zurima ramadhan
Member
- Oct 26, 2024
- 5
- 0
Na Zurima Ramadhan, Zanzibar.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma amesema kuandaliwa kwa mpango mkakati pamoja na muongozo wa ulinzi katika michezo utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika Sekta ya michezo na kuboresaha mazingira wezeshi ya michezo kwa washiriki na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Jinsia katika Michezo Zanzibar pamoja na muongozo wa ulinzi katika michezo uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong Mpirani mkoa wa mjini magharib unguja.
Amesema kupitia mpango huo utasaidia kuweka dira na hatua madhubuti itakayofanikisha maendeleo katika sekta ya michezo kuwa jumuishi na kuzingatia usawa wa kijinsia na kuleta mabadiliko chanya.
Aidha amesema mpango huo ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wanawake na wanaume kupata fursa sawa za kushiriki ili kufanikisha maendeleo katika sekta ya michezo pamoja na kuwawesha wanawake kushiriki kikamilifu katika michezo kuanzia ngazi ya jamii hadi taifa.
Mkurugenzi wa jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA Jamila Mahmoud amesema wameandaa muongozo wa kumlinda mwanamichezo na kupunguza ukatili wa kijinsia katika michezo ili kuwa na mazingira salama, jumuishi, na endelevu ya Michezo kwa wote.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Mfamau Lali Mfamau amesema lengo la Wizara kufanikisha dhamira moja ya kuendeleza usawa wa kijinsia, jumuishi na uwezo wa michezo katika kuleta mabadiliko.
Kwa upande wake Meneja wa kanda ya Michezo kwa Maendeleo Barani Afrika (GIZ) Kristin Richter amesema watahakikisha wanakuza usawa wa kijinsia na ujumuisha kupitia michezo kwa kuhakikisha upatikanaji wa fursa sawa kwa wanawake, wasichana na watu wenye mahitaji maalum ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Kwa upande wake Meneja wa kanda ya Michezo kwa Maendeleo Barani Afrika (GIZ) Kristin Richter amesema watahakikisha wanakuza usawa wa kijinsia na ujumuisha kupitia michezo ili lengo la upatikanaji wa fursa sawa kwa wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu liweze kufikiwa.
Mkakati huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa mradi wa kanda wa michezo kwa maendeleo Afrika unaotekelezwa na GIZ, wadau mbali mbali wakiwemo wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, asasi za kiraia ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA, mashirika ya michezo na jamii kwa ujumla.