Musa Hassan 'Mgosi' ammwagia sifa Obrey Chirwa

Musa Hassan 'Mgosi' ammwagia sifa Obrey Chirwa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
CHIRWA VS ALGERIA.JPG

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi, amesema kuwa kwenye Ligi Kuu Bara mshambuliaji mbishi uwanjani ni Obrey Chirwa wa Yanga.

Chirwa ambaye amekuwa tishio katika kufunga, mpaka sasa ana mabao sita yakiwa mawili nyuma ya anayeongoza ambaye ni Emmanuel Okwi wa Simba.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Global TV Online, Mgosi alisema hata akichezewa faulo bado mchezaji huyo amekuwa hakati tamaa kiasi cha kuwafanya mabeki wengi kumuogopa.

“Enzi zangu mimi hata ukinichezea rafu vipi, ndiyo kwanza nakuja kwani straika ukigongwa kidogo halafu ukahama upande unampa kichwa yule beki kuwa kakuweza.

“Katika ligi kuu, kwa sasa straika nunda ni Chirwa kwani ndiye namuona hata ukimchezea rafu vipi bado atakufuata, mwingine ni John Bocco,” alisema Mgosi.
Mgosi alikuwa mmoja wa washambuliaji matata na wasumbufu wanapokuwa uwanjani.
Mshambuliaji huyo aliyetokea Mtibwa Sugar kutua Simba, alikuwa akihofiwa sana na mashabiki wa Yanga kipindi timu hizo zinapokutana.
 
mgosi anaongea sana juzi juzi alikuwa anamshauri Okwi namna ya kufunga mabao akiwa mkoani sijui kwanini alikuwa hatumii mbinu hizo kwani msimu wa mwisho kabla hajatundika daluga alifunga bao moja tu
 
mgosi anaongea sana juzi juzi alikuwa anamshauri Okwi namna ya kufunga mabao akiwa mkoani sijui kwanini alikuwa hatumii mbinu hizo kwani msimu wa mwisho kabla hajatundika daluga alifunga bao moja tu

mbona unamhukume kwa kufunga bao 1 wakati jua limezama, hukumbuki wakati wake alikuwa anafanyaje?
Hata hivyo ushauri anaweza toa yeyote ndio maana mashabiki wanampangia kikosi kocha mwenye vyeti
 
Wabongo bwana, hivi angeishia kusema ukweli wa moyo wake asingeeleweka hadi akaamua asawazishe na upande wa simba kwa namna ya uongo?
 
Back
Top Bottom