Museveni aeleza kutaka kujua kilichokwama katika mpango wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Tanga

Museveni aeleza kutaka kujua kilichokwama katika mpango wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Tanga

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema atafuatilia kujua kilichotokea kuhusu mpango uliopendekezwa wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote (Dangote Oil Refinery) mjini Tanga, Tanzania.

Museveni amesema mazungumzo kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho yalikuwa yamefanyika kati yake na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Kenya, William Ruto, lakini mpango huo ulikumbwa na changamoto.

Alisema, “Kulikuwa na baadhi ya matatizo, sijui nini kilitokea. Kwa hiyo nataka kwanza kufuatilia hilo,” akieleza kuwa anataka kubaini chanzo cha changamoto hizo kabla Uganda haijafikiria kuwekeza katika kiwanda kingine cha kusafisha mafuta katika ukanda huo.

Museveni alitoa kauli hiyo Jumatano, Septemba 30, 2026, wakati wa hafla ya kuanza ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote East Africa Petroleum Refinery mjini Lamu, Kenya.

Lamu ilichaguliwa kuwa eneo la ujenzi wa kiwanda hicho baada ya Tanga kutajwa awali kama eneo lililokuwa likizingatiwa. Mradi wa Lamu unatarajiwa kuhusisha uwekezaji wa takribani Sh40 trilioni, pamoja na uwekezaji katika sekta ya umeme, hali itakayofanya thamani ya uwekezaji wote kufikia zaidi ya Sh100 trilioni.

Mradi huo umetajwa kuwa miongoni mwa uwekezaji mkubwa zaidi wa sekta binafsi nchini Kenya. Kampuni ya Dangote inatarajiwa kumiliki hisa asilimia 70, huku serikali ya Kenya na washirika wake wakimiliki asilimia 30 iliyobaki.
 
Waarabu hawawezi kukubali jambo Hilo la kujenga kiwanda cha mafuta tz
 
Amchek Samuya, yeye ndo mwenye majibu yote

Samuya hoyeeeeeeeeeeeeee 😂
 
Samuya alilewa na kumbato la Chivayo fursa ikaondoka
 
Back
Top Bottom