Muro kakosea kwenda Yanga, Yanga nayo imekosea kumpata Muro

kalagabaho

wewe umetumwa nini? mbona huongelei timu yenu mbovu ni hakuna mfano kinacho kutekenya kitu gani we manji au sanga?. muro yuko makini sana ndo maana kaitwa mkurugenzi wa habari ww ulitaka aongelee simba?
 
Last edited by a moderator:
ngasa alikubaliana na nani mambo hayo?...naona hujui hata kinachojadiliwa hapa! upeo wako umegota kwenye tope la uwanja wenu
Wewe nawe unarukia tu kama mmama aliyebanwa na pichu!! Hujuikutumia alama za kuuliza wewe? Hapo unaona kuna mahali nimesema alikubaliana na mtu? Jitahidi kuelewa maana ya kutumia hizi alama?????, !!! Usiwe unakurupuka tu!!
 
wewe umetumwa nini? mbona huongelei timu yenu mbovu ni hakuna mfano kinacho kutekenya kitu gani we manji au sanga?. muro yuko makini sana ndo maana kaitwa mkurugenzi wa habari ww ulitaka aongelee simba?
Umeona mkuu! Haka kajamaa ka-mikia kana shida sana kanataka tukubaliane na maelezo ya kenyewe!!
 
Kalamzuvendi

Huna hoja wewe unaingiza kwenye timu mambo binafsi
ya mtu. Mbona yanga mnaliwa mitaani huku hatusemi, au unafanya watu hawajui yanga mlichofanyana Mbeya kwa kulala mzungu wa nne kwenye kitanda mimoja?

Matokeo yake kocha wa watu mzungu Saintf hajui kuweka siri akabwabwaja hadharani mkamtimua kwa kuona aibu.
 
Last edited by a moderator:
Masuke


Me katika hili sioni haja ya kumtetea Ngassa. Yeye alikubaliana na Simba aongeze mwaka mmoja na wakampa 30M, then baada ya hapo Yanga nao wakamfuata akawakubalia, maneno yakasikika na Simba wakasema Ngassa hawezi kwenda kuchezea timu nyingine kwa kuwa tumeshakubaliana nae atacheza hapa kwa mwaka mwingine mmoja.

Kusikia hivyo Yanga wakakaa nae na kumhoji kama kweli alikubaliana na Simba na alichukua pesa zao? Ngassa akakataa kabisa kuwa hakuchukua pesa ya Simba. Basi Yanga wakakubaliana nae wakampa chake akasaini.

Baadae Simba wakafungua mashtaka TFF na walipopeleka vielelezo kwenye kamati ya maadili na hadhi ya wachezaji ikabainika kweli Ngassa alichukua pesa za Simba 30M. Wakamuamuru alipe pamoja na faini ya 50% ndo maana ikafika 45M wakamfungia na mechi 6. Issue ikawa atalipaje? Yanga wao wakasema hawahusiki na deni la Ngassa.

Tena kama mtakumbuka ni huyuhuyu Ngassa wakati analipa zile pesa alisema kuwa hajalipiwa na mtu yeyote bali yeye ana biashara zake hivyo amejilipia mwenyewe ila kwa kuwa ni pesa nyingi anawaomba wana Yanga wamsaidie kupunguza machungu kwa kumchangia kwenye Account yake ya Bank ya CRDB na akaitaja kabisa,

Eti juzi kafunga magoli mawili anasingizia kuwa ana uwezo mkubwa wa kufunga na atafanya hivyo kama Yanga watamlipia deni. Anajikanyagnyaga Tu.
 
Last edited by a moderator:
Masikrodinga

Anacholalamikia Ngasa kwa sasa ni kwa nini walikuwa wanakata hela kwenye mshahara wake halafu hawapeleki benki mpaka ikasababisha makato yapande kutoka milioni moja hadi milioni mbili kufidia muda ambao hela hazikupelekwa.
 
Last edited by a moderator:
hivi nani anamjua msemaji wa man u, real Madrid arsenal na timu nyengine ulaya? nianze hapa kwanza
 
Job K

Nakupa saluti mkuu mtu ukope mwenyewe tena kwa ujinga wako wakutofikiri kabla ya kutenda then wanachama tuje kukulipia.
 
Last edited by a moderator:
Job K

Alikopa kuilipa Simba sh million 45.So hakununua hata pipi.
 
Last edited by a moderator:
Wale wawili waliowashitaki FIFA mmewalipa milioni mia na ushee zao?

Mosoti anawadai nyie!!! Na hivi mechi zenu mnaingiza kiduchu sijui mtatoa wapi hela ya kumlipa!!
 
Job K

Huna haja ya kutukana Watanzania wote, hiyo imetokea kwa mwanayanga anaeipenda timu yake hata kuwa tayari kuichezea bureeee na kuacha mafwedha ya Simba na Elmereck ya Sudan.
 
Last edited by a moderator:
Anacholalamikia Ngasa kwa sasa ni kwa nini walikuwa wanakata hela kwenye mshahara wake halafu hawapeleki benki mpaka ikasababisha makato yapande kutoka milioni moja hadi milioni mbili kufidia muda ambao hela hazikupelekwa.

Sawa Masuke, nakuelewa vizuri sana. Lakini katika players ambao hawana weledi huyu dogo ni namba moja. Me naamini angekaa vizuri na uongozi wa Yanga kuelezea tatizo lake la deni la CRDB wangemshughulikia tu coz liko wazi na nyaraka lazima zipo kuwa fedha hazikupelekwa Bank, zile ambazo yeye Ngassa alikatwa na Bank hazikwenda ina maana kuna maofisa wa Yanga (naamini ni wale ambao wameondolewa) walifanya ubadhirifu, Yanga wangefanya utaratibu wa kuzilipa CRDB bil ya kumuathiri mchezaji. Naamini Yanga ni taasisi kubwa wasingeshindwa kufanya hivyo. Hata hivyo inashangaza kwa kuwa hatujui walikubaliana vp, mara nyingi inakuwaga mshahara wa Ngassa ungekuwa unapitia CRDB wanachukua chao then wanamwachia chake kwenye Account, sasa je inamaana kwa kipindi chote hicho hata yeye Ngassa alikuwa halipwi mshahara? Na kwa nn CRDB wakae kimya mwaka mzima? Siamini kitengo cha mikopo cha Bank yeyote hapa nchini kinaweza kukaa kimya kwa muda wote huo bila ya pesa yao kurudishwa.

Turudi kwa Ngassa, je kulikuwa kuna haja gani ya yeye kutamka kuwa ana uwezo mkubwa wa kufunga isipokuwa deni ndo linamsumbua, inamaana alisubiri afunge ndipo ayaseme haya? Ngassa hatakiwi kuonewa huruma.

Hata hivyo sakata hili linafichua siri nyingi kuwa mfumo wa ulipaji wa mishahara ya wachezaji lipo shaghalabaghala sana Tz, hivi wanakatwa kodi? wanalipiwa mifuko ya hifadhi (NSSF, LAPF n.k)
 
hivi nani anamjua msemaji wa man u, real Madrid arsenal na timu nyengine ulaya? nianze hapa kwanza

Mi simjui. hata wa Simba simjui ila wa Yanga tega sikio kwenye redio kila siku kwenye kipindi cha michezo utamsikia anaunguruma tuu!
 
Jodoki Kalimilo

Kumbukumbu nilizonazo mchezaji ndie eliyekua wa mwanzo kwenda kwenye vyombo vya habari kama angekua anajua mkopo ni siri yake na taratibu nzima za mkopo wala asingelialia kwenye media angekubali utaratibu ufatwe yeye aendelee kuomba hisani ya mdhamini ambae ni klabu.

Muro alikua anaelezea maswala ya taratibu za mkopo wala hakukua na shida mchezaji alichukulia msaada au hisani ni jambo la kisheria, ajifunze sasa na wachezaji wengine wajifunze. Sio kuingia kwenye wajibu leo halafu kesho kwenye kuutimiza inakua tabu.
 
Last edited by a moderator:
Kalamzuvendi

Hili jambo niliwahi lisikia, na likaingia mpaka timu ya taifa beki takribani zote nasikia zilipata hisani ya kocha mwenye asili ya "Asia " aliekua akipumzika.
 
Last edited by a moderator:
Mi simjui. hata wa Simba simjui ila wa Yanga tega sikio kwenye redio kila siku kwenye kipindi cha michezo utamsikia anaunguruma tuu!

Muro kaanza usemaji juzi tu lakini kama ingekuwa ni idadi ya post za JF angekuwa amemzidi Masau Bwire au Thobias Kifaru
 
Syzygus

Mkuu unategemea embe dodo kwenye Mfenesi. Ukitaka matusi, kupiga marefa, kutojua sheria za mikataba, sifa za kijinga utazipata Yanga.
 
Last edited by a moderator:
Wewe na Simba wote ni 'mbumbumbu' (Rage).

Mbumbumbu hayo ni maneno binafsi ya rage lakini hakujua kuwa waliomuweka madarakani ndiyo waliomuondoa.
Sikitiko kwa wenzetu ambao wanajipa moyo kuwa ni werevu wakati Manji anawatukana matusi makubwa kwa vitendo vyake.
Manji amesogeza mbele uchaguzi mkuu, yanga imefyata mkia.
Manjia amekataa mechi ya leo isirushwe luningani bila sababu, yanga mmefyata.
Anaajiri na kusajiri hata mafundi viatu kutoka Brazil anavyotaka, yanga mmeufyata.
Jipimeni wenyewe mjipe jina mnalostahi maana hata mbumbumbu kwenu bado ni sifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…