DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuungana kijeshi na kimkakati ili kulinda usalama wa bara hili, akidai kuwa ingawa mataifa makubwa kama Marekani yana nguvu kubwa angani na baharini, Afrika inaweza kuwa na faida kubwa katika vita vya nchi kavu.
Akizungumza na vijana nchini Uganda jana, Rais Museveni ameeleza kuwa Marekani inatawala nyanja mbalimbali za kijeshi kama baharini, angani na nchi kavu. Amesema kuwa Afrika iko nyuma katika nyanja hizo, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa baadaye wa bara hili.
Rais Museveni amekosoa viongozi wa zamani wa Afrika, akidai kuwa baadhi yao walipendelea kubaki kuwa "samaki wakubwa kwenye kidimbwi kidogo" badala ya kuunganisha nguvu. Amesema kukosekana kwa umoja wa kijeshi na rasilimali kunafanya Afrika kushindwa kujenga uwezo katika nyanja za anga na bahari.