu the best kwa Amd ni 6400xt, kwa Nvidia Gtx 1650.
Kama ni power supply kubwa inayoweza kumudu gpu nyingi angalia mfuko wako mwenyewe. Ukipata latest kama Rtx 3000 series ama hizi zinazotoka za 4000 series ni vyema zaidi.
Pia angalia minimum requirement ya software unazotumia kupata information zaidi.
Tafuta thinkpad 11e yenye i3 6100u inatosha kwa matumizi yako, ram atleast 8GB na badili hdd weka ssd.Chief-Mkwawa Mkuu heshima tele kwako na nitoe shukrani zangu za dhat kwa kunisaidia kuhusu issue za IT. Nina bajeti ya laki 5 nahitaji laptop zile ndogo kwa size prefarably min laptop ambapo matumiz yangu ni kutumia sana word, excel, powerpoint, kuangalia video files na kusurf internet ambapo naweza kufungua hata page 10 kwa wakati mmoja (japo moja ndiyo inakuwa active yaan naisoma kwa wakati but ni dakik tu naweza switch kwenye page nyingine, then page nyingine). In fact mimi siyo mtu wa gaming but napenda laptop iwe faster siyo nimefungua word documents kama 5 hivi, then kuna audio inaplay background, halaf kuna excel doc 2 zimefunguliwa, then kuna pdf, na powerpoint halaf kuja kuopen browser nakuta laptop nzito hiki ndiyo kitu sikitaki, nataka laptop iwe faster. Kingine mimi ni mdau sana wa kudownload larger video files. So naomba unisaidie kwa matumiz hayo hapo juu nichukue min laptop yenye specification gani mkuu? hapo naongelea zile used na ambaye nitakaa nayo hata 4-5 years na itakuwa inakaa na charge na ambayo itakubali latest window edition na vipogram kama zoom, skype for business n.k napendelea sana HP brand but if kuna brand nyingine nzuri ni sawa we nishauri tu.
Shukrani sana mkuu wakati naitafuta hii uliyonishauri nikakutana na laptop hii Brand : hpTafuta thinkpad 11e yenye i3 6100u inatosha kwa matumizi yako, ram atleast 8GB na badili hdd weka ssd.
11e kioo chake ni inch 11, so ni size ya Tablet tu.
Mtaani vipo used bei inarange 400k mpaka 500k kwa hio i3.
Haina neno mkuu, hakikisha ram ni 8GB, kama ni 4GB cheki kama ipo slot ya ku upgrade ili baadae uongeze ram,Shukrani sana mkuu wakati naitafuta hii uliyonishauri nikakutana na laptop hii Brand : hp
model : Hp Probook 11 G2
processor : core i3
generation : 6th gen
processor type : Intel (R) Core (TM) i3-6100U CPU @ 2.30GHz 2.30GHz (4CPUs)~ Vipi hii mkuu nayo unashaurije ni nzuri kama hiyo Lenovo ya thinkpad 11e yenye i3 6100u? nisamehe bure nimekariri kuwa laptop za HP brand ni nzuri zaidi🤣🤣
Shukran sana Chief kwa ushauri wako Mungu akuzidishie kwa muda wako unaoutoa sadaka kutupa nondo hapa JF.Haina neno mkuu, hakikisha ram ni 8GB, kama ni 4GB cheki kama ipo slot ya ku upgrade ili baadae uongeze ram,
I3 gen ya 8 ina nguvu kuliko i5 gen ya 4 ila utofauti mdogo sana. Hutapata advantage yoyote kubwa.Chief habari za muda kidogo nilipotea ila bado tuko pa1 kwenye group letu Leo na naswali kidgo hapa
Mashine yangu ni core i5 4gen ram8 ddr3 SSD gb128 hard disk tb 4.5 graphic card yangu Ile Ile Rx 550
Ila kwa game zakisasa kama God of war napata performance ndogo Sana nilikuwa nataka kufanya upgrade
Kuna mashine nataka nichukue core i3 8gen ram12 ddr4 ssd GB128 VIP nikiweka na card yangu naweza pata performance ya juu kuzidi Hii core i5 yangu Kaka! Au ninunue card ingne tu?View attachment 2388961
Kwaiyo unanishaulije chief hapo? Ninunue GPU mpya Tu sio?I3 gen ya 8 ina nguvu kuliko i5 gen ya 4 ila utofauti mdogo sana. Hutapata advantage yoyote kubwa.
Sema uzuri wa i3 gen ya 8 ina advantage ya upgrade path nzuri, unaweza huko mbele ukaweka i7 ama i9 gen ya 9.
Minimum requirements ya god of war ni
I5 2500k
Gtx 960M
Hivyo unaona hapo kwenye cpu inataka gen ya 2 tu, cpu yako imekidhi mahitaji ila gpu ndio inataka kubwa zaidi.
Sababu crypto zimecrash gpu zinashuka sana bei, Gtx 1650 na Rx 6400xt sasa hivi ndio zina nguvu zaidi kwa gpu zisizotumia waya, zinazoingia kwenye hizi machine zetu za kina dell na Hp.