Muosha huoshwa

Hicho kisasi ulikilipa kisomi sana.
Uligawa dose ya maana, maumivu yakaingia kimya kimya bila kupigizana kelele.

Kwa maelezo haya na wengine wenye tabia chafu kama hizo wajifunze na wajirekebishe.

Bado hawa wa:'tuma na ya kutolea', halafu mtu haji!

Nabuni mbinu bora ya kulipa kisasi cha mapenzi, ninajua mapenzi yanauma kuliko maumivu ya kupoteza mali, wee ngoja!
 
Kwanini useme si wewe?
 
Mimi siwezi kumfanyia binadam mwenzangu ukatili wa aina hii, hata kama alinitenda mabaya.
Uko sahihi endapo kuipata laki mbili kwako ww ni rahisi yan sio kazi ngumu. Lakini hebu jiweke ktk nafasi ya e.g. kijana msomi hana chanzo cha kipato au ajira inayoeleweka. Anabangaiza huku na kule (Hustler) na ameweza kujinyima akadunduliza hadi imefika 2k. Atasononeka mno (anaweza hata kutoa machozi) akikumbuka sulba alizopitia kufikia kiasi hicho halafu sasa eti lijamaa fulani kwa ulaghai linazichukua kiulaini hivo. Hiyo sio sawa. Sasa roho itasuuzikaje (usinambie habari za mwachie Mungu) kama sio kwa kulipa kisasi kitu ambacho ni sahihi na ni stahili yake?? Tukemee na Tusilee uovu. Ukilipa kisasi tena kwa mafanikio 100% + utaona raha yake. We jaribu uone.
 
Mimi siwezi kumfanyia binadam mwenzangu ukatili wa aina hii, hata kama alinitenda mabaya.
Uko sahihi endapo kuipata laki mbili kwako ww ni rahisi yan sio kazi ngumu. Lakini hebu jiweke ktk nafasi ya e.g. kijana msomi hana chanzo cha kipato au ajira inayoeleweka. Anabangaiza huku na kule (Hustler) na ameweza kujinyima akadunduliza hadi imefika 2k. Atasononeka mno (anaweza hata kutoa machozi) akikumbuka sulba alizopitia kufikia kiasi hicho halafu sasa eti lijamaa fulani kwa ulaghai linazichukua kiulaini hivo. Hiyo sio sawa. Sasa roho itasuuzikaje (usinambie habari za mwachie Mungu) kama sio kwa kulipa kisasi kitu ambacho ni sahihi na ni stahili yake?? Tukemee na Tusilee uovu. Ukilipa kisasi tena kwa mafanikio 100%+ utaona raha yake.
 
😅😅😅kama stori hivi.

Hivi ndivyo inavyokuwa kama wewe ni Mwanaume unawadanganya wanawake kwamba utawaoa miaka inakaka yangu ana miaka 26 unamsubirisha hadi anagonga 31 then unamwambia huna mpango tena umepata mwingine. Kinachofata ni kwa watoto wako au wa dada yako au Kaka yako.

Kuna siku utakuja kujua ni Karma too late.
 
Nimeipenda kiongoz mpambanajii
 
Mzee baba una roho ya kinyama, watu wa jino kwa jino sio wa kukaa nao karibu.
Yaani miezi zaidi ya sita bado una hasira na mchizi kisa laki.
Kama mtu hajali maumivu yako kwa nini wewe ujali ya kwake?

We jamaa ni mbinafsi una roho mbaya kama huyo jamaa wa kwanza.

Hujaona unyama wa Muuza vifaranga wa kwanza unamsema wa pili?
 
Nyie watu wa Pwani mnaua mtu huku mnamchekea. 4R
 
Una akili sana sana. Naamini akili hii kubwa ingetumika katika level za kisector, taasisi, au Mamlaka za umma ingenufaisha Wa Tz wenzio wengi. Kuliko kukunufaisha ww tuu. Na mie nitakutafuta kwa mechi zangu pia mkuu, maana watusikuiz hawajui kujali viatu na mapito ya wengine.
 
Deni Halilipwi kwa Deni

Nilimpenda sana, kwa moyo wangu wote. Alikuwa mwanafunzi, maisha yake yalitegemea hela za wazazi na mara chache alipopata pesa za matumizi, zilikwisha haraka. Lakini kila mara alipokuwa na shida, mimi ndiye niliyemsaidia.

“Mpenzi, naomba nishikie elfu tano tu, nitakurudishia nikitumiwa hela na mzazi,” alisema siku moja. Nilimpa. Lakini siku zikapita, miezi ikapita, hakurudisha.

Mara nyingine tena, “Naomba unisaidie nauli, niko mbali na sina hata senti.” Nikampa tena. Ilikuwa kawaida sasa—alikopa, akaahidi kulipa, lakini hakuwahi kurudisha hata shilingi.

Siku moja alinifuata akiwa na jambo la dharura. Alikuwa na simu aliyotaka kuiuza, akaniomba nimtafutie mteja haraka. Kwa kuwa nilimpenda, sikuona tabu. Nikahangaika, nikazunguka, hatimaye nikampata mtu aliyekubali kununua simu hiyo.

Nilipopokea pesa kutoka kwa mnunuzi, nilizihisi mkononi mwangu na akili yangu ikarudi kwenye madeni yote aliyoniwekea. Nikamwangalia na tabasamu la maana.

“Hizi pesa sizikupi,” nilimwambia kwa utulivu.

Alinitazama kwa mshangao. “Unamaanisha nini?”

“Namaanisha nakudai pesa nyingi sana. Hizi ndio malipo yangu kwa kila hela uliyokopa na hukuwahi kurudisha.”

Uso wake ulibadilika. Alionekana kushangaa, kisha akatikisa kichwa huku akitabasamu kwa huzuni. “Nilifikiri unanisaidia kwa sababu unanipenda.”

“Ndio, nilikupenda. Lakini deni siyo sehemu ya mapenzi.”

Alinyamaza kwa muda, kisha akaondoka bila kusema neno jingine. Tangu siku hiyo, simu zake zilipungua, meseji hazikuja tena.

Na hapo ndipo nilipojifunza somo moja kubwa—dawa ya moto ni moto.
 
Watu wa mbeya ni wakarimu ila ni wa visasi sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…