Muosha huoshwa

Muosha huoshwa

Kama mtu hajali maumivu yako kwa nini wewe ujali ya kwake?

We jamaa ni mbinafsi una roho mbaya kama huyo jamaa wa kwanza.

Hujaona unyama wa Muuza vifaranga wa kwanza unamsema wa pili?
Yeah. ana maamuzi yanayoegemea upande mmoja(Biasness)
 
Habari muda wadau bila shaka mko salama na wenye udhaifu Mungu awape wepesi
Leo nawaletea mkasa ambao uliniumiza Sana Moyo .
Miaka kadhaa iliopita nilikuepo mkoani Mbeya
Shughuli zangu zilikua ufugaji samaki na kilimo cha strawberry
Nikakutana na mdau mmoja hapa jamii forum akahitaji mbegu za samaki

Tukakubaliana gharama nikaandaa mzigo nikapanda Costa mpk Uyole hapo nakea kiwira
Na hapo uyole ndo sehem tuopatana kuonana
Badda ya kufika na kumpa Taarifa akasema sawa nakuja
Nilikaa kwa masaa manne hakupokea tena simu zangu wala kujibu ujumbe nika mcheki WhatsApp yupo online namtumia ujumbe unatia bluetick lkn hajibu. Kwa kifupi alinipotezea nilipata hasara ya laki moja lkn nikasema sawa
Nilipanga kulipa kisasi japo kwa kuchelewa lkn niliendelea kumtafuta hakunijibu
Baada ya miezi sita nikampigia kwa namba nyengine nikamuuliza kama naweza kupata mbegu za samaki akasema zipo
Nilimuuliza kwasababu ktk kipindi alichonitia hasara niligundua naye ni mtu anaefanya shughuli kama ya kwangu kwahio aliamua kunikomoa hakua na nia ya kuhitaji mbegu hizo

Kwahio baada ya kumuuliza akajibu ndio nikaweka oda ya vifaranga vya samaki 3000 . Sawa na laki tisa(900,000)
Nikamwambia nipo kyela nikamtumia 15,000 hii kwaajili ya mifuko ya kubebea hao viumbe. Hapo ndo akazidi kuingia laini
Nkamwambia akodishe Noah ntalipa Mimi ili mbegu hizo na chakula cha kuanzia vikae vzr akasema sawa
Siku inayofuata saa saa tisa mchana akanipa Taarifa kua washaanza Safari
Na gharama za gari nilishazikubali kwa maelewano wakifika ntalipa pesa yao
Sasa ili kuthibitisha kuwa ni kweli anakuja nikamuambia ukifika kiwira Kuna bahasha yangu utaichukua uje nayo akasema sawa
Nikaandaa karatasi iliosemeka hivi

MIMI ni yule jamaa ulieniambia unataka mbegu za samaki nkaja uyole halafu ukanipotezea nawewe onja machungu .

Nikaweka ndani ya bahasha nikampa kijana akaenda nayo mpk kwenye soko la kiwira maarufu Tandale nikampa namba ya simu wakawasiliana
Walivyofika akamkabidhi na gari ikaondoka kulekekea kyela

Walivyofika kyela nikamwambia nendeni pale kwenye mtaa ambao Kuna mashine za kukoboa mpunga Kuna dogo anakuja kiwachukua
Na hapo muda ulikua ushaenda Sana.

Nikazima simu kwanza baada ya dk 5 wakampigia yule kulijana aliewapa bahasha hakupokea
Nikawasha simu yangu nikawapigia jamaa alivyopokea tu nkamwambia bro ile bahasha unayo? Akajibu ndio nikamwambia fungua uisome inamaelekezo
Baada ya dk 2 jamaa ananipigia simu analia
Hapo roho yangu ikawa nyeupeee
Nina kisa kimoja mkuu
 
Uko sahihi endapo kuipata laki mbili kwako ww ni rahisi yan sio kazi ngumu. Lakini hebu jiweke ktk nafasi ya e.g. kijana msomi hana chanzo cha kipato au ajira inayoeleweka. Anabangaiza huku na kule (Hustler) na ameweza kujinyima akadunduliza hadi imefika 2k. Atasononeka mno (anaweza hata kutoa machozi) akikumbuka sulba alizopitia kufikia kiasi hicho halafu sasa eti lijamaa fulani kwa ulaghai linazichukua kiulaini hivo. Hiyo sio sawa. Sasa roho itasuuzikaje (usinambie habari za mwachie Mungu) kama sio kwa kulipa kisasi kitu ambacho ni sahihi na ni stahili yake?? Tukemee na Tusilee uovu. Ukilipa kisasi tena kwa mafanikio 100% + utaona raha yake. We jaribu uone.
SURE MKUU
 
Kama mtu hajali maumivu yako kwa nini wewe ujali ya kwake?

We jamaa ni mbinafsi una roho mbaya kama huyo jamaa wa kwanza.

Hujaona unyama wa Muuza vifaranga wa kwanza unamsema wa pili?
Mkuu kuna kusahau, ndivyo tulivyoumbwa.

Sasa mtu miezi 6 mwamba hasahau aiee
 
Mmh; Sipati picha kwamba umeenda shambani (Bishara) na ukapanda mbegu (Ulaghai na Ubabe) halafu eti unasahau kukumbuka kwamba kuna siku utaenda kuvuna(Utalipizwa kisasi).
Basi tumetofautiana mkuu, binafsi sinaga visasi vya muda mrefu.
 
Back
Top Bottom